Sio hana akili , kwa uzoefu wang, mwanaume(shetani) sa nyingine anakuwa na katabia cha kujaribu , sasa mwanamke(yesu) unaejaribiwa unatakiwa utumie akili. Shida ni kwamba yeye ndo anatengeneza mazingira ya kuliwa tunda , anatakiwa asimfeel jamaa , ajiepushe mbona inawezekana.kwanza mwanaume anaekutaka na wewe ni mke wa mtu jua hakupendi wala hana akili
anakupenda kwa sababu anajua wewe ni cheap huna gharama na akishakukula atakuzarau kama takataka vile na kukutangaza utashangaa unatongozwa na ofisi nzima
Ha haaaaaaaaa bora aje kwangu au sioachana na huyo shetani dear hata kama una nyege bora ukapige game mbali huko heshima hainunuliwi mamii
Angalia mazuri tu ya Mme wako usiangalie mabaya alafu hurumia watoto maana hujui huyo jamaa anamatatizo gani mfano magonjwa ukimwi which will affect your kids. Mwogope Mungu na uone hiyo sauti ya mwanamme ni shetani katika ukware wa kukupotezea reputation yako. Be careful mwombe sana Mungu akupe jicho la tatu katika hili. Kitendo cha masaa machache kitakuharibia heshma yako iliyopo milele
.....Huyo mwaname ameshamsoma movement zake na kugundua kwamba anamtaka na anajiketa, ni suala la muda tuu, ndiyo maana anazidi kufukuzia.Kuna wanaume ving'ang'anizi kasha jua wewe ni mke wa mtu lakini bado anajisogeza kuna siku ataangukia pabaya.
iulize kwanini ulivyozingua aliuchuna wiki nzima...
Ungekuwa mke mwema hata hayo mazoea na huyo MUHUNI usingeyaendekeza, na MUMEO usingemuita JAMAA...
Halafu utatafunwa, kuvunjiwa ndoa na kupigwa chini fasta. Jiulize kwanini ulivyozingua aliuchuna wiki nzima...
Wakuu nahitaji mawazo yenu kwa kipindi hiki cha majaribu nachopitia.
Mi nimeolewa nna miaka kama 9 kwenye ndoa na kwa kipindi hiki chote nimepitia mazuri na changamoto pia ila sikuwahi kujutia ndoa.Jamaa aliyenioa ni msomi na anajua kuitafuta hela.Kiufupi tuna maisha mazuri nina kila kitu nachokihitaji km nyumba,usafiri wa maana na two beautiful kids.
Ktk kipindi cha ndoa nimepitia changamoto kwa huyu mume wangu.Kiufupi anapenda starehe pombe kwa sana na company za washikaji.Me sio mnywaji wala sitoki kiivo nikitoka job ni home kuangalia watoto na nyumba.Kiufupi ni mke mwema flan!!yes najiamini kwa hilo.Jamaa nishafumania msg za wanawake mara kibao ila naishia kusamehe na sikuwahi kuwaza kulipiza.Huwa nasali sana nikipitia hizi changamoto na Mungu ananivusha salama.
Sasa basi kilichonifanya nilete huu uzi jamvini ni situation niliyonayo now.Kiufupi miezi km 6 iliyopita nimekutana na jamaa ktk kazi flani.Jamaa ana mvuto na alikua ananipa attention flan ivi throughout..Tuliclick haraka sana tukawa close.Ilitokea tu sijui kwa nn..Nilinotice jamaa ananicare vby sana. Mwanzo nilichukulia poa ila siku zilivoendelea kwenda nikaanza kumfeel taratibu.
The eye contact was awkward btn us na imefika mahali najiona nashindwa kuresist.Nikiwa nae under one room nashindwa kabisa napoteza uchangamfu naishiwa pozi kbs.Jamaa anaonyesha interest za wazi ila najikaza knowing kwamba am married ataniona a cheap woman.
Huwa tunaongea mambo mengi na ananieleza issues zake kibao.Kuna siku alinifungukia ila nikavunga nikamwambia its better tuwe mbalimbali coz me ni mke wa mtu na siwezi cheat on my husband.Baada ya hapo akanikaushia km wiki.Aisee nilikonda kwa mawazo.Baadae tukaanza kuwasiliana upya na jamaa anaomba kidate na mm anataka tuspend tym wawili.Kashanialika kwake mara kibao nachomoa.Imefika mahali najiona ntashindwa huko tunakoelekea siko.
Kiufupi kinachonitatiza ni haya yafuatayo:
1.jamaa anajua me ni mke wa mtu so its obvious anataka game tu hakuna mapenzi.
2.Since ni coworker baada ya game ntamwangaliaje ofcn?
3.Naogopa reputation yangu among my workmates wakijua nimetoka na jamaa since wanaume hawana siri.Aisee mi ni mdada nayejiheshimu na wananiona nina bonge la mume.
4.Namfeel mno jamaa na siimagine kupotezea hizi feeling.Ni mtu anayenifanya niwe happy muda wote,confident about myself na I feel lyk a woman again.
Wakuu nisaidieni namna nitakavyohandle hii situation maana naumia kiukweli natamani niuridhishe moyo wangu ila nawaza consequence,kumpotezea jamaa nashindwa naumia at the same time sitaki kuharibu maisha yangu.
Nadhani hujanielewaHapo kwenye bold unaonyesha kama vile mgeni kwenye hayo masuala.
Una akili na iman ungeendeleq kusoma zaid ungekua kama Nyerere(jokes)Usijaribu kugegedwa na mfanyakazi mwenzako tena ofisi moja...
1. Hatokuheshimu
2. Hutokua huru ata ukitaka kumuacha kutakua na woga fulani na vizuizi
3. Ukipata nafasi ya juu utashindwa kumuongoza
4. Ofisini wakijua kua mke wa mtu unagegedwa na kijana hapo watakudharau tu.
Hizo ni feelings tu, trust me... Humpendi huyo kaka! Matatizo ya kwenye ndoa yako ndo yanasababisha yote hayo. Umesema wewe ni mke mwema, endelea kua mke mwema na achana na mihemko ya kijinga... Ukilala nae huyo inaonesha umekata tama kabisa katika ndoa yako, ata Mungu hawezi kukusaidia. Hurekebishi kosa kwa kosa kipenzi...
Kama unatafuta pa kutolea stress basi tafuta hobby... Nunua swimming costume kaogelee...
ni kweli mkuu watu wanacheat sana hata huyu mama anaruhusiwa kucheat sema tatizo lake anataka kupiga tukio la mtyu wa karibu ni very risk atafute chimbo la mbali hukoNdo maana nimesema kwenye post nyingine hapo juu kuwa michango ya wanaume wengine kwenye huu uzi ni very interesting.
My understanding is that it takes two to tango, meaning that hata mume wake anahusika kwa hili. Vinginevyo, mke wake asinge-develop hisia kwa mtu mwingine.
Kama mleta mada atafanya yote alivyoshauriwa hapa, hakutakuwa na mabadiliko mpaka pale mume wake atakapotambua tatizo na kukubali kubadilika pia.
Ila ukweli ni kwamba wake za watu huwa wana-cheat tena sana tuu sema they know how to do it bila kukamatwa.
Well SAID!!!!Dada pole sana ila nitakushauri nankukuuliza kwa kauli tofaut na wenzangu,,,hua sina kauli nzur sana hvyo nisamehe maana ukikereka ndio vzr ndio utakua umeelewa,,
Binadamu wengi vichwa panzi wanaamin kwamba ukijua kuitafuta hela na kuipata,,ukawa na mirad mingi unakua umefanikiwa,,, nonsense..
Binadamu tukiwa tunapata pesa wengi tunasahau tulipotoka,umejiuliza kwa nn mumeo ni mlevi?? Sawa unasali sana hua unaombea mumeo aachane na shetan wa pombe??
Binadamu hasa MWANAUME huwa hakataliwi kwa maneno tu,,anakataliwa kwa vitendo,,we umejiweka karibu then unataka ushauri kweli?au unamtaka unaigopa tu kusema hapa jukwaani?
Pole sana kwa unayopitia so ina maana huku jukwaan zikifika comment 200 na 150 inakushauri umpe jamaa hyo BWIMBWI YAKO utakuja kutupa mrehesho hapa??
Ndoa yako na watoto wako vina thaman kuliko dushe la huyo jamaa anaetaka kukumwagia mizungu yake bas,,,umeipigania ndoa miaka 9 halaf karagos mmoja aje kukuzuzua kwa kipi haswa?? Mm ni mwanaume tena mwanaume naejielewa na mwnye misimamo lakin tabia za wanaume unazijua vzr akishakupa bakora zake??
Kumfumania mumeo kwa sms au vip sio kigezo cha wewe kurudisha kisa umemfuma sms kwa simu yake..
NB: maisha ya kupata pesa na kumiliki vingi sio kwamba ndio mafanikio pekee,,mafanikio ni kua na vingi ambavyo pesa haiwez kununua,,umefanikiwa katika sekta ya maisha ila unataka kuyachezea mafanikio yako ktk liwazo la mwili na hisia duuuh,,,kitu pekee kisichoisha kwa mwanadam yaan kisicho na limit ni uvumiliv,vumilia na muepuke sana na umkatalie kwa vitendo sio maneno...
Karibu tusikilize nyimbo ya 4 NON BLONDES- whats up
Tchao