Nimempenda baba yake zaidi

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,738
215,921
Habari za J5 wapendwa

Huyu kijana tulifahamiana miaka miwili iliyopita, wiki iliyopita alinikaribisha nyumbani kwao nikamuone baba yake. Nimefika nyumbani baba alituandalia vizuri sana, baba anaishi peke yake na chakula aliomba kipikwe na caterer. Nimevutiwa Zaidi na ucheshi wa baba kuliko huyu rafiki yangu sasa jinsi ya kuswitch hapa ni shughuli.

Huyu rafiki yangu alizaliwa wakati baba yake akiwa mwanafunzi, na baba aliendelea na shule mtoto akiwa kwa mama yake. Miaka mingi ilipita mpaka baba kumaliza elimu, mama alishaolewa hivyo rafiki yangu alikuja kulelewa na baba akiwa teenager, baba alikuja kuoa lakini mke alishatangulia mbele za haki. Baba na mtoto wamepishana umri kama miaka 20 hivi, na baba ni wa kileo kiaina sasa hapa niko njia ya panda, kuwapotezea wote maana yake huyu rafiki yangu hatanielewa akisikia niko na mdingi wake.

Huyu rafiki hatujafikia kula tunda la katikati, lakini kwa mzee nimeishiwa kabisa. Ushauri jamani.
 
kaa nao wote bhana
 
Safari moja huanzisha nyingine....
Japo ulikuwa msemo usio rasmi lakini unakufaa.
Angalia kile moyo unataka usije ukaolewa na kijana halafu ukampa tamu baba.
Ningelikuwa huyo kijana wala nisingekuchukia ukiniambia kwani utakuwa mama.
 
Dadekiiii!!!!!
Umenikumbusha mwaka juzi kuna binti nilikua nataka nimtokee maana nilikua nampenda balaa. Sasa ikawa kila nikimfuata nipige nae story ananiambia eti oohoo nampenda BABA YAKO ANA MACHO MAZURI agriiiiii, yaani namuogopa mama yako tu lol. Ikabidi nimpotezee maana kwa jinsi fatha anavyopenda totoz inaweza kua alisha mmwaga maji maana hata fatha bado yupo 43yrs
 
Back
Top Bottom