Nimeona Samaki Aina ya Papa Mnadani Lamu Mombasa

Nimeona Samaki Aina ya Papa Mnadani Lamu Mombasa

Najua hilo! Mm nmefanya biashara ya uvuvi pia papa Nlikuwa nafukuzia mapezi unajua kuna papá mweusi na Mweupe yaani aina ya sumbwi na sarawanzi hao ni aina ya papa

Ova
Nilikuwa nafanya biashara ya kuuza meno yao kwa watalii
 
Habari ya saa hii jameni,nimeona papa wa urefu kama futa tatu na ushee akiuzwa kwa soko ya samaki.

Swali nataka uliza😛apa analiwa? Because once nilipata kusikia wako wenye sumu hawafai kwa kukula.

Just curious mazee
Kwetu Tanga tunakula. Anakaushwa vizuri tu. Zamani tulikuwa na soko kabisa maarufu kama mabadanda ya Papa
 
Hata nyama pori unawezaipaka chumvi na kuianika.

Kwa papa nawezakumalizia ugali wako wa kilo mbili peke yangu. Apikwe na nazi, nyanya chungu (Ngogwe) bamia na pilipili. dah hapo sijaongezea mchunga wa nazi uliokamuliwa kidogo ukabakishwa ule uchungu kwa mbali😛😛😛
Binzari isikosekane hapo kwenye mchuzi. Papa ni mtamu
 
Back
Top Bottom