Maneno ya faraja kwa viongozi waandamizi wa Serikali kuelekea Awamu mpya ya Taifa letu

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Unapoingia kwenye UCHAGUZI hasa katika nchi zinazoendelea kama ya kwetu upo uwezekano mkubwa baada ya matokeo viongozi walioshiriki kusimamia flani ashinde wakapoteza kazi baada ya kiongozi huyo kuingia madarakani.

Katiba yetu imempa mamlaka Rais kuteua na kutengua mtu yeyote aliyepo chini yake bila kuhitaji uthibitisho wa kwanini amefanya hivyo.

Tarehe 28/10/2020 tunakwenda kupiga kura kuamua Nani atatawala awamu ijayo. Katika kura hiyo yupo mtu ana wadhifa wa Wazuri mkuu Sasa ila Hana uhakika wakuwa Waziri mkuu baada ya UCHAGUZI bila kujali chama gani kitashinda. Kwa sababu wakishinda upinzani watateua PM wao na akishinda chama kilichopo pia atateua mtu mwingine au kumwacha aliyepo.

Wapo Mawaziri na Manaibu Waziri, hakuna mwenye uhakika baada ya UCHAGUZI atakua Waziri kwa sababu akiingia mpinzani atateua Baraza lake akichaguliwa aliyepo atateua Baraza lake. Hawa mawazir wa sasa wanayonafasi ndogo sana yakurudi kwenye Baraza kwa sababu chama kilipata wagombea kwa mwono wa Mwenyekiti hivyo Mwenyekiti anaweza akawa tayari alishawapanga kwenye safu ya Mawaziri wewe uliyepo ukakaa benchi.

Wapo wakuu wa mikoa na wilaya nao pia hawana uhakika kwa sababu upinzani Wana safu yao lakini pia CCM mgombea wao amepita maeneo mengi nakukutana na watu wengi waliomsaidia na ambao awali hakuwajua. Akiwateua hao wewe RC na DC tayari unarudi kazi yako ya awali uliyokua unafanya.

Wapo makatibu wakuu wa Wizara, ninyi anzeni kupaki kabisa kuondoka kwenye nyumba zenu mnazoishi. Katika kampeni wagombea wamebaini mapungufu makubwa saba huko chini, ninyi amkuweza kuyabaini hivyo wakipewa nchi wataanza na ninyi kushindwa kuwashauri vizuri wanasiasa kuhusu vipaombele vya wananchi. Kumbukeni ninyi ndio wataalamu wa nchi mnaowashari wanasiasa. Amkutenda vyema ndiyo maana kero zimekuwa nyingi sana.

Wakuu wa vyombo pia mnapaswa kujipanga kwa sababu wagombea wote wameona mnavyotenda na mlivyotenda wakati wa miaka mitano. Wamesikia wananchi wanasema nini lakini pia kuwakumbusha, Hawa wagombea wamekabiliana na mapokeo ya watendaji wenu huko mikoani. Yawezekana kazi nzuri aliyofanya RPC wa mkoa flani ikawa tiketi yake ya kua IGP baada ya uchaguzi sawa sawa na vyombo vingine. Jiandaeni kisaikologia kwamba hakuna namna mnaweza jiakikishia kuwepo kwenye nafasi zenu kwa mwaka mmoja toka uchaguzi upite.

Kama hao viongozi wataathirika Basi wakurugenzi hawapo salama, wapo watakaorudi wizarani au kwenda nyumbani. Jiandaeni kisaikolojia.

HAYA MANENO YATATIMIA NDANI YA MWAKA MMOJA TOKA SERIKALI MPYA IAPISHWE.

Kwanini nimewaandikia haya, nimeandika kuwakumbusha ninyi viongozi na familia zenu mnalo jukumu lakufanya kazi kwa kumtegemea Mungu kuliko kufanya kazi kwa kumfuraisha mwanadamu. Nimeandika kuwakumbusha kwamba, wale wote mliosikia wanapewa ahadi za ajiri kwenye majukwaa ya siasa au vikao vya ndani Basi awakuahidiwa nafasi mpya kimuundo bali waliahidiwa nafasi yako. Weka mizigo yako sawa ukielekezwa kuondoka usipate presha mtoa riziki ni Mungu na si mwanadamu

Uchaguzi mwema
 
Back
Top Bottom