Nimemuota jirani yangu akiwa chumbani kwangu usiku

MAKULUGA

JF-Expert Member
Jan 21, 2011
7,173
9,398
Ni tukio la kushangaza kidogo.

Majuzi nikiwa usingizini nilimuona jirani yangu akiwa chumbani kwangu ananiangalia akitabasamu! Nilipoamka alitoweka!

Ni binti mmoja ameshika Dini yake kwa mwonekano wa kibinadamu. Nimejaribu kulipuuza tukio hili nichukulie kuwa ilikuwa ni ndoto tu, lakini moyo unakataa kwa sababu nilipoamka nilikuta naweweseka sana.

Naamini hapa nitapata maelezo ya kina ya tukio hili na pengine ushauri muafaka!

Kinachoniuma zaidi siku hiyo sikuvaa chochote na kulikuwa na joto kali kwa hiyo hata shuka sikulihitaji!
 
Kama unavuta kete 3 punguza uanze kuvuta moja
Kama unaishi na mtu nyumbani kwako awe mwanao,Ndugu,mke,mine au mtu yeyote akikuambia jambo kama aliloandika hapa mtoa mada,usimpuuze,fanya utafiti.

Katika utafiti utagundua mengi,na hata kama sio kweli utagundua kua huyo aliokuambia habari Hiyo Ana matatizo makubwa na anahitaji kusaidiwa.

Pengine anaumwa,ameanza kuchanganyikiwa au vinginevyo.

Unaweza kugundua kuwa anafuatwa na wachawi,au wachawi wanaisumbua familia yako na Yeye kapewa nguvu na Mungu ya kuwaona.

Zaidi ya hapo unaweza kugundua Mambo mengine yasiyo ya kawaida.

Watu makini huwa hawadharau kitu.

Na Hiyo ndio akili.
 
Salute mkuu mi niliwahi kuchanjia dawa ya kuwaona wachawi mbona inatisha sana,walikuwa wakija chumbani usiku uchi
 
Back
Top Bottom