Elections 2010 Ngoma CCM, CHADEMA Arusha bado mbichi

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Ngoma CCM, CHADEMA Arusha bado mbichi


*Mbunge kutoka Tanga ashiriki tena uchaguzi
*CHADEMA waususia, wasema hawashiriki uhuni


Na Glory Mhiliwa, Arusha
MBUNGE wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga kupitia CCM, Bi. Mary Chatanda jana alizidi kuleta mvutano wa
kisiasa baada ya kushiriki kwenye uchaguzi Jumuia ya Serikali za Mitaa Tanzania (ALAT) mkoa wa Arusha na kusababisha wajumbe wa CHADEMA kuususia.

Hii ni mara pili kwa mbunge huyo kupitia Mkoa wa Tanga kuzua tafrani kama hiyo baada ya kushiriki uchaguzi wa meya na naibu wake katika Manipaa ya Arusha, hatua iliyopingwa na madiwani wa CHADEMA, huku CCM wakisisitiza kuwa ni halali kufanya hivyo.

Kutokana na kitendo cha Bi. Chatanda ambaye pia ni Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, wajumbe wa CHADEMA waliondoka katika mkutano huo wakisema wasingewe kushiriki kuchakachua sheria kwa kuchagua wajumbe wa ALAT, huku akimshirikishwa mjumbe haramu.

Hata hivyo, vigogo wa CCM ambao ni wabunge mkoani Arusha na wajumbe wa kikao hicho, Bw. Edward Lowassa (Monduli), Lekule Laizer (Longido), Bw. Goodluck Ole Medeye (Arumeru Magharibi), Bw. Jeremiah Sumari (Arumeru Mashariki) pamoja na Meya anayelalamikiwa wa Manispaa ya Arusha, Bw. Gaudence Lyimo hawakuhudhuria.

Kikao hicho kiliendeshwa na mwenyekiti wa muda, Bw. Ismail Katamboi, ambaye ni diwani wa Kata ya Kisongo, ambaye alisema kukuwapo kwa wajumbe sita wa CHADEMA siyo sababu ya kuwazuia kuendelea na uchaguzi huo.

Akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi, Mbunge wa Arusha Mjini, Bw. Godbles Lema alisema, "Sisi tumetoka ndani ya kikao hiki kwa sababu ya huyu Bi. Mary Chatanda ambaye ni mbunge wa Tanga, iweje leo apige kura za kuchagua wawakilishi wa mkoa Arusha," alisema Lema.

Alisema kuwa kinachofanyika sasa kwa Mkoa wa Arusha ni uhuni na siyo demokrasia, hivyo bora wawaachie wenye chama tawala wafanye kila wanachotaka, ila wao hawako
tayari kushiriki kuchakachua sheria kwa kuchagua wajumbe, huku wakimshirikisha mjumbe haramu.

Kikao hicho kilitakiwa kuchagua, mwakilishi ALAT Taifa, Mwenyekiti na makamu wake mkoa, katibu na Mweka hazina.

Pamoja na Bw. Lema wajumbe wengine wa CHADEMA waliosusa uchaguzi huo ni Bi. Cecilia Paleso, Diwani Viti Maalum- Karatu, Lazaro Maasai, Mwenyekiti Halmashauri ya Karatu, Joyce Mukya, Mbunge Viti maalumu Arusha, Winner Kitembe, Diwani wa Karatu na Mchungaji Israel Natse ambaye ni Mbunge Karatu.

Kikao hicho kilitakiwa kuwa na wajumbe halali 40, lakini baada ya wajumbe sita wa CHADEMA kutoka na wengine ambao hawakuhudhuria, walibaki 28 wa CCM ambao waliendelea, na kumchagua Bw. Godfrey Majola, mwenyekiti wa Halmashauri ya Meru kuwa Mwenyekiti wa ALAT mkoa.

Msuguano huo umeendelea kutoka mkoani Arusha wakati vumbi lililotimka kutokana na polisi kuzima maandamano wa CHADEMA kupinga uchaguzi wa meya likiwa halitatua.

Katika tukio hilo, watu watatu waliripotiwa kuuawa na polisi kwa risasi na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa, na chama hicho kimendaa mazishi ya 'kitaifa' yatakayofanyika katika viwanja vya NMC kesho.

Katika hatua nyingine, Anneth Kagenda anaripoti kuwa Baraza la Wazee wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, limewataka viongozi wa dini kukaa kimya na kutojiingiza kwenye siasa kwa kutoa msimamo kuhusu suala hilo la Arusha kwa madai kuwa kufanya hivyo kunaweza kuleta maafa makubwa nchini.

Hayo yalisemwa jijini Dar es Salaam jana, na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Bw. Mohamed Mtulia wakati akitoa tamko la kukemea vurugu za Mkoani Arusha zilizotokea Januari 5, 2011.

Alisema kuwa wamesikitishwa na kauli hizo ambazo zinaashiria matakwa ya kidini katika masuala ya kisiasa, kwa kuwa jambo hilo likiachiwa litaitumbukiza nchi katika machafuko ya kidini.

"Sisi wazee tunawaomba maaskofu na viongozi wengine wote wa kidini kuiacha siasa kwa wanasiasa, kwani kitendo cha maaskofu wa Arusha kukataa kumtambua Meya wa Jiji hilo ambaye pia amekataliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinaleta wasiwasi wa kujitokeza viongozi wengine wa kidini na kujipa mamlaka ya kutowatambua viongozi wasiowakubali kama walivyofanya maaskofu hao," alisema Katibu Mtulia.

Alisema kuwa wanaamini kwamba Dkt. Willibrod Slaa aligombea urais katika uchaguzi uliopita wa mwaka 2010 na kama angekuwa 'chaguo la Mungu' basi angekuwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa nchi, na bila shaka asingeridhia Mwenyekiti au Katibu wa chama chochote cha siasa apinge kwa maneno na vitendo, amri halali za mamlaka za kisheria zilizoundwa kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi.

"Pamoja na kusikitishwa na nguvu iliyotumika ni wajibu wetu kuitafakari nguvu hiyo na je, ilikuwa lazima itumike au haikuwa lazima, hivi kikundi cha raia kinachoelekea kituo cha polisi kwa ajili ya kuwatoa watuhumiwa kwa nguvu kimedhamilia nini, na je, jamii inafahamu nguvu waliyonayo raia hao na wanaowaunga mkono?" alihoji Bw. Mtulia.

Aidha alisema kuwa wazee hao wanaamini kuwa endapo uvamizi wa kituo cha polisi ambacho kinawahifadhi watuhumiwa, pamoja na silaha na nyaraka muhimu ungefanikiwa na silaha zikaangukia mikononi mwa raia wa kawaida wasio na nia njema, kungekuwa na uwezekano mkubwa wa kutumika vibaya na kuleta madhara makubwa.

"Ni dhahiri kuwa waliokusudia kuvamia kituo hicho wangefanikiwa na kupora silaha ili zisaidie kuwatoa watuhumiwa, hali ingekuwa mbaya sana na pia kama angalizo la Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) lingefuatwa, yaliyotokea yasingetokea," alisema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza hilo Bw. Athuman Mwinyimvua alisema kuwa wanatoa pole kwa wale wote walioathiriwa na vurugu zile kwa kupoteza mali huku wengine wakipoteza maisha na wale waliojeruhiwa.




25 Maoni:

blank.gif

Anonymous said... Mohamed Mtulia, acha kuongea upuuzi kama huu wakati raia wasio na hatia wameuawa kwa uroho wa madaraka ya viongozi wa CCM. Unaleta dhana y akufikirika kuwa eti CHADEMA walikwenda kuvamia kituo cha polisi ili wapore silaha? Hayo ni mawazo mgando. Halafu kumbuka wewe huna hadhi ya kuwaelekeza maaskofu na mapadre ni nini cha kufanya. Wewe na mashekh wenzako fanyeni yenu ya Koran misikitini, yanayowahusu wa Biblia waachieni wenyewe. Excuse me!
January 10, 2011 8:34 PM
blank.gif

Anonymous said... RIP nyie wazee njaa. Majina yote yanaja ulikana ni dini gani? Hivi kwa nini hatuna shule za maana au hospital za maana za kiislam? angalia vyuo vikuu vingapi, huduma ngapi zinazotolewa na waislam. Badala ya kujenga shule, hospital mnajenga misikiti tena barabani!!!! Ujinga muda wenu wa kufikiri umekwisha sanda zinawasubiri. Hivi da ndo kuna wazee?? kazi kunywa kahawa basi. Narudia RIP
January 10, 2011 8:39 PM
blank.gif

Anonymous said... hivi hawa niwazee au uchwala msome madarasa hayata wakomboa ukisikia tu jina limeanzia na mzee wa barakashee utajua nipumbu tu zinazo fuata ooo udini hivi hamna hoja wa kristu wangekuwa wadini wangewachagua hawa ndg zenu wanaolipeleke taifa kudidimia kiuchumi mjue kuongoza hamwezi ni jaziba ya udini tu kila kukicha.
January 10, 2011 9:08 PM
blank.gif

Anonymous said... Kwa kweli kwa hili serkali ya sisiemu haiwezi kukwepa lawama.wamaona kabisa kuwa kuna tatizo bado wanaendelea kuruhusu chaguzi za namna hiyo kufanyika,wanataka wao tu ndio wawe madarakani hata kama hawakuwekwa na nguvu ya wananchi.kwani uchaguzi ukirudiwa Arusha kwa uangalizi na kufuata sheria zote za uchaguzi na ikaonekana ccm wameshida chadema haiwezi lalamika.lakini kwa uroho wa madaraka wanapindisha sheria na kuonekana wameshinda,pia hembu liwekeni wazi nani anaestahili kupiga kura ktk kumchagua meya wa jiji???mtu mbaya sana anaeharibu amani nchini ni pamoja na Yusufu Makamba,pia hata jeshi la polisi,huyu mama pia mbunge wa tanga aangaliwe pia,
January 10, 2011 9:38 PM
blank.gif

Anonymous said... Hawa ndio wazee wanaomshauri Rais na kula mapochopocho ya Ikulu. Wanafikiri TZ ni mali yao. Au wanafikiri wangealikwa kwenda kula maharagwe. Kwa taarifa yenu hakuna maharagwe ni majonzi. Huo udini ni nyinyi mnao kama kawaida yenu, na ndio maana nchi zote zenye waislam ni matatizo matutpu. Kama sio kuwasaidia kwenye Elimu sijui mngefa je. Mnachukua kuvuli cha udini muanze kufunga mabomu kiunoni na kutumia makwanja yenu yaliyoko humo msikitini.
January 10, 2011 9:49 PM
blank.gif

Anonymous said... Chadema (Chama Cha Demokrasia na Maandamano) Nyie ndio wa kulaumiwa kwa nini hamkutii amri halali ya kutokuandamana iliyotolewa na IGP>. Nyie ndio mmesababisha mambo yote haya. Namsihi Hakimu awafunge wote walioshutakiwa kwa kutotii sheria miaka 10 kila Mmoja nyie ndio mlisababisha watu wakauawa kama mngeenda tu kwenye mkutano kistaarabu yote hayao yasingetokea lakaini mkaandamana kinyime cha sheria mnataka mfnaye mambo yenu manavyotaka nyinyi ili jumuia ya kimataifa iwaone CCm wabaya nyie ndio wabaya. Haya na hao maaskofu nduguze Slaa hawamtambui Meyawa Arusha ni maajabu wao ni kina nanai au walitaka Slaa awe rais ili nchi iwe ya kikirito hatukubali siye waislamu
January 10, 2011 9:49 PM
blank.gif

pETRO eUSEBIUS mSELEWA said... Chatandaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaeeeeeeeeeeeeeeee! Ondooooooooooooooooooookaaaaaaaa kwa jina la Yesu!
January 10, 2011 9:50 PM
blank.gif

Anonymous said... Huyo mama Chatanda damu iliomwagika imwangukie yeye,na akatubu makosa hayo vinginevyo dhamira itamshtaki,
January 10, 2011 9:59 PM
blank.gif

Anonymous said... Chatanda kaombe radhi watakunyang'anya ukristo wako. Kumbuka yaliowafika wakristo wa sumbawanga walioikataa Chadema Kanisa limewafanya nini? Umemsikia Malecela alivyokuita mtovu wa nidhamu.

Hivi kwa nini chama cha CHADEMA kisifutwe kwa kuubeba udini. Kwa nini Mbowe na Padre Slaa wasijiuzulu kwa kushindwa kuwachunga kondoo zao na kuwasabibishia maafa ambayo yanaepukika.

Balaa la umasikini la Nchi hii limeletwa na Nyerere. Tuwe w Kweli. Ilifikia watu wanakwenda uchi, wakalazimishwa kula sembe la Yanga, wakakosa hata sabuni ya kuogea na dawa ya meno,tukawa tutanunua chakula kwa kadi na kiwango alichoweka yeye.Maovu matupu. Watu kuwekwa ndani bila ya kufikishwa mahakamani. Ubabe mtupu. Lakini hatawasikia Maaskofu kulaani au kukosoa utawala huwo. Ni Unafiki wa kikatoliki na Udini tu ndio uliotawala nchi hii hivi sasa, Nayote kwa sababu CHADEMA chama cha Maaskofu kimeshindwa uchaguzi na kitaendelea kushindwa maisha. Kwa vile dhamira zao zinajuulikana sasa na kila mpenda amani
January 10, 2011 10:18 PM
blank.gif

Anonymous said... Nimependa maoni yoote leo ah. Ntalala kwa raha sana.
January 10, 2011 10:20 PM
blank.gif

Anonymous said... sasa nimeelewa kwa nini tunaambiwa viongozi wa dini wasijiingize kwenye siasa. Wakitaka wavue majoho waingie kwenye ulingo.

Matoeo ni haya hapa.soma wachangiaji.Mgogoro wa Chadema na CCM umekiwa matusi baina ya wakristo na waislamu. Vitone vya matusi aina hii vinaweza kuleta mfarakano usiotegemewa kwenye jamii.

Na hili limekuja baada ya viongozi wa dini kuanza kuleta chokochoko au kuegemea upande mmoja.

hatari mti na macho
January 10, 2011 10:25 PM
blank.gif

Anonymous said... Hili limekuja baada ya CCM kutaka kwa nguvu kutawala bila kufuata kanuni. Ntu yeyote anao uhuru wa kuhimiza amani; na zaidi sana viongozi wa dini. Maoni ya kuleta amani yasichukuliwe kama maoni ya udini. Udini sasa unaletwa na Chatanda na mashekh wanaojibu maaskofu kana kwamba hawapaswi kukemea maovu ili kudumisha amani nchini. Tunapotoa maoni tufikirie kwa kichwa si kwa tumbo!
January 10, 2011 10:36 PM
blank.gif

Anonymous said... HIVI NYIE WAFUASI WA CHADEMA MMEKUWA WEHU? WENGINE WAKITOA MAONI MNAWATUKANA NA KUWAKEBEHI LAKINI MAASKOFU WAKISEMA SAWA,HUO NI UJINGA WA KUPINDUKIA,KAMA MAASKOFU WAKISEMA NI HAKI YAO KUTOA MAONI,KAMA WAISLAMU WA MKOA WA ARUSHA WALISEMA NI HAKI YAO YA KUTOA MAONI NA KAMA HAO WAZEE WA DAR-ES-SALAAM WALISEMA PIA NI HAKI YAO YA KUTOA MAONI,LEO KUNA GAZETI LINASEMA MWANZA KIKUNDI FULANI CHA WATU WANATAKA KIKWETE AJIUZULU NAO NI HAKI YAO KUTOA MAONI,NYIE MKISHA ONA JINA LA KIISLAMU TU TAYARI VICHAA VINAWAPANDA. KOMENI WAACHIENI WENYE MAONI YAO WATOE.
January 10, 2011 10:38 PM
blank.gif

Anonymous said... Wewe mbunge wa Arusha unaoongoza kihuni hapo,waeleze watu sheria za nchi zinasemaje kuhusu diwani wa kuteuliwa kutoka katika vyama na haki zake sio kila siku kuleta migongano isiyo na tija kwa jiji letu la Arusha. weka sheria wazi inasemaje? kutuambia tu huyu ni mtu wa Tanga wakati ni katibu wa CCM wa Arusha na anaishi Arusha haitoshi,wewe kwenu ni Moshi na sio Arusha basi nenda kwenu Moshi.
January 10, 2011 10:45 PM
blank.gif

Anonymous said... Mary Chatanda ni muislamu? Acha ujuha wewe, watu wanaotoa maoni yao, nao piani haki yao kufanya hivyo. Upo hapo!
January 10, 2011 10:59 PM
blank.gif

Anonymous said... MNALOLILETEA MZAHA LEO KWA KUANDIKA UTUMBO KWA KUTAKA MJIFURAHISHE, KESHO LITAWALIZA. NA MTALIA NYOTE BILA KUJALI KUWA WANA CCM AU CHADEMA. NG'ANG'ANIENI TU MADARAKA DAWA YA WOTE SASA IKOJIKONI. NA TUKANENI SANA WACHUNGAJI TENA KWANGUVU ZOTE, CHAMOTO KITAKUJA IKIWA TU NIDHAMU YA NNCHI HAITARUDISHWA NA VIONGOZI WA CCM WENYE UROHO WA MADARAKA. NANYI CHADEMA ACHENI MAMBO HAYA YA KUPIGANIA UKOMBOZI WA MTANZANIA, KWANI KWASASA SI WAKATI WAKE, MTAJICHOSHA BURE NA HAKUNA LITAKALOSAIDIA, MWAJUA FIKA KUWA SERIKALI YA TZ IMOMIKONONI MWA KIKWETE NA AMEMILIKI HATA JESHI LA POLISI NA KWAO SASA KUUWA WATANZANIA WA FUASI WA VYAMA VYA UPINZANI NI KUTAKA WAPANDISHWE VYEO KILA MTU ANAJUA KWA SERA SASA YA CCM NI KUUWA WATANZANIA WASIO WAFUASI WA CCM. CHADEMA TULIENI WAACHIENI CCM WAENDELEE KULA MPAKA WAPASUKE
January 10, 2011 11:10 PM
blank.gif

Kiduku said... Kwanini CCM wanaogopa maandano kuliko mahakama? Jibu ni rahisi, mahakama zetu sio huru, anayeteua majaji woooote nchini ni mwenyekiti wao wa CCM taifa, hivyo ni sawa na kesi ya nyani kula mahindi kumpelekea ngedere akaamue. Maandamano yanaogopewa na serikali zote kandamizi duniani, maana ni maandamano pekee nyenye nguvu ya kukusanya watu wanyonge ili waende wakakusanyike pahala ili wajulishwe ukweli halisi wa mambo, matukio na ubaya wa watawala na hatua za kuchukua.

Kamwe msikimbilie mahakamani, hamtapata kitu huko, kimbilieni maandamano na mikutano ya hadhara sio mahakamani, ona kesi ya mgombea binafsi ya mch. Mtikila ilivyoamuliwa na mahakama ya juu, ona kesi ya Ditopile, ona kesi ya zombe, ona dowans, ona kesi ya mzee wa vijisenti ya kuua, ona, ona, ona,.........

Ndiyo maana makamba na wenzake hawaishi kusema muende mahakamani ili mkakatwe shigo zenu kwa panga butu ya kijani ya mwenyekiti wao wa CCM.

Maandamano ndiyo mwiba wa madhalimu, andamaneni hadi mfe wote, sio kwenda mahakamani mtavuliwa huko kwa nyavu zenye rangi ya kijani ndiyo maana wanawasakizia mahakamani. Tuchukue uwamuzi mgumu hata ikididi kupoteza maisha ili kuzikomboa njia kuu za demokrasia na utawala wa sheria ili watu tuishi kwa amani na utulivu wa kweli
January 10, 2011 11:35 PM
blank.gif

Anonymous said... Hawa wazee wa Dar siku zote tunawajua, wameshapungukiwa hekima!!! Mawazo yao ni yaleyale ya chama kimoja. Binafsi siwezi kuwashangaaa, ndio hao waliomshangilia Rais wakati anatishia wafanyakazi na kukataa kura zao!!! Sidhani kama leo wanaweza kubadilika na kuwakemea CCM na Serikali yake.
January 11, 2011 12:37 AM
blank.gif

Anonymous said... Basi tugawane nchi tupige kura sehemu ipi ya Tanzania iwe serikali ya kiislamu na sehemu gani serikali ya kikristo. Maana mnakazania udini udini kana kwama ni Mgawo wa umeme. ACHENi UPUZI Ninyi nyote mnaoingiza udini kwenye mijadala ni Wapumbavu kabisa.
January 11, 2011 12:46 AM
blank.gif

Anonymous said... Mtaji wa CCM ni Ujinga na umasisikini, jinsi ujinga unavyopungua na ndio mwisho wao unavyofika, sisi wenye akili hatuwezi kumisikiliza huyo mtulia mpuuzi atakuwa amepewa hela kidogo ili aongee agange njaa
January 11, 2011 1:07 AM
blank.gif

Anonymous said... Jamani sasa watanzania na ukiristo umevuka mpaka.matusi mpaka kwa raisi sasa yanavuka mpaka.ni bora mkawatukana maaskofu wanaoingilia mambo ya siasa badala ya kumtukana raisi.nyie wakiristu mnasema mmesoma kuliko nani?wacheni kujigamba wakati ujui ni chuo gani ambacho wewe umesoma na waislamu atujasoma.huo ni ulimbukeni wa karne tuu.wacheni kujigamba wakati magamba ujaona.
January 11, 2011 1:17 AM
blank.gif

Anonymous said... hakuna mwenye hati miliki ya siasa nchini. wnasiasa wanafiki hawapendi kukosolewa hata siku moja. mbona hao maaskofu wakiwasifia hamuiti kuingilia siasa na dini ; wakiwakosoa mnasema dini kuingilia siasa. what is your principle then? mbona mko selective? makamba akitumia biblia kutetea oppression hamusemi anachanganya dini na siasa. what is your principle then? what is dini what is siasa? zote ni platform za kumhudumia mwananchi; zote zina uhuru wa kutoa maoni kukosoa na kushauri; hakuna mwenye hati miliki zaidi ya mwingine. zote ni social tools kwa ajili ya mwanadamu. dhana ya kutochanganya Siasa na Dini inatumiwa kama silaha ya oppressive leaders kuendeleza kuwakandamiza wengine. Viongozi wadini msikubali kufungwa midomo wala kuwa maspika wa oppressive leaders. kwanza, askofu, mwalimu, polisi, mbunge, mwanachama cha siasa au NGO wote wana haki ya kikatiba kutetea maslahi ya mwananchi - hakuna wa kumtukana mwningine. kiongozi akiwa mfano wa kufuata sheria na utaratibu, hatalaumiwa na yeyote. kama sheria hazifai tuzibadilishe kwa demokrasia ya wazi. asijifanye mtu mmoja alizaliwa na label au hati miliki juu ya wengine!! Maskofu na mashehe endeleeni kukosoa wote wanaoleta ukorofi wa kisiasa na kijamii. yote hayo ni mauovu. mwanasiasa anayeona kukoselewa hakufai ajisafishe tu awe safi morally and ethically; no manipulation hapa. tukatae kucheza huo mpira wa kinafiki sasa. kiongozi mbovu akosolewe bila woga. na anayejiona mzuri asimame ajitetee mwenyewe. mtu asiwe laudspeaker ya mtuhumiwa. ukiwa na tuhuma zinakujia jibu, tena kama unajiona msafi jibu tu lakini weka wazi usafi wako, usitukane wanaokukosoa, wala kutumia mtu mwingine kukujibia.
January 11, 2011 1:39 AM
blank.gif

Anonymous said... WAKRISTO KUWENI MACHO YALITOKEA EGYPTI YATAWAKUTA. SIMLISIKIA WIKI MBILI ZILIZOPITA WAKRISTO ZAIDI YA ISHIRINI WALIUWAWA KANISANI. MAMBO HAYA MABOMU KIUNONI YANAKUJA. SASA WAMESHTUA IRINGA. HILO NI LA MGAMBO LIMESHALIA.
January 11, 2011 2:08 AM
blank.gif

Anonymous said... Namjibu ndugu wa pili juu. Kiongozi wa dini akikosoa taratibu za uchaguzi na maangamzi yalitokea; au ukitoa maoni yake kuhusu mwelekeo unaofaa - hajajiingiza katika siasa. Lakini akisema "hamtambui Meya" basi amejiingiza katika siasa kwa sababu he has taken a political stand. Amechukua msimamo wa kisiasa na hiyo ni kijiingiza katika siasa. Hapo atakuwa open kuhujumiwa kwamba alitumia criteria gani kutomtambua Meya. Ni wazi atakuwa amejitosa katika mgogoro wa siasa kinyume na maadili ya uongozi wa kidini.Narudia: wanahaki ya kusema kwamba chaguzi zifanyike kwa haki na uadilifu. Lakini hawana haki ya kusema fulani kashinda/kashindwa au fulani nina mtambua/simtambui. Their calling (as religious leaders) requires them to steer clear of partisan positions. Wako, Mwendapole
January 11, 2011 3:46 AM
blank.gif

Anonymous said... By the way, Maaskofu pia ni raia wa Tanzania, wanaposhiriki siasa ni kama raia wngine, tena wao wanaona mbele zaidi kuliko akina Makamba.

Makamba anaona leo tu, hajui ya kesho na mtondo. Ndio maana anapofumbua kinywa chake haoni aibu wala hatari ya maneno yake. Hajui hayo maneno yatawaandama watoto wake na wajukuu zake hadi kaburini. Kama ambavyo leo mtu akijitambulisha kuwa yeye ni mjukuu wa Hitler wa ujerumani, wengi watastuka wakisikia ni mjukuu wa Makamba.
Tusiwe wanafiki, CCM ina udini, na wanautumia kuwatishia wengine ili waogope kuitwa wadini. Hakuna mtanzania asiye na dini. Kama si muislam au mkristo atakuwa na imani ya kimila. Ila watu wanapokwepa kusema ukweli ili wasionekane wadini, wanakuwa waongo.

Hawa wanaojiita wazee wa DSM hawajui kuwa CCM wamecheza rafu? Acheni unafiki. Hawa ni wazee wa CCM sio wa DSM.

Viongozi wa serikali wanatakiwa wawatumikie wananchi wote, sio wanaCCM. Haki itendeke kwa watu wote. Hata CCM wangekuwa wanaonewa wangeandamana tu.
January 11, 2011 4:48 AM
 
Wahenga walinena asiyesikia la Mkuuhuvunjika guu................................
 
Chatanda azua tena mvutano CCM, Chadema Arusha

Imeandikwa na John Mhala, Arusha; Tarehe: 10th January 2011 @ 23:47 Imesomwa na watu: 1012; Jumla ya maoni: 0








WABUNGE na madiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), jana walisusa kushiriki uchaguzi wa Jumuiya za Serikali za Mitaa Tanzania (ALAT) katika Mkoa wa Arusha.

Walifikia hatua hiyo wakipinga uwepo wa Mbunge wa Viti maalumu kupitia Jumuiya ya Wanawake (UWT) wa Mkoa wa Tanga, Mery Chatanda katika mkutano huo.

Mbunge wa Jimbo la Karatu, Mchungaji Israel Natse ambaye alitaka ufafanuzi wa Chatanda kuwepo katika kikao hicho, kwa kuwa kanuni za Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) wabunge wanaopaswa kuhudhuria kikao hicho, ni wa Mkoa wa Arusha tu na sio vinginevyo.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa muda wa mkutano huo, Ismail Katamboi ambaye ni Diwani wa kata ya Kisongo, katika Halmashauri ya Arusha, alisema Chatanda ni mjumbe halali wa kikao hicho na kutaka shughuli za kikao hicho kuendelea.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Karatu, Lazaro Massay alisimama na kumtaka Katamboi kueleza kama Chatanda ni Mbunge wa Arusha ama Tanga.

Lakini Katamboi hakutaka kujibu swali hilo kama alivyotaka Massay bali alisisitiza kuwa Chatanga ni mjumbe halali wa mkutano huo wa Alat na hakutoa ufafanuzi zaidi.

Baada ya jibu hilo, Diwani Julius ole Sekayane (CCM) ambaye alimwakilisha Meya wa Jiji la Arusha, alisimama na kuwataka wajumbe kuendelea mkutano kwa kuwa Chatanda ni mjumbe halali katika mkutano huo na anayedai kuwa sio halali amekosea.

Baada ya malumbano hayo, wabunge wa Chadema, Natse wa Karatu na Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema na madiwani wote wa Chadema waliondoka ndani ya ukumbi wakisema hawako tayari kushiriki uchaguzi huo.

Natse akizungumza nje ya ukumbi, alisema Chatanda sio mjumbe halali na pili wao wanaungana na wenzao kusema kuwa hawamtambui Meya wa Jiji la Arusha Gaudence Lyimo kwani hakuchaguliwa kufuata kanuni za Tamisemi.

Mkutano huo wa Alat Mkoa wa Arusha hushirikisha wabunge wote wa mkoa, wenyeviti wa halmashauri za wilaya, wakurugenzi wa halmashauri zote na madiwani wawili waliochaguliwa na baraza la madiwani la wilaya husika.

Mkutano huo ulikuwa wa kumchagua Mwenyekiti wa Alat mkoa wa Arusha, mweka hazina, kamati ya utendaji na mbunge mwakilishi wa mkoa katika mkutano mkuu wa Alat Taifa.
 
WABUNGE na madiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), jana walisusa kushiriki uchaguzi wa Jumuiya za Serikali za Mitaa Tanzania (ALAT) katika Mkoa wa Arusha.

Walifikia hatua hiyo wakipinga uwepo wa Mbunge wa Viti maalumu kupitia Jumuiya ya Wanawake (UWT) wa Mkoa wa Tanga, Mery Chatanda katika mkutano huo.

Mbunge wa Jimbo la Karatu, Mchungaji Israel Natse ambaye alitaka ufafanuzi wa Chatanda kuwepo katika kikao hicho, kwa kuwa kanuni za Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) wabunge wanaopaswa kuhudhuria kikao hicho, ni wa Mkoa wa Arusha tu na sio vinginevyo.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa muda wa mkutano huo, Ismail Katamboi ambaye ni Diwani wa kata ya Kisongo, katika Halmashauri ya Arusha, alisema Chatanda ni mjumbe halali wa kikao hicho na kutaka shughuli za kikao hicho kuendelea.

Hivi nchi hii kweli wapo viongozi? Mbona kila mtu anafanya atakavyo tu? Hivi NEC wapo wapi hapa?
 
TANGAZO:
You Are Now Entering No man's Land, going by the name Tanzania!
..
Nguvu ya huyu mama nadhani inamshinda hadi aliyemweka kwenye nafasi hiyo!
Could she be a freemason too?..
Naombeni picha yake itundikwe hapa!
 
Safari, Ruhuza waeleza dawa ya mgogoro Chadema, CCM Arusha Monday, 10 January 2011 21:05

Fidelis Butahe na Geofrey Nyang'oro

ILI kuepusha shari jijini Arusha , mwanazuoni aliyebobea katika sheria, Profesa Abdallah Safari amesema ili CCM na Chadema wakae chungu kimoja kesi waliyofunguliwa viongozi wa Chadema ifutwe.

Tayari Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa ameshasema kuwa hawawezi kukaa na CCM kwa kuwa chama hicho na serikali yake ni katili na ya kihuni huku Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba naye akisema hawawezi kukaa na Chadema.

Lakini jana, Profesa Safari alisema kuna umuhimu wa kufutwa kwa kesi hiyo kwa kuwa hata Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha alishavitaka vyama hivyo vikae pamoja kuzungumzia mfarakano ulioleta maafa mjini Arusha.

Viongozi wa Chadema waliofunguliwa kesi ya kufanya mkusanyiko kinyume na sheria Januari 6 mwaka huu ni Mwenyekiti, Freeman Mbowe, Katibu wake, Dk Slaa pamoja na wabunge watatu wa chama hicho.

"Waziri alishazungumza suala hili, lakini binafsi naona kama halitawezekana kwa kuwa tayari viongozi wa Chadema wameshafunguliwa mashitaka, sidhani kama wanaweza kukubali kukaa meza moja na CCM wakati wana kesi mahakamani, sidhani,"alisema Profesa Safari.

Alisema kuwa itakuwa rahisi kwa viongozi wa vyama hivyo viwili kuzungumza kama kesi hiyo itafutwa na kuongeza kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani anatakiwa kumshauri rais Jakaya Kikwete kuhusu hali hiyo.

"Waziri Nahodha anaweza kumshauri rais Kikwete ambaye naye anaweza kumtaka Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kufuta kesi kwa kuwa DPP hawezi kufuta kesi bila kutakiwa kufanya hivyo na rais,"alisema Profesa Safari.

Katibu wa Chama Cha NCCR Mageuzi Samuel Ruhuza alisema siyo kitu kizuri kwa vyama hivyo kuonyesha ubabe katika msuala yanayohusu maslahi ya umma. "Hilo wanalojadili linahusu maslahi ya nchi,wanapoonyesha ubabe ni kwa manufaa ya nani? "alihoji Ruhuza na kuwataka CCM na Chadema kukaa meza moja kulipatia ufumbuzi suala hilo.

Alisema katika sakata la Arusha pande zote zinazohusika zimefanya makosa kwa kuwa CCM ilimpeleka mjumbe kupiga kura asiyehusika wa eneo hilo,Chadema imekaidi amri ya jeshi la polisi, polisi nao wameua badala ya kukamata wahalifu.

Ruhuza alizitaka pande zote zinazohusika kukutana na meza moja kujadili mstakabali wa sakata hilo ambalo limezifikisha siasa za Tanzania pabaya kwa kusababisha vifo vya watu watatu na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa.
 
TANGAZO:
You Are Now Entering No man's Land, going by the name Tanzania!
..
Nguvu ya huyu mama nadhani inamshinda hadi aliyemweka kwenye nafasi hiyo!
Could she be a freemason too?..
Naombeni picha yake itundikwe hapa!

Worthy observations.........................
 
Chadema protest rival party official's presence
Monday, 10 January 2011 22:38

By Moses Mashalla
The Citizen Correspondent

Arusha. The standoff between Chadema and Arusha City authorities took a new turn yesterday when the opposition party representatives marched out of a meeting organised by the Association of Local Authorities in Tanzania (ALAT).

The councillors were apparently objecting the presence of Ms Mary Chatanda, the Arusha regional CCM secretary and the party's Special Seats MP for Tanga Region, in the meeting.

The walkout took place at the Arusha district commissioner's office at around 11 am when six Chadema representatives stormed out even before serious business started.

The meeting was expected to elect ALAT's chairman and secretary for the region as well as select the member of Parliament to represent the region in ALAT meetings at the national level.

A regional treasurer for the association as well as six members of the executive committee were also to be elected during the meeting, the first since the October 31 General Election.

Those who marched out included Arusha Urban MP Godbless Lema and his Karatu counterpart Israel Natse, both legislators on a Chadema ticket.

In the meantime, the Muslim Council of Tanzania (Bakwata) in Arusha Region has issued a statement recognising the new Arusha mayor, Mr Gaudence Lyimo (CCM), whose election is being contested by Chadema.

Making the announcement, however, the Bakwata regional secretary, Sheikh Abdulkarim Jonjo, said it was not upon religious leaders to recognise political leaders.

Meanwhile, the Tanganyika Law Society (TLS) yesterday called on the government to probe the killings by police of three civilians in Arusha last Wednesday, when the law enforcers tried to stop a peaceful demonstration by Chadema supporters.

The society said in a statement it issued yesterday that the police's action was denied citizens rights of association, assembly and expression that is guaranteed by the Constitution.

"The TLS calls on the government to investigate this unfortunate incident, to bring those accountable to task and to continue using peaceful means in upholding the rule of law and securing democracy for national good," read part of TLS statement.
TLS has become the latest prominent organization to join a wave of condemnations of the killings following those of religious leaders, human rights organizations and politicians.
Police opened fire at the defiant demonstrators who were protesting alleged irregularities in the election Arusha City's mayor.
The bar association whose functions include overseeing observance of the rule of law and good governance also condemned the use of excessive force by the Police to disperse an unarmed and peaceful crowd.

Additional reporting by Mussa Juma (Arusha) and Bernard James (Dar)
 
Umeya Arusha wazidi kuitesa CCM


na Ramadhani Siwayombe, Arusha


amka2.gif
UONGOZI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha, umeiomba Ofisi ya Waziri Mkuu kutoa tamko kuhusiana na uchaguzi wa Meya jiji la Arusha, ili kuondoa utata.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari jana Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Onesmo ole Nangole, alisema suluhisho la mgogoro wa uchaguzi wa umeya jiji la Arusha ni Ofisi ya Waziri Mkuu ama Waziri Mkuu mwenyewe kutoa tamko juu ya uchaguzi huo.
Alisema kila uchaguzi una taratibu zake na usimamizi wake na katika uchaguzi wa halmashauri zote uko katika kanuni zinazoandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), hivyo wao ndio wanaopaswa kutoa tamko juu ya hilo.
Alifafanua kimsingi hakuna ugomvi wowote baina ya vyama vya CCM na CHADEMA hadi kuwe na wazo la kusema vikutane kusuluhisha suala hilo ambalo ni la kikanuni na kisheria.
"Uchaguzi wa kumpata meya ulifanyika na kusimamiwa na mkurugenzi na matokeo kutangazwa na msimamizi ambaye alikuwa mkurugenzi; kutokana na hali iliyojitokeza naomba Waziri Mkuu atoe tamko ili kumaliza tatizo,'' alisema Nangole.
Naye Katibu Mkuu wa CCM Mkoa wa Arusha, Mary Chatanda, ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu, alisema anashangazwa na utata unaojitokeza kuhusiana na yeye kuwa mbunge Arusha wakati alipigiwa kura mkoani Tanga.
Alisema kila chama cha siasa kina utaratibu wake katika kupata wabunge wake wa viti maalumu na kuwapangia mahala pa kufanyia kazi, hivyo chama chake kimempangia kufanya kazi mkoa wa Arusha na ndivyo kilivyowasilisha ofisi ya Bunge.
Akitolea mfano CHADEMA alisema wao kama chama walikuwa na utaratibu wao kupata wabunge wa viti maalumu na kuwapangia mahala pa kufanyia kazi na ndio maana wabunge kama Lucy Owenya na Grace Kiwelu wa Moshi wamepangiwa wilaya ya Hai ambako ndiko walikopigia kura katika baraza la madiwani.
Aidha, akizungumzia tamko la Makamu Mwenyekiti wa chama hicho na Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela, kumtaka awaombe radhi maaskofu kwa tamko lake kuwataka wavue majoho ya uaskofu na waingie katika siasa, Chatanda alisema hayo ni mawazo ya Malecela.
"Nasema hivi hayo ni mawazo yake na mimi namheshimu mzee wetu huyo, hata hivyo siwezi kuomba radhi kutokana na mawazo binafsi ya mtu. Mimi naamini nilichokisema ni sahihi,'' alisema Chatanda.
Baada ya maaskofu mkoa wa Arusha kutoa tamko la kutomtambua meya wa Arusha na kuwa hawatatoa ushirikiano kwake, Chatanda naye alitoa tamko kuwataka maaskofu hao kuvua majoho yao na kujiingiza katika siasa.
 
Jamani tunaona utani lakini nawambia ukweli Tanzania yetu inaelekea kubaya. Ni watu wachache kama hawa akina Makamba na Chitanda.... ambao shida yao ni kutimiza malengo yao ya mda mfupi wanaoharibu amani. Na tusipokuwa makini..hatuna pa kukimbilia. Hivi unajua mpaka leo sioni kwa nini JK na serikali yake wanashindwa kulimaliza hili swala? Pinda anashindwa nini kuelekeza (kama waziri mkuu mwenye dhamana ya TAMISEMI) uchaguzi urudiwe kwa kufuata sheria na haki.? kama CCM wakishinda..well and good..kama CHADEMA wakishinda well and good. To be honest..sikutegemea kama Kikwete atakuwa this kind of a president. Lakini tutavuna tulichopanda. So sad sasa hili swala linaangaliwa kwa udini...jamani tunakwenda wapi?

Hivi hawa maaskofu wangekuwa wadini....wangemfanyia kampeni Kikwete? Jamani Kikwete should be the last person to entertain this kind of thinking.

Lakini, hakika..JK na serikali yake..wamecheza na kitu wasichojua consequences zake. Udini ni kitu kibaya sana. Idea ya udini ndo hiyo imeshaingia TZ. Trust me you. Msishangae kesho watu wakaanza kubaguliwa kwa misingi ya udini iwe mashuleni au maofisini.... JK you will bear this cross and nobody else.
 
Huyu mwanamke anatimiza/anafanya kazi aliyotumwa na waliomweka. Ila ajiulize Batlda yuko wapi kwa sasa.
 
Tendwa: Vurugu na mauaji ya Arusha Chadema hawawezi kukwepa lawama

Na Joyce Mmasi
"KILA chama cha siasa kitakuwa na haki ya kufanya mikutano ya kisiasa na maandamano kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa, hii ni sehemu tu ya haki za vyama vya siasa iliyoelezwa katika sheria namba tano ya mwaka 1992 ya vyama vya siasa.
Sheria hii pia katika sehemu ya tatu kifungu 1 (e) imeeleza wajibu wa vyama vya siasa na kueleza moja ya wajibu huo ni kufanya mkutano wa kisiasa na maandamano bila kufanya vurugu kwa mujibu wa sheria.

Sehemu ya nne katika sheria hii ya vyama vya siasa pia inaeleza wajibu wa msajili wa vyama vya siasa ambapo katika kifungu 1 (c) kinaeleza wajibu wa msajili wa vyama vya siasa, ni kuzuia kitendo cha uvunjifu wa kanuni za maadili kisiendelee na kukitaka chama au kiongozi wa chama kujirekebisha.

Inakuwaje vyama vya siasa vinazuiwa kutimiza wajibu na haki zao kwa mujibu wa sheria hiyo. Imekuwa ni kawaida kwa jeshi la polisi kuzuia kufanyika kwa maandamano na mikutano ya hadhara vinavyoandaliwa na vyama vya siasa, je, hatua hii ya polisi ni halali?
Msajili wa vyama vya siasa nchini, John Tendwa anasema serikali inapaswa kusikilizwa na kwamba endapo kutakuwa na zuio au ushauri katika utekelezaji wa haki au wajibu, chama kinachohusika kinapaswa kusikiliza na kutii.

Kauli ya Tendwa inafuatiwa na vurugu zilizosababishwa na maandamano ya wafuasi wa Chadema ambao walikuwa wakitekeleza vipengele hivyo vya sheria ya vyama vya siasa licha ya kuzuiwa na serikali kupitia jeshi la polisi.
Tendwa anasema endapo Chadema wangesikiliza amri ya jeshi la polisi na kuitii, kusingekuwa na vurugu wala matukio ya umwagaji wa damu yaliyofanyika mkoani Arusha.

Anasema jeshi la polisi kwa kutilia mashaka maandamano yao, walizuia maandamano hayo licha ya kuyaruhusu awali na kuruhusu mkutano pekee ambao walifanya hivyo kutokana na kujiandaa kulinda amani katika mkutano huo na maandamano.

Anasema kwa mujibu wa maelezo ya polisi, kulikuwa na kila dalili ya maandalizi ya vurugu yaliyoandaliwa na wafuasi wa chama hicho na hivyo kuruhusiwa kwa maandamano hayo kungepelekea vurugu, uvunjifu wa amani nap engine vifo vingi zaidi.

Nini chanzo cha vurugu hizo
Chanzo cha vurugu za Arusha ni kupinga uchaguzi wa Meya wa jiji hilo ambapo madiwani wa CCM pamoja na mmoja kutoka TLP walishiriki uchaguzi na kumchagua kiongozi wa jiji hilo, baada ya wale wa Chadema kugoma kutokana na kutokukubaliana na ushiriki wa mjumbe mmoja wa CCM aliyejulikana kama Mary Chatanda ambaye ni mbunge wa viti maalum kupitia mkoa wa Tanga.

Msajili anasemaje juu ya utata wa mbunge huyu wa viti maalum na malalamiko ya Chadema? "Nadhani Chadema hawako wazi katika hili, kwani uhalali wa Mary Chatanda lilishatolewa ufafanuzi na katibu wa Bunge. Sheria iko wazi na ilifafanuliwa na katibu wa bunge baada ya madiwani wa pande zote mbili kuonyesha utata walipokuwa katika kikao cha kwanza cha uchaguzi wa Meya, ambapo vyama vyote viwili vilikuwa vikilalamikia ushiriki wa mjumbe mmoja mmoja kutoka kila chama".

Anasema ufafanuzi walioupata juu ya uhalali wa wabunge hao wa viti maalum waliokuwa wakilalamikiwa na vyama vyote viwili ni kwamba, sheria inawatambua wabunge kama madiwani wa sehemu wanazotoka na inaendelea kufafanua chama kinachowakilishwa na mbunge wa viti maalum, kitakuwa na haki ya kumpangia kazi sehemu yoyote isipokuwa hataruhusiwa kufanya kazi katika eneo lingine.

Anasema baada ya ufafanuzi huo utata wa suala la uwakilishi wa mbunge huyo wa viti maalum ukawa umemalizika na kwamba haelewi sababu za Chadema kususa kuendelea na uchaguzi wa Meya na kushangazwa na chama hicho kukwepa kueleza wafuasi wake suala hilo huku ikiendelea kushikilia msimamo wa kutomtambua mbunge huyo wa viti maalum wa CCM.

Uhalali wa uchaguzi wa Meya
Msajili anasema, baada ya kususia uchaguzi uliofanywa bila Chadema kushiriki vyama hivyo viwili vinavyohusika katika suala hilo vilipaswa kuzungumza ili kupatikana kwa suluhu na kwamba yeye alikubali kuwa msuluhishi, lakini anasema hajui sababu ya chadema kuamua kuitisha maandamano kabla ya kumalizika kwa mazungumzo ambayo anasema anaamini yangeweza kuleta suluhu na kujenga amani miongoni mwao.

Anasema jambo moja ambalo haliko wazi na ambalo angependa Chadema wakaliweka bayana ni kueleza wazi agenda yao, na nini wanachokitaka au wanachokusudia badala ya kufanya mambo ambayo kwa namna moja ama nyingine yanaweza kuhatarisha amani na kupunguza imani ya wananchi dhidi ya chama hicho.

"Haijulikani hasa wanataka nini, maana kama ni kweli ilikuwa uhalali wa Mary Chatanda walishasomewa sheria na wakaelewa. Awali walizungumzia suala la kutaka katiba, kila mtu aliunga mimi nimeunga mkono nimetoa maoni yangu, Waziri mkuu naye kasema, na mwisho rais ameridhia, sasa waeleze wanataka nini ili madai yao yawe wazi na yaeleweke," anasema.

Msajili anasema inavyoonekana, ndani ya chama hicho, wapo baadhi ya viongozi wanataka kudanganya wananchi na kuficha kuwaeleza ukweli na akasema ni vyema kwa vyama vya siasa kufuata taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa sheria.

Ushauri wa Tendwa kwa Polisi, CCM na Chadema
Tendwa anasema pamoja na huzuni iliyotawala kufuatia vurugu zilivyosababisha mauaji, ni vyema kwa jeshi la polisi kuangalia uwezekano wa kuepuka vurugu na badala yake kutumia nguvu zinazoweza kuhatarisha maisha ya watu.

Wananchi nao wasikubali kutumika na vyama vya siasa au baadhi ya watu, waepuke vurugu na watii maagizo wanayopewa, kama polisi ambaye ni mlinzi wa amani amezuia maandamano, wananchi wanapaswa kutii amri halali ya polisi, na vyama vya siasa kupitia viongozi wao vifuate taratibu ili kuimarisha amani na kuepuka vurugu zinazoweza kuleta maafa.

Anasema vyama vya siasa hususani Chadema kinapaswa kuepuka kutoa shutuma za mara kwa mara dhidi ya chama tawala huku akitolea mfano katika mikutano yake mingi na vyama vya siasa, vimekuwa vikitumia muda mwingi kushutumu chama tawala badala ya kutoa hoja ya kujenga nchi.

Kwa upande wa CCM, msajili anasema kama chama kiongozi kinapaswa kuwa makini na kushirikiana na vyama vingine katika kutatua migogoro ili kuepuka matukio yanayoweza kuhatarisha amani ya nchi.


Source : Mwananchi
 
Back
Top Bottom