Nimenenepa isivyo kawaida

litutumbwe

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2023
Posts
731
Reaction score
1,378
Wanajamvi za muda huu. Kilichonileta jamvini kwa wajuvi muda huu ni ili tatizo langu linalonisumbua. Nimevunga nimeona hali inazidi kuwa mbaya na hivyo kulazimika kuliweka wazi.

Mimi kiasili nina mwili wa wastani tu, mwaka jana kati kati nikaanza kunenepa. Nilichukulia ni hali ya kawaida. Ila nilizidi kunenepa na kg kuongezeka.

Hivi hapa nilipo nina kilo 95 kasoro. Ngozi ya paji la uso imeshuka chini. Nikiwa nasali wakati wa kula chakula huku nimenyosha mikono, ngozi za vidole zinaning'inia chini na kuchezacheza.

Nikivua nguo tu mwili unafutuka futuka mpaka nahisi aibu mno kwa mpenzi wangu. Chooni kwa kupima tu haraka haraka najisaidia kinyesi kilo kasoro kwa mkupuo. Kama nikiwa kijijini basi natumia maji ndoo kubwa iliyojaa kukamilisha shughuli nzima.

Naumia mno ndugu zangu. Shingoni nyuma yakichwa ngozi zimejikunja kunja hali inayonilazimu kuvaa kofia walau niifiche hali hiyo.

Nikiwa napeleka moto inanilazimu tumbo langu lote nilikusanye na kulimwaga juu ya tumbo la mpenzi wangu. Kama ni dog basi tumbo langu nalimwaga juu ya mgongo wake.

Hali hii mpaka lini?

Nachoka kuandika msaada tafadhalini.
 
Hahahah pole Sana mkuu...sema kuna watu wanahitaji kunenepa lakn so kwa unene unaouelezea hapa...
.punguza kula jinyime mkuu na tizi kidg...

Cheza mpira hata kama utakuwa unaugusa Mara mbili jua linazama fresh, kitendo Cha kutembea huku na kule ukiwa uwanjani utaburn fat kwa wingi mwezi mmoja tu utaona mabadliko makubwa sana.
 
Hahahaha!. Pole sana Mkuu..

Ningependa kujua ulaji wako kwa siku unakuaje? Unafanya majukumu yako wakati umekaa?

Kuna aina ya milo unapaswa kupunguza kama si kuiacha kabisa. Kuna aina ya vinywaji vya kula kwa macho tu.

Vizuri umejitambua mapema. Unaweza kujidhibiti.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…