Nimemsikiliza Godbless Lema katika The Big Ajenda Star TV, yupo vizuri kichwani kuwazidi wapinzani wote hapa Tanzania

mm namuona ni mlalamikaji zaidi sio problems solver

Maani huwezi kuja laumu watumishi kulipwa pesa ndogo wakati vyanzo vyetu vya mapato vipo very limited.

Angekuja na experience ya huko alipotoka na kushauri tufanye 1, 2, 3 ili kukuza mapato yetu ili years to come tulipe maslai mazuri kwa watumishi wetu.

Tofauti na hapo lema ni mtafuta attention zisizo na maana.
Kukuza mapato wakati wanalaumu serikali kukusanya kodi na kukuza wio wa kodi. Hawa watu wanajua kulaumu tu ila solutions hawana!

Wanasema bodaboda ni laana, viwanda tuliua ambavyo vingeajiri hao bodaboda. Sasa waulize tunafufua vipi hivyo viwanda hawana majibu. Angesema tu kila kiwanda pale Arusha (General Tyre) yeye kama Mbunge alifanya jitihada gani kushauri au kwenda na mpango kazi bungeni/au hata Mkoani kufufua kiwanda unakuta hakuna alichofanya.
 
Wewe na huyo Lema wako wote viraza tu

Chukua idadi walimu + idadi ya polisi alafu zidisha na mshahara wa 1.5 M uone kama nchi itaweza kulipa huo mshahara
Kwaiyo wanalipwa mshaharamdogo kwasababu ya wingi wao siyo kazi wanayofanya non sense think twice
 
Kukuza mapato wakati wanalaumu serikali kukusanya kodi na kukuza wio wa kodi. Hawa watu wanajua kulaumu tu ila solutions hawana!

Wanasema bodaboda ni laana, viwanda tuliua ambavyo vingeajiri hao bodaboda. Sasa waulize tunafufua vipi hivyo viwanda hawana majibu. Angesema tu kila kiwanda pale Arusha (General Tyre) yeye kama Mbunge alifanya jitihada gani kushauri au kwenda na mpango kazi bungeni/au hata Mkoani kufufua kiwanda unakuta hakuna alichofanya.
Kumbuka huyo nimpinzan kazi yake nikushauri au umesahau kuwa lema mala nyingi amewekwa ndani na mkuu wa mkoa kwakusema matatizo ya Arusha
 
Anza na namba kumi na 11 kwanza kwa maana hayo mengine yametokana na elimu yake ndogo saaana
Ambayo hiyo namba 11 ni uongo? Elimu Tanzania ina issue gani? Nipe tofauti ya mtu mwenye elimu na asiye na elimu hapa Tanzania. Tuanzie na dawa ya Covid aliyokunywa Profesa Kabudi hadharani toka Madagascar ikiwa haijadhibitishwa Kimaabara.
 
Kumbuka huyo nimpinzan kazi yake nikushauri au umesahau kuwa lema mala nyingi amewekwa ndani na mkuu wa mkoa kwakusema matatizo ya Arusha
Niletee hapa clip au quote yeyote ya Lema akitoa mchango chanya iwe bungeni au popote kuhusu kufufua kiwanda cha General Tyre.
 
Lema ana Akili nyingi Sana Kichwani na pia ana Huwezo mzuri wa kuchambua Mambo ya kiasiasa ,kiuchumi,kijamii na kiutamaduni.

Watz Wamefungwa Akili na wanaamini umasikini ni mpango wa Mungu kumbe sio kweli .

Nimeshtushwa alipoongelea Mwalimu kulipwa lakitano na Askari police anayeanza Kazi kulipwa laki nee. Sasa kwa huu mshahara huwezi hata kujenga nyumba Wala kusomesha watoto shule za maana zaidi ya kuendelea kuwa masikini wa kutupwa.

Kiufupi Chadema wamuongezee Lema ulinzi mkali maana huyu ndo nabii mbeba maono tuliyekuwa tunamsubiri mwana wa Adam

Nillikuwa sitaki kupiga kura lakini lazima nipige kura 2025 na ntaajiandikisha Arusha badala ya Bukoba Ahsante Sana Lema.
Sasa mbona alipokuwa Mbunge hakutoa hoja kuwa Bajeti ya Bunge ipunguzwe na kupelekwa kwa Waalimu na Askari?
 
Tz Walimu zaidi ya 70% wanapokea pesa taslimu chini ya 400,000/- ma-bank wanawafaidi kuwakopesha na kuwakata, ma-heslb yanawakata bila huruma na lichama lao lahovyo kuliko chama chochote hata cha walevi kinaitwa CWT Kaziyao nikuwaibia hakiwezi kutetea jambo lolote! Kinawaibia hela mpaka aibu.
Mwalimu akiita mwanafunzi mjinga namshangaa sana, bora mtoto kuliko mtu mzima mjinga anayeongozwa na lichama lakinyonyaji CWT.
 
Ninachokiona kwa Lema ni kupinga uamsikini kwa nguvu zake zote. Yaani hauvumilii umasikini kabisa, ndio maana anaukemea kwa lugha ngumu. Tatizo anakemea umasikini kwenye jamii iliyoridhika na umasikini. Kwenye jamii ambayo umasikini ni ufahari, ni ngumu kidogo Lema kueleweka.
Anakejeli njia za kuishi za watu wa kipato cha chini ambao ndio wengi kote barani Afrika. Umasikini sio 'pepo' la kukemewa ili litoke, labda kama anaamini hivyo, which is delusional.
 
Anakejeli njia za kuishi za watu wa kipato cha chini ambao ndio wengi kote barani Afrika. Umasikini sio 'pepo' la kukemewa ili litoke, labda kama anaamini hivyo, which is delusional.

Ni kweli kabisa, kwenye jamii ya watu walioridhika na umasikini, anachokiongea Lema huchukuliwa kama kejeli. Lakini bila lugha za watu kama kina Lema, watu wataendelea kuona umasikini ni ufahari pindi watakapoitwa wanyonge na wanasiasa matapeli.
 
Ambayo hiyo namba 11 ni uongo? Elimu Tanzania ina issue gani? Nipe tofauti ya mtu mwenye elimu na asiye na elimu hapa Tanzania. Tuanzie na dawa ya Covid aliyokunywa Profesa Kabudi hadharani toka Madagascar ikiwa haijadhibitishwa Kimaabara.
huwezi ona tofauti kwa maana nawe umeweza kuwa mateka wa mtu aliekimbia umande kama Lema itakuwa vigumu kukupa ufafanuzi wa tofauti iliyopo
 
Sasa mbona alipokuwa Mbunge hakutoa hoja kuwa Bajeti ya Bunge ipunguzwe na kupelekwa kwa Waalimu na Askari?
Umesahahu kuwa huyu nyumbu ubunge ndio ilikuwa ajira yake ya kwanza .Na kwa kuwa alikuwa kwenye juhudi za kujiweka sawa bada ya kupata ajira leo baad ya kushiba anaanza kejeli
 
Ambayo hiyo namba 11 ni uongo? Elimu Tanzania ina issue gani? Nipe tofauti ya mtu mwenye elimu na asiye na elimu hapa Tanzania. Tuanzie na dawa ya Covid aliyokunywa Profesa Kabudi hadharani toka Madagascar ikiwa haijadhibitishwa Kimaabara.
Kwa hiyo ni sifa kutangazia umma kuwa yeye ni mchagga ? ili iweje ?kwa taarifa yako huyu nyumbu sio mchgga bali ni mmachame ambao wanajificha kwenye kivuli cha uchagga
 
Kwa hiyo ni sifa kutangazia umma kuwa yeye ni mchagga ? ili iweje ?kwa taarifa yako huyu nyumbu sio mchgga bali ni mmachame ambao wanajificha kwenye kivuli cha uchagga

Nimesema weka mtiririko wa huo mjadala ilikuwaje akafikia hitimisho la kusema kuwa yeye ni mchaga. Sio ubebe maneno utakayo kwenye maelezo yake, kisha uje uyalete hapa kwa lengo la kubeba nia yako ya upotoshaji wa kijinga.
 
huwezi ona tofauti kwa maana nawe umeweza kuwa mateka wa mtu aliekimbia umande kama Lema itakuwa vigumu kukupa ufafanuzi wa tofauti iliyopo

Nimekuambia Profesa Kabudi ni msomi, nikakupa na mfano wa yeye kunywa dawa ambayo haina scientific proof mbele ya umma. Sasa kwa kitendo kile kuna utofauti gani kati ya msomi na ambaye si msomi? Sioni kama una majibu zaidi ya porojo.
 
Ni kweli kabisa, kwenye jamii ya watu walioridhika na umasikini, anachokiongea Lema huchukuliwa kama kejeli. Lakini bila lugha za watu kama kina Lema, watu wataendelea kuona umasikini ni ufahari pindi watakapoitwa wanyonge na wanasiasa matapeli.
Hakuna mtu anapenda umasikini, hali ya nchi leo hii ni bora kuliko ilivyokuwa 1961, maendeleo ni mchakato unachukua muda, kauli za lema hazibadili chochote wa kuharakisha maendeleo.
 
Hakuna mtu anapenda umasikini, hali ya nchi leo hii ni bora kuliko ilivyokuwa 1961, maendeleo ni mchakato unachukua muda, kauli za lema hazibadili chochote wa kuharakisha maendeleo.

Sasa kama kauli za Lema hazibadili chochote, ww nini kinakuliza?
 
Back
Top Bottom