Binti anataka kuharibu penzi la mama yake kwa baba aliyemlea tangu akiwa na miaka 7

Corluka Neven

JF-Expert Member
Apr 26, 2017
316
339
Leo Rafiki yangu kanisimulia👇🏻

Jamaa anasema, kuna mwamba alioa mwanamke mwenye mtoto wa miaka saba, akamlea yule binti kiroho safi kabisa na kwa upendo japo si bintiye akamsomesha inshot huduma zote jamaa akawa anatoa.

Baadae yule mwanamke wakafanikiwa kupata watoto wengine, sasa yule binti wa kumlea akawa mkubwa akapata kazi nje ya Tanzania now ni mtu anajiweza amejenga mjengo wake lakini bado hajaolewa. Lakini sasa Baba wa huyu binti yupo hai ila alioa mwanamke mwingine na wote wanakaa sehemu moja.

Jamaa anasema, binti anataka kufanya kitu cha ajabu sana yaani anataka Mama yake aachane na huyu mwanaume aliyemlea toka yupo na miaka saba ili Mama yake eti aolewa na Baba yake, sijui unaelewa? Yaani eti yeye awaunganishe wazee wake wakati Baba yake alioa mwanamke mwingine na akazaa naye na Mama yake pia aliolewa na akazaa watoto wengine na huyu Baba aliyemlea binti.

Sasa sijui atatumia mbinu gani kuwauganisha, dunia ina viumbe sana hii.

Mambo ni mchanganyo sana 🙌🏾
 
JF kuna watu wa ajabu sana, kuna kipindi mada zilizokuwa wanawake vs wanaume wenye vibamia (UUME MDOGO) gafla imekuwa vijana vs single mama.

je, tutafika na wahusika wanajisikia vipi huko walipo? Itoshe kusema JF tusiitumie kama jukwaa la kuwakatisha wengine tamaa na kuwapa msongo wa mawazo bila sababu.. Tuitumie kwenye kujifunza, kuhabarishana, kusaidiana na mengine yote mazuri.


Dini ya kweli ni kuheshimu dini ya mwenzako.

NIONGEZEE kali moja 🙄
 
Back
Top Bottom