Nimempenda sana msichana huyu!!

yantuzu

Senior Member
Dec 10, 2011
115
16
Hello wana JF wenzangu! Ndugu zangu kuna Binti mmoja nimekutana naye katika mtandao wa kijamii wa Facebook. Ki ukweli sijaelewa hata ilikuwaje hadi akawa friend wangu, ila nakumbuka niliona tu friend request yake na mara moja nikamkubalia kuwa one of my friends. Mara nyingi huwa si-add watu ambao siwajui lakini kwa huyu sikufikiria mara mbili, mara moja nilimkubalia.

Niliangalia profile yake kama kuna "Mutual friend" lakini sijaona. Maramoja nilianza kuchat naye na nikagundua kuwa ni Single girl na mimi ni single boy hivyo baada ya kujuana kwa siku kadhaa nimejikuta nampenda sana yaani kiasi kwamba yakipita masaa mawili sijaongea naye nakuwa mpweke sana.

Bado hatujaonana face to face, na yeye ana wasiwasi kuwa pengine tukionana naweza kumtosa hivyo wakati mwingine ana-hestate kuwa na mimi full hadi tutakapoonana na kuongea, last wk ndio kamaliza Elimu ya University pale UD na wk 2 zijazo nitaonana naye maana atakuja huku mahali nilipo coz nimemtafutia job tayari.

Sasa ndugu zangu mawazo kwangu ni jinsi ambavyo ninamatarajio makubwa sana kutoka kwa yule binti, je kama atakuwa tofauti na ninavyotarajia nifanyeje maana nimekuwa crazy sana juu yake?? Je yeye ndiye? Hebu wadau mnisaidie mawazo hapo!!
 
Tatizo hujawa muwazi,kwanza swala la muhimi ni wewe unatarajia nini??maana kama umeongea nae siku zote kuna mambo unatarajia.Unaweza kuwa unatarajia ni mrefu kumbe mfupi ni mfupi kumbe mrefu,ni mweupe kumbe kweusi maana picha nazo simchezo.Sasa kwaza matarajio yako kisha ushauri wangu.Au unawasiwasi atachukua kazi na kusepa??Kumbuka usione vyaelea vimeundwa.
 
Hee, utoto bwana, eti yeye ndiye? sasa sisi tunajuaje

Hivi unataka kushauriwa kwa hili?
tuusemee moyo wako? khaaa jamani.
Haya kwa vile uko crazy over her ingawa hatujajua umempendea sura au nini? basi kubali yote.
 
mh,mambo ya mtandao duh. . . kaka mahusiano ya style hyo ni ngumu kuendelea ku-exist. make kila m1 wenu ana imagination zake. yan ushamuumba hyo dada mpk na nguo ukamvalisha hadi make up ukampaka,cku ukikutana nae thn ukute ni tofaut na ulivyotarajia utakuwa very disappointed. we onana naye kwanza ndo utajua kuwa unampenda ama la. . . huez sema ur crazy over her kwa kuckia saut na kuona pics zake tu. u need to see each other first. . . talk face to face e.t.c. n-way all the best!
 
Pole sana! Yaani wasichana wote uliowahikukutana nao hawakukupendeza isipokuwa huyo wa fb? Duh kweli kazi! Ninawasiwasi na uwezo wako wakufikiri na inaonesha wewe ni mtu usiye na msimamo na maamuzi yako. Poor wewe! Na kwahili lazima ujejuta siku moja. Kwakuwa umekufa kwa msichana usiye mjua subiri either kuzikwa or kufufuliwe naye utakapo mwona. Kila heri!
 
Sasa hapa unataka ushauri gani?????

Ni vizuri ukausikiliza moyo wako zaidi!
 
Mmh.. Yameshawahi kuota ndoto ya aina yako... Nilikuwa mpaka napanga harusi kwa mtu ambaye sijawahi kumuona... Lahaula... Tulivyokuja kuonana yaani alikuwa tofauti na vile nilivyokuwa nam imagine.. Communication iliishia siku ile ile ya kuonana... Nakutakia kila la heri lakini usipanie sana kwani kuna uwezekano mkubwa mmoja kati yenu akawa disappointed na muonekano wa mwenzie..
 
Me na kushauri jitayarishe kumuona alivyo mbaya- kwani haukutegemea.

Ulimtafutia kazi ili akuone wa maana, jiandae kwa lolote hata dharau,hapo atakapo gundua una magaga- kwani haukutegemea

jiandae kukute profile yake kule fb imebaki vilevile-single- kwani hakutegemea kuwa na wewe.

Jaribu kutulia mpokee vizuri mwambie jinsi unavyo mpenda zaidi ya ndugu zako na rafiki zako kwani haukuwatafutia kazi ume mtafutia yeye- kwani haukutegemea.
 
Hee, utoto bwana, eti yeye ndiye? sasa sisi tunajuaje

Hivi unataka kushauriwa kwa hili?
tuusemee moyo wako? khaaa jamani.
Haya kwa vile uko crazy over her ingawa hatujajua umempendea sura au nini? basi kubali yote.

umeona eeh! dada yangu wa moyoni. lolest mapenzi ya dotcom yanatabu. heri siye tuliokuwa tunachaguliwa na wazazi enzi hizo uhakika na uzuri wa mtu kisura na kitabia ulikuwepo kuliko hawa wa fb.
 
Pole sana! Yaani wasichana wote uliowahikukutana nao hawakukupendeza isipokuwa huyo wa fb? Duh kweli kazi! Ninawasiwasi na uwezo wako wakufikiri na inaonesha wewe ni mtu usiye na msimamo na maamuzi yako. Poor wewe! Na kwahili lazima ujejuta siku moja. Kwakuwa umekufa kwa msichana usiye mjua subiri either kuzikwa or kufufuliwe naye utakapo mwona. Kila heri!

Usimlaumu
 
mie mwenyewe nimekutana na mtu facebook,picha nilizoweka ni za 2010 sasa hivi nimenenepa ile kishenzi naogopa hadi kukutana naye,ila am falling for him jamani nisipopata text yake naumwa......mapenzi ya facebook mataaaaaaaaaaaaaamu ukimpata mtu wa ukweeeeeeeeeeeee.....
 
umeona eeh! dada yangu wa moyoni. lolest mapenzi ya dotcom yanatabu. heri siye tuliokuwa tunachaguliwa na wazazi enzi hizo uhakika na uzuri wa mtu kisura na kitabia ulikuwepo kuliko hawa wa fb.

Ha hahaaaa keshakuwa crazy halafu anaomba ushauri..... anataka tumkatili moyo wake...
 
Tatizo hujawa muwazi,kwanza swala la muhimi ni wewe unatarajia nini??maana kama umeongea nae siku zote kuna mambo unatarajia.Unaweza kuwa unatarajia ni mrefu kumbe mfupi ni mfupi kumbe mrefu,ni mweupe kumbe kweusi maana picha nazo simchezo.Sasa kwaza matarajio yako kisha ushauri wangu.Au unawasiwasi atachukua kazi na kusepa??Kumbuka usione vyaelea vimeundwa.

Matarajio yangu kwake ni makubwa, yaani the way nnavyomwangalia kwenye picha zake naona she is perfect for me...amejaribu kuwa muwazi zaidi kujielezea kwangu kuhusu figure yake n.k lakini kama ulivyosema picha haziaminiki! Kiujumla natarajia awe mchumba wangu na nimemwamini sana.
 
we endelea kujiongopea, usikute picha alioweka hapo face book sio yake, amka dogo tafuta wasichana kwa miguu kama babu zetu, achana na teknologia utalamba galasa
 
Uongo mwingine bana,yani mtu humjui,tayari ushampatia na kazi?
 
Back
Top Bottom