Nimeonja pendo lako

Nimeonja pendo lako

Nimeonja pendo lako nikajua u mwemaaa,nitakushukuru nitawainua wote wakusifu wewe!

Na upole wako Bwana,na huruma yako wewe,umenitendea wema usiopimika,Nitakushukuru na kukutukuza wewe.

Kina baba simameni ukapige makofi*2
rudia kiitikio.
Tumsifu GOD
Ngurumo za upako siyo!!!Bwana ni mwema poke makofi yangu shangwe na vigele gele Ameeeeen...........God bless you.
 
1. Nimeonja pendo lako,
nimejua u mwema
Nitakushukuru
nitawainua wote wakusifu
wewe
Nitawaongoza wote waimbe
kwa furaha
Nitakushukuru
nitawainua wote wakusifu
wewe
Ukarimu wako ee Bwana,
na huruma yako wewe
Msamaha wako ee Bwana,
na upole wako wewe
Umenitendea wema
usiopimika
Nitakushukuru
nitawainua wote wakusifu
wewe.
2. Kina mama simameni, piga
vigelegele -
Kina baba nyanyukeni,
mkapige makofi -
3. Watu wote nesanesa,
chezeni kwa furaha -
Inua mikono juu,
mshangilieni Bwana -
4. Watawa washangilie,
makasisi waimbe -
Walei warukeruke, waseme
aleluya -
5. Vitambaa mikononi,
vipeperushwe juu -
Na vichwa viyumbeyumbe,
kwa mwendo wa kuringa -
6. Nitakushukuru mimi, na
nyumba yangu yote -
Nitayatangaza haya, maisha
yangu yote -
 
Haka kawimbo kalikua kananikoshaga sana kipindi hicho ndo ministranti(Altar boy)
 
Ujumbe mzur unatumia vizur smart phone yako mungu alikupa nawe unaitumia vema kuelimishia jamii nasiyo kudownload pono
 
Japo umeuliza kibaa baa nakujibu tuu... mtunzi ni Bernad Mukasa, mtunzi mahiri wa enzi hizo...lakini hazikumtoa sana kwani enzi hizo muziki wa injili ulikuwa haulipi kidunia dunia kama sasa, ila ukweli nyimbo zake ni tamu mno
Real
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom