Barua ya wazi kwa RC Makonda: Nenda Ikulu, majina ya Wauza Madawa yapo mezani kwa Rais Magufuli

The Tomorrow People

JF-Expert Member
Jul 11, 2013
2,674
2,801
COMMON BROTHER PAUL MAKONDA PUT JOKE ASIDE IN DRUG WAR!

•Weka kamba kwa 'singo' usibembee

•Usitutoe kwenye mjadala wa mkoa wa Dar wenye facilities zote za elimu kuvurunda

Na Bollen Ngetti

NIMECHEKA sana, tena kwa sauti namna RC Makonda (Dar) alivyotangaza 'fatwa' (kiama) kwa wauza sembe, unga Dar akisisitiza, "niko tayari kufa" hahahahaa. Makonda yuko tayari kufa kwa kuwataja kina Wema Sepetu, TID, Chid Ben, Mr. Blue na maafande 9 wa vituo vya polisi. Nipeni mbavu spea.

Hatua hii ya Jasiri Paul Makonda kutangaza kiama kwa wauza 'drugs' imenikumbusha kisa cha mkulima mmoja nchini Kenya kaskazini mwa Nairobi aliyejulikana kwa jina la Muchuka.

Muchuka alichoka maisha ya kulea watoto 8 pamoja na mke (9), baba yake (10) na yeye (11) hivyo akafanya uamuzi mgumu wa kwenda porini kujinyonga. Akachukua kamba.

Muchuka akapanda juu ya mti na kufunga kamba ili ajinyonge. Alipovaa kamba shingoni na kujaribu kujiachia akakuta Shingo inauma. Akashusha kamba kifuani (kwapani) nako akakuta inauma. Muchuka akashusha kamba usawa wa tumboni nako akahisi tumbo kukatwa ndipo akashusha kamba hadi usawa wa kiuno kwa chini kidogo kwenye makalio akajiachia. Lakini alipojiachia kwa nguvu badala ya kujinyonga Muchuka akajikuta anabembea raha mustarehe.

Mpita njia (jirani yake) akamkuta na kumuuliza kwa Kiswahili cha Kikenya, "Muchuka, we fanya nini hapa?" Muchuka: "mi najinyonga, maisa magumu sana, I can't afford." Ndipo mpita njia akamwambia, "Muchuka, weka muchezo chini, weka kamba kwa singo na ufe mara moja."

Huyu ndiye Mkuu wetu wa Mkoa, Paul Makonda. Anabembea kupambana na "drug dealers". Anachekesha. Hivi unampa Chid Ben na TID wito wa kuja polisi eti unapambana na "drug dealers?" Are you serious my brother from another mother? Paul?! Huu ni utani wa February.

Hii orodha ya wauza sembe alikuwa nayo Mzee Mkapa. Alipoogopa kutaja akampa Mzee Yusuf Makamba aliyetangaza kuyataja majina hadharani. Wala usijitetee eti nataja wa mkoa wangu tu. Mizungu ya unga yote iko Dar ndio kuna kila kitu! Makamba alipoyaona yale majina akaugua kifuaduro. Akaahirisha Press Conference. Jakaya akasema, "wauza unga nawajua kwa majina na hata viongozi wa dini wamo!" Akiwa karibu kustaafu akasema, "vita ya dawa za kulevya ni ngumu maana mtandao wake ni mpana na imara ndani na nje ya nchi!"

Kama kweli Makonda ameamua kupambana na "maruhani" wa unga Dar, aache kubembea, aache mzaha na kina Mr. Blue. Aende Ikulu, majina yao yako mezani kwa JPM Jakaya aliziacha. Ayachambue ya Dar ndipo atangaze hadharani. Hatokuta Chidibenzi. Atawakuta "wenyewe" na umma utapata kilicho bora. Atakutana na wengine aliowazindulia makampuni yao. Atakutana na kada mbalimbali: polisi, wanajeshi, wafanyabiashara, wachungaji, waombolezaji, maaskafu nk. Hapa Makonda atakuwa "tayari kufa." Lkn si hii bembea.
[HASHTAG]#UzalendoKwanza[/HASHTAG].
#MvurundoKidato_4 vepeee!

Majina ya wauza Madawa ya Kulevya: Kikwete anayo!

=====

ORODHA ya askari polisi 17, wasanii na watu mbalimbali 18 waliotajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wiki hii katika sakata la dawa za kulevya, itasaidia kuwanasa watumiaji, wasambazaji na wauzaji wakubwa wa dawa za kulevya nchini?

Hili ni swali ambalo sasa linaonekana kuumiza vichwa vya watu wengi, hasa ikizingatiwa kwamba suala hilo bado lipo chini ya uchunguzi wa vyombo vya ulinzi na usalama.

Miongoni mwa askari hao, 12 tayari wamesimamishwa kazi na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Ernest Mangu ili kupisha uchunguzi wa jambo hilo.

Ni uchunguzi huo ndio utakaobaini sababu za wao kutajwa katika sakata hilo la dawa za kulevya kama ambavyo alibainisha Makonda wiki hii.

Kusimamishwa kazi kwa askari hao na kuwekwa chini ya ulinzi katika Kituo Kikuu cha Polisi, wasanii na watu kadhaa kwa mahojiano, wapo ambao wanadhani kwa vyovyote kutaliwezesha Jeshi la Polisi kupata taarifa zaidi.

Wasanii waliotajwa na ambao walikuwa wameripoti polisi tangu juzi kwa mahojiano, ni pamoja na Wema Sepetu, Hamidu Chambuso ‘Dogo Hamidu’, Khalid Mohamed ‘TID’ na Babuu wa Kitaa.

Kabla ya hapo, mwanzoni mwa wiki hii wakati akitangaza orodha hiyo kwa mara ya kwanza, Makonda alisema alikuwa amewaweka ndani Ahmed Hashim Ngahemela (Petit Man), Said Masoud Lina (Alteza), Nassor Mohamed Nassor , Bakari Mohamed Khelef na Omar.

Katika orodha hiyo ya wasanii na watu mbalimbali, akiwamo Vanessa Mdee, mrembo anayependezesha video za muziki, Tunda na wengine wanne ambao watapaswa kufika kituoni kesho kutokana na wito wa Makonda nao huenda wakazalisha taarifa nyingine mpya.

Si hilo tu uchunguzi dhidi ya askari, watu na wasanii waliotajwa katika orodha hiyo, pia unaweza kuthibitisha au kutothibitisha tuhuma zinazowakabili.

Iwapo watapatikana baadhi ya wanaotumia, au wanaouza dawa hizo, ni dhahiri kuwa upo uwezekano wa kuwataja wanaowauzia au kufanya nao biashara hiyo na hatimaye katika mlolongo huo yatafikiwa majina ya vigogo wakubwa wa biashara hiyo.

Endapo hilo litafanikiwa, litafuta madai dhidi ya Makonda kuwa ameamua kuwaacha mapapa na kukamata vidagaa wa dawa hizo.

Juzi, Makonda kwa maneno yake alisema: “Kuwahoji hawa itatusaidia mambo mawili, kuna mwingine anasema ameacha, lakini anasema hakumbuki alipochukua, basi kama unatumia unajua yanapouzwa, kama hujui unapata wapi maana yake wewe unatengeneza dawa, ukitengeneza dawa ukaitumia mwenyewe haina shida ukiisambaza tunakutafuta.”

Ismail Juma, mkazi wa Magomeni, alisema endapo harakati hizo za Makonda zitafanikisha kujulikana na kuwataja kwa majina vigogo wa unga, wakiwamo wale ambao wamekuwa wakinyooshewa vidole na wananchi, atajijengea si tu heshima bali uaminifu mkubwa na kuandika historia mpya kwa taifa hili baada ya wengi kugwaya kufichua wanamtandao huo.

Kumbukumbu zinaonesha kuwa mwaka 2006 kupitia Waziri wa Usalama wa Raia, Bakari Mwapachu, Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete aliwahi kupatiwa orodha ya majina 58 wakiwamo polisi 20 na baadhi ya makamanda wa polisi wa mikoa, waliotajwa na wananchi kuwa wanajihusisha na mtandao wa dawa za kulevya.

Kikwete hadi anaondoka madarakani Novemba 5, mwaka juzi, hakuwahi kutaja kwa majina watu wanaojishughulisha na biashara hiyo licha ya mara kadhaa kudai kuwa alikuwa na orodha ndefu ya watu hao.

Ikulu yake iliwahi kusema kuwa orodha hiyo alikuwa ameikabidhi kwa Mkuu wa Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya.

Mwaka 2013, akiwa na wadhifa wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Uratibu), William Lukuvi, akiwa bungeni alisema iwapo akitaja majina ya wauza unga basi hata humo bungeni hawatapona.

Alipostaafu aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa, aliwahi kukiri kutikiswa na baadhi ya vigogo wa dawa hizo.

Nzowa aliwahi kuliambia MTANZANIA Jumapili kuwa mmoja wa waliomtikisa ni bilionea Mtanzania anayedaiwa kuwa kinara wa mtandao wa dawa za kulevya, Ali Khatib Haji Hassan maarufu kama Shikuba (47) ambaye baadaye alikamatwa baada ya Marekani kutangaza kutaifisha mali zake.

Katika hilo, Nzowa alikwenda mbali zaidi na kudai kuwa wauza unga hao waliwahi kutishia kumuua baada ya kugoma kupokea rushwa ya Sh bilioni 3 ili kuwaacha wapange mikakati na watuhumiwa wakuu wa dawa hizo aliokuwa amewakamata.

Nzowa alidai kuwa tukio hilo lilipangwa kufanyika akiwa nchini Kenya alikokwenda kuhudhuria mkutano ulioandaliwa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa jijini Nairobi.

Mwaka jana, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga kabla Rais Dk. John Magufuli hajamtoa kwenye nafasi yake, alipata kigugumizi kuweka hadharani orodha ya majina ya wafanyabiashara wa dawa za kulevya, licha ya kuliagiza Jeshi la Polisi limpatie kwa kusema kuwa jambo hilo halitasaidia kukomesha biashara hiyo.

Kutokana na hayo, mtihani mkubwa unaoelezwa kwa Makonda dhidi ya vita aliyoianzisha ni namna ya kuwafikia mapapa hao.

Chanzo: Mtanzania
 
Tatizo ni kuwa wauza dawa na mafisadi ya nchi hii yameweka serikali na mahakama mfukoni......

Hii vita inawezekana kama kutakuwa na utashi wa kisera na kisiasa........

Hatua ya kwanza ilikuwa ni kutaifisha mali za wahusika wakuu wa biashara hili hiyo pesa iende kusaidia waathirika wa bithaa zao........

Vita ya pili kuikataa na kuondoa pesa yote inayotokana na madawa ya kulevya kwenye mzunguko kuanzia Sasa yaani kufatilia jinsi wanavyofanya utakatishaji...........

Hii vita ni kubwa na nigependekeza sheria Kali ya kupiga Risasi kwa mtuumiwa yeyote atakayekamatwa kwenye hili...........

Watu wawe tunafanya kazi halali na kusomesha watoto kwenye shule nzuri kwa garama kubwa mwisho wa siku waje kuwa kama Chid Benz?.......
 
Mkuu ebu acha tabia cha kichawi.......Makonda ana mamlaka gani ya kwenda ikulu na kuomba listi ya wauza madawa ya kulevya???????....Hicho unachokitaka demand mkuu wa nchi awataje.....Makonda ana timiza wajibu wa level yake amabayo ni mkoa.....Nategemea wana jf wote tunge mpongeza makonda kwenye hili maana haijawai tokea ndani ya nchi hii kiongozi awataje watu kwa majina juu ya madawa ya kulevya......Na hii si vita ya lele mama.....Fatilia juu ya nchi na serikali zinazopambana na madrug dealer ndio utaelewa ujasiri wa huyu bwana mdogo.....Namalizia kusema wewe utakuwa ni mmoja wa wauza madawa ya kulevya......

Halafu suala la kidato cha nne mnamuonea tu huyu kijana wa watu naona kila mtu ana mnyooshea kidole yeye as if yeye kataka mkoa wake upate hayo matokeo.....Ni upuuzi tu......Wazazi mnashindwa kutimiza wajibu wenu nyumbani kwa watoto wenu mnataka serikali iwalele........
Wazazi timizeni wajibu zenu nyumbani afu mwisho wa siku muikabe serikali
 
Hii *fatwa* haina baraka ya mashekhe atulie tu apambane na kupandisha ufaulu wa watoto wa dasilamu, amuulize Waziri wa mambo ya ndani kwanini anaongelea chumbani tena akiwa kavaaa taulo na mswaki wenye dawa ya colget hili swala na sio barazani???Nchi itayumba bro Mako yule nzowa anajua network yote lakini hakuwahi kutaja hata mmoja......
 
Safari ndefu inaanza na hatua moja. Hongera Makonda kwa Kuanza hatua ya kwanza. Wengine wote waliotajwa wakiwa madarakani wakiwemo Marais waliendeleza ngonjera na hawakuthubutu hata kuwataja! Big up Bro. Makonda.
 
COMMON BROTHER PAUL MAKONDA PUT JOKE ASIDE IN DRUG WAR!

•Weka kamba kwa 'singo' usibembee

•Usitutoe kwenye mjadala wa mkoa wa Dar wenye facilities zote za elimu kuvurunda

Na Bollen Ngetti

NIMECHEKA sana, tena kwa sauti namna RC Makonda (Dar) alivyotangaza 'fatwa' (kiama) kwa wauza sembe, unga Dar akisisitiza, "niko tayari kufa" hahahahaa. Makonda yuko tayari kufa kwa kuwataja kina Wema Sepetu, TID, Chid Ben, Mr. Blue na maafande 9 wa vituo vya polisi. Nipeni mbavu spea.

Hatua hii ya Jasiri Paul Makonda kutangaza kiama kwa wauza 'drugs' imenikumbusha kisa cha mkulima mmoja nchini Kenya kaskazini mwa Nairobi aliyejulikana kwa jina la Muchuka.

Muchuka alichoka maisha ya kulea watoto 8 pamoja na mke (9), baba yake (10) na yeye (11) hivyo akafanya uamuzi mgumu wa kwenda porini kujinyonga. Akachukua kamba.

Muchuka akapanda juu ya mti na kufunga kamba ili ajinyonge. Alipovaa kamba shingoni na kujaribu kujiachia akakuta Shingo inauma. Akashusha kamba kifuani (kwapani) nako akakuta inauma. Muchuka akashusha kamba usawa wa tumboni nako akahisi tumbo kukatwa ndipo akashusha kamba hadi usawa wa kiuno kwa chini kidogo kwenye makalio akajiachia. Lakini alipojiachia kwa nguvu badala ya kujinyonga Muchuka akajikuta anabembea raha mustarehe.

Mpita njia (jirani yake) akamkuta na kumuuliza kwa Kiswahili cha Kikenya, "Muchuka, we fanya nini hapa?" Muchuka: "mi najinyonga, maisa magumu sana, I can't afford." Ndipo mpita njia akamwambia, "Muchuka, weka muchezo chini, weka kamba kwa singo na ufe mara moja."

Huyu ndiye Mkuu wetu wa Mkoa, Paul Makonda. Anabembea kupambana na "drug dealers". Anachekesha. Hivi unampa Chid Ben na TID wito wa kuja polisi eti unapambana na "drug dealers?" Are you serious my brother from another mother? Paul?! Huu ni utani wa February.

Hii orodha ya wauza sembe alikuwa nayo Mzee Mkapa. Alipoogopa kutaja akampa Mzee Yusuf Makamba aliyetangaza kuyataja majina hadharani. Wala usijitetee eti nataja wa mkoa wangu tu. Mizungu ya unga yote iko Dar ndio kuna kila kitu! Makamba alipoyaona yale majina akaugua kifuaduro. Akaahirisha Press Conference. Jakaya akasema, "wauza unga nawajua kwa majina na hata viongozi wa dini wamo!" Akiwa karibu kustaafu akasema, "vita ya dawa za kulevya ni ngumu maana mtandao wake ni mpana na imara ndani na nje ya nchi!"

Kama kweli Makonda ameamua kupambana na "maruhani" wa unga Dar, aache kubembea, aache mzaha na kina Mr. Blue. Aende Ikulu, majina yao yako mezani kwa JPM Jakaya aliziacha. Ayachambue ya Dar ndipo atangaze hadharani. Hatokuta Chidibenzi. Atawakuta "wenyewe" na umma utapata kilicho bora. Atakutana na wengine aliowazindulia makampuni yao. Atakutana na kada mbalimbali: polisi, wanajeshi, wafanyabiashara, wachungaji, waombolezaji, maaskafu nk. Hapa Makonda atakuwa "tayari kufa." Lkn si hii bembea.
[HASHTAG]#UzalendoKwanza[/HASHTAG].
#MvurundoKidato_4 vepeee!

Majina ya wauza Madawa ya Kulevya: Kikwete anayo!

Siku atakayokwenda Ikulu kuomba iyo list ndio nitatoa dukuduku lng lao nawacha kiporo
 
Wewe nae huwa ni kanafki........
WATAJE HAO WAUZA Madawa hapa ndio mahala pake kuisaidia nchi hii.......
Mimi ni mnafiki lakini uo ndio ukweli utamkamata mtoto wa mfalme aliyepita?.....

Au unataka kurudi chato airport na ikulu ulivyojenga uko vyote viwe vichaka?........
 
Kama kweli Makonda ameamua kupambana na "maruhani" wa unga Dar, aache kubembea, aache mzaha na kina Mr. Blue. Aende Ikulu, majina yao yako mezani kwa JPM .... Atakutana na wengine aliowazindulia makampuni yao. Atakutana na kada mbalimbali: polisi, wanajeshi, wafanyabiashara, wachungaji, waombolezaji, maaskafu nk. Hapa Makonda atakuwa "tayari kufa." Lkn si hii bembea.
Bila shaka atawakuta na waliouchangia mkoa madawati ya Elimu Bure
 
Lakini amejaribu
Kwani hakuna aliyethubutu kuwataja hata hao mnaowaita vidagaa
Watanza tuache kukatishana tamaa
Na sio kupinga kila jambo
Hivi inahitaji ujasiri gani katika kumtambua na kumtaja hadharani Chiz Benz kwamba ni mwathirika wa madawa ya kulevya? mtu ambae mwenyewe amekiri hadharani, mhe Mwigulu alipata uthibitisho alipokwenda kumtembelea mama yake mzazi,alishapelekwa sober house halafu leo unasema Makonda amethubutu?

Naona ile siku ya wajinga duniani mnailazimisha kuwa leo Tar 2 Feb 2017.
 
Zamani ulikuwa ukisikia madawa yamekamatwa tulikuwa tunashuhudia yakiteketezwa na vyombo vya habari vikishuhudia. Sasa hivi utasikia flani amekamatwa na kete kadhaa halafu kimyaaaa!!!!!
 
Back
Top Bottom