Nimemkumbuka Dr. Slaa

Nimemkumbuka Dr. Slaa

Chama kimebaki Instagram, Twitter na JF. Leo twende na membe, kesho tusimame na kamanda lissu. Siku si nying tutaambia tukimbie na makamba...
 
Huyo Dr Slaa wa kipindi hicho akikutana na huyu Dr Slaa wenu wa sasa ambaye ni balozi lazima wapigane na mmoja atamvunja mwenzake ule mkono.
 
"Nitakapo apishwa kuwa rais wa JMT, mwakipesile ukatafute nchi ya kwenda" maneno ya ukali na gadhabu ya Dr wilbrod Slaa wakati wa kufunga kampeni za uchaguzi wa mwaka 2010 pale jijini mbeya. Itakumbukwa kuwa mkuu wa mkoa wa mbeya kwa wakati huo John mwakipesile, alifanya kila aina ya figisu kuhakikisha Dr slaa hafanyi mkutano mbeya, kwanza umeme ulikatika jiji zima na pia polisi walikua wanachelewesha kuanza kwa mkutano ilihali mwisho wa kampeni ulikua saa kumi na mbili jioni. CCM walimuogopa Dr slaa, alikua na ufuasi mkubwa wa vijana waliokua wakitaka new regime

Nakumbuka nilikua kidato cha tano wilayani Rungwe mkoani mbeya, hivyo niliruka ukuta na masela na kusafiri mpaka mbeya mjini kumsikiliza Dr. Slaa was a presidential material, alikua anajua kuhutubia, anajua kujenga hoja, na msimamo mkali kwa vile anavyoamini. "Nikiwa rais elimu Bure toka chekechea mpaka chuo kikuu, nikiwa rais sitaki kumuona mtanzania anaishi nyumba ya tembe..." Rafiki yangu mmoja alikua afande pale mjini alininon'goneza "hakika hili jamaa hata mie natamani lichukue nchi".Hakika Dr slaa aliijua siasa.

Hata baada ya kuukosa uraisi dr slaa alipania kukijenga chama mpaka kwenye ngazi ya shina, CHADEMA ilipata uungwaji mkono mkubwa sana kipindi hiki. Kila ukivaa kombati za kaki mtaani ulionekana kuwa shujaa tena kamanda kweli kweli.
Kwa wakati huo kua chadema ilikua ni sifa tosha, spirit ya Dr slaa ilienea kwa vijana wengi wadogo nchini. Ilikua ni nadra kumkuta kijana ccm, wazazi wangu wote ni CCM ila walishangaa jinsi mtoto wao nilipokua nawapa shule ya upinzani. Nakumbuka mama alinambia... " mwanangu siasa haitakiwi uwaamini watu kiasi hicho, hyo ni kazi ya kutafuta kula kama kazi nyingine tu". Wala sikua na habari.

2015 mwenyekiti alifanya kosa kubwa sana ambalo litakitafuna chama kwa mda mrefu sana. Ile gia alioibadilisha hewani ilifungua vichwa vya vijana wengi ikiwepo mimi na kuamini kuwa siasa ya upinzani ya Tanzania ilikua ni ya viongozi wenye njaa, wasio na misimamo, na wenye uchu wa madaraka, eti mtu aliye ndani ya chama kwa mda mrefu, mtu aliyeshiriki kueneza Sera, hoja na propaganda ashindwe kuaminiwa na badala yake aje mtu tuliemtusi na kumpa kila aina ya tuhuma!!!. Lahaula ilikua kituko. Hakuna kampeni ziliojaza watu za upinzani, kama kampeni za kukemea ufisadi!! Kumbuka oparesheni sangara, Ile list of shame ya Dr slaa ilifungua milango ya fahamu ya watanzania kuhusu nchi yao. Lakini mambo yote haya yalibadiliswa ndani ya wiki mbili tu baada ya mwenyekiti kubadili gia angani na kumchukua kamanda dhaifu ambaye hakuwahi hata kuvaa kaki, ilionyesha dhahiri alikuja kimwili tu ila kiroho alikua kule aliporudi saizi. makamanda hawakuongelea tena kuhusu ufisadi badala yake tulizungushwa mikono kuimba mabadiliko.. Walio jikoni wana siri nzito juu ya nani alifaidika na uzungushwaji mikono huu.

Leo hii CHADEMA hujui kama wana katibu mkuu, jamaa yupo yupo tu. Vijana wao na wabunge wao wanaendesha siasa kiujanja ujanja tu. Wanadandia kila hoja mitandaoni, hawana zile amsha amsha za Dr wengi wamekaa kipigaji pigaji tu kusubiri kuunga juhudi. Eti wanashabikia kiongozi wa ccm kumchallenge magufuri 2020, inaonekana hata adui yao saizi hawamjui.
Binafsi niliistaafu siasa za Tanzania 2015 nikijikita zaidi na kutafuta namna ya kulea kizazi changu kijacho, sasa nimeamua kuwa mtizamaji tu... Upinzani una safari ndefu kwenda kuishika dola, huu ni ukweli mchungu kuumeza.

The irreplaceable.
Bila shaka Rais wa moyo wako alikuangusha!!
 
Mleta uzi umetumwa?
Uhuru uliokuwepo kipindi kile 2005-2015 ndio uliopo leo?
Vyama vya upinzani vilikuwa na nafasi ya kufanya mikutano ya siasa, je leo hii vyama hivyo vinaruhusiwa?
Unamlaum Mwenyekiti wa CHADEMA, kuna mtu amefilisiwa kama yeye?
Unawalaumu wabunge, katibu mkuu wote wa CHADEMA, unataka watupwe kwenye mifuko, wavunjwe miguu, wafilisiwe? Kuna watu wa upande wa pili au wale wapinzani njaa wamefunguliwa mashitaka na kesi za kila aina kama viongozi wa vyama halisi vya Upinzani?

Wewe mwenyewe umepumua tu kwa kuandika post ya kupongeza au kushabikia upande ule, reverse uone moto wake!

Kukaa kimya bado ni mbinu.
 
Dr slaa alikua mbunifu na mwanasiasa aliejiamini hakuogopa kupigwa mabomu pia alikua mjenga hoja makini ccm wakikua kwenye hofu kila waliposikia dr slaa atakuwa na mkutano na wandishi wa habari au wananchi wa kawaida dr alihamasisha sana wananchi kujiandikisha kupiga kura na kweli wakahamasika .usaliti alioufanya mbowe na kamati kuu yake kuleta kapi la ccm na kumtosa kamanda Dr slaa tena kwa maneno ya kumdhalilisha yeye na familia yake niliumia sana nikaichukia siasa ya nchi hii....Dr slaa kazunguka nchi nzima kutuliza hali ya siasa ndani ya chama baada ya zitto na genge lake kufukuzwa wakati mwingine anapondwa mpaka mawe..wakati huo mbowe na wajumbe wa kamati kuu wamejificha ndani lakini Dr yuko mtaani kuweka hali sawa alafu dakika za mwisho wanaleta jizi la ccm na kulikabizi chama Dr anatukanwa hovyo bila kujua kapiganaje kukijenga chama aisee MUNGU ni mwema amtupi mja wake acha ale mema ya nchi uko aliko chadema walimuona afai basi komaeni na katibu mkuu wenu uyo bubu
 
Siku hizi anatamka maneno "Mheshimiwa Rais, mheshimiwa waziri" Hakuwahi kutamka hivyo kwa miaka 24 iliyopita. Nikikutana naye nitamkumbusha ile hotuba yake pale Igunga.
 
...
Dr Mihogo alimkimbia Lowassa sasa Lowassa karudi aliko sijui itakuwaje
....njoo na hoja zinazo eleweka sio vioja namna dr slaa sio mwanachama wa chama chochote bali ni mtumishi wa umma...uyo lowasa mabadiliko wenu baada yakuwa mmemsafisha mkasema sio fisadi mkaramba uhalo wenu karudi kuwa mwanachama wa ccm...nyakati zingine muwe mnatumia akili zenu mnapotumwa na uyo makengeza wenu
 
Siku hizi anatamka maneno "Mheshimiwa Rais, mheshimiwa waziri" Hakuwahi kutamka hivyo kwa miaka 24 iliyopita. Nikikutana naye nitamkumbusha ile hotuba yake pale Igunga.
.....hahahaaa usisahau kumkumbusha mbowe nani fisadi namba moja tanzania....msigwa alisema mtu atakaemshabikia lowasa akapimwe akili ivi waliozungusha mikono wakiimba mabadiliko lini mtawapeleka milembe?
 
Huyo Dr Slaa wa kipindi hicho akikutana na huyu Dr Slaa wenu wa sasa ambaye ni balozi lazima wapigane na mmoja atamvunja mwenzake ule mkono.
..... hahahaaa kweli ndg Kama ambavyo mbowe aliesema lowasa fisadi na mbowe aliesema lowasa ndie mabadiliko na mkombozi wa chadema hakika siku wakikutana hapo ufipa lazima ngumi za moto zipigwe mpaka mmoja kengeza liishe..
 
Mleta uzi umetumwa?
Uhuru uliokuwepo kipindi kile 2005-2015 ndio uliopo leo?
Vyama vya upinzani vilikuwa na nafasi ya kufanya mikutano ya siasa, je leo hii vyama hivyo vinaruhusiwa?
Unamlaum Mwenyekiti wa CHADEMA, kuna mtu amefilisiwa kama yeye?
Unawalaumu wabunge, katibu mkuu wote wa CHADEMA, unataka watupwe kwenye mifuko, wavunjwe miguu, wafilisiwe? Kuna watu wa upande wa pili au wale wapinzani njaa wamefunguliwa mashitaka na kesi za kila aina kama viongozi wa vyama halisi vya Upinzani?

Wewe mwenyewe umepumua tu kwa kuandika post ya kupongeza au kushabikia upande ule, reverse uone moto wake!

Kukaa kimya bado ni mbinu.
Wabunge wote wameruhusiwa kufanya siasa kwenye majimbo yao. Vyama vyote vimeruhusiwa kufanya mikutano ya ndani. Kutoa press release pia kumebaniwa? Katibu mkuu anafanya hivyo? Sema kweli mashinji anaweza hata kujenga hoja yule?
 
Dr slaa alikua mbunifu na mwanasiasa aliejiamini hakuogopa kupigwa mabomu pia alikua mjenga hoja makini ccm wakikua kwenye hofu kila waliposikia dr slaa atakuwa na mkutano na wandishi wa habari au wananchi wa kawaida dr alihamasisha sana wananchi kujiandikisha kupiga kura na kweli wakahamasika .usaliti alioufanya mbowe na kamati kuu yake kuleta kapi la ccm na kumtosa kamanda Dr slaa tena kwa maneno ya kumdhalilisha yeye na familia yake niliumia sana nikaichukia siasa ya nchi hii....Dr slaa kazunguka nchi nzima kutuliza hali ya siasa ndani ya chama baada ya zitto na genge lake kufukuzwa wakati mwingine anapondwa mpaka mawe..wakati huo mbowe na wajumbe wa kamati kuu wamejificha ndani lakini Dr yuko mtaani kuweka hali sawa alafu dakika za mwisho wanaleta jizi la ccm na kulikabizi chama Dr anatukanwa hovyo bila kujua kapiganaje kukijenga chama aisee MUNGU ni mwema amtupi mja wake acha ale mema ya nchi uko aliko chadema walimuona afai basi komaeni na katibu mkuu wenu uyo bubu
Sijui niongeze nini hapo? Ndio maana mpaka Leo CHADEMA hawana wanachosimamia, hoja ya ufisadi iliyowapa jina inawatafun wenyewe saiz
 
Slaa kaondoka chadema kwa ustadi mkubwa sana, lengo ni kulinda reputation yake atakapukuwa nje ya chadema, na sasa anakula matunda ya kazi aliyoifanya.
Slaa nae ana reputation??
 
Back
Top Bottom