eeehhhh!!!!! pole sana
Mentor mie naomba nikutabirie, sijui siku yako ya kuzaliwa ila June 2014 tarehe 1 hadi 10 utapata aliye wa ubavu wako. Na huyu hatokuacha hata iweje na wewe hutomkatia tamaa hata iweje. Sida itakuja kwenye kabila sina uhakika maana mara nyingi wachaga mnaoana wenyewe kwa wenyewe.
Kilala heri kuingia mwaka 2014.
Kitu kingine hata kama hizi unazoweka hapa ni hadithi, kumbuka kuwa in real life mdomo wako unaumba chochote utakachosema( mauti na uzima vi ndani ya vinywa vyenu), malmala nawapeni, funguo za mauti na kuzimu lolote mtakalofunga duniani litafungwa mbinguni na lolote mtakalofungua mbinguni litafunguliwa mbinguni) ni baadgi ya maneno aliyoyasema yesu kuonesha mamlaka tuliyonayo juu ya vinywa vyetu.
Shetani huwa anatumia sana vinywa vyetu kutuangamiza na tukikiri maovu au mabaya anatushtakia kwa mungu nae mungu wetu si muongo neno lake lazima litimie so utajikuta linatimia lile unalosema.
Fikiria mara ngapi umejitamkia daah mimi ni mzembe nimesahau kitu flani, au daah mimi ni mjinga nimesahau hela nyumbani things like that vinztufanya tuzidi kuwa wajinga au wazembe.
Najua wewe ni mtu wa dini (nime-refer signature yako) ila usipende kujikiria madhaifu kama ''bado nipo nipo sana'' in real life hata ukipata mke wa kuoa na kuweka matumaini lazima apotee maana umeshatamka sana haya maneno.
My advice: ingia mwaka 2014 bila kujitamkia maneno yatakayokurudisha nyuma na yale uliyokwishajitamkia yafute na yabaki na mwaka 2013 yasivuke kuja 2014.
Ukijaliwa kupata mke na kupata mtoto ntafurahi ukimuita Jael au Ebenezer Junior.