It takes two to tangle. Kweli kizazi chetu cha sasa hivi kimekomaa tu na "kudumu" katika Ndoa, haijalishi huna furaha wala nini, wewe kaa tu humo hadi kifo kitakapokukuta. Kila mahusiano au hata kuwa single kuna changamoto na Uvumilivu unahitajika , but mahusiano yanapokuwa "project ya Uvumilivu", that's too much Abeg
Kuna watu wanaishi kwenye ndoa ila mioyo, akili, hisia na utu wao umekufa kabisa. Ni vile tu hawezi kutoka humo kwenye ndoa, kwanza jamii itamuonaje? Mpumbavu aliyeshindwa ndoa? Hawa wanaume ni kama maboss kwenye ndoa, mke jitahidi tu kushikilia ndoa yako, ukichoka ndo na ndoa imechoka, mume yeye hahusiki katika kuitunza ndoa. So sad, sijui watoto wetu wa kiume watakuwa waume wa aina gani huko baadaye