Nimemchoka sana mama yangu

Nimemchoka sana mama yangu

WW LAZIMA UWE WIFE MATERIAL UKIINGIA KWENYE NDOA SIO SIRI NATAFUTA WATU WA HIVI, WALIOPITIA CHANGAMOTO, HAKUNA LINALOSABABISHWA WASUMBUA SIO WABINYA SAUTI WENGINE HUKO MTAANI
Huko Pm nadhani kumeshajaa maombia ya uchumba!
 
Uswaze ndoa.. piga shule kwanza then mengine yatafata..hzo ni dalili za mafanikio kwenye maisha yako..
 
Pole sana dada yangu.
Anachokifanya mama yako analipiza kisasi kwa yote aliyofanyiwa na mzazi wake (baba yako)
inaonekana mama yako alikuwa anampenda sana baba yako na alikuwa anategemea ataolewa naye lkn imetokea kinyume kwahiyo anaona njia rahisi ya kulipiza kisasi ni kukuchukia na kukunyanyasa ww.
Hii hutokea sana kwa baadhi ya wanawake waliodhurumiwa penzi.
Wanawake hupishana kimtazamo na kihisia, wengine huwapenda sana watoto wao na wanaona ni kama ndiyo faraja yao lkn wengine wanakuwa km mama yako.

Kubaliana na hali na uone km ni ya kawaida tu ktk maisha. Msamehe mama yako na vumilia huku unatafuta sehemu ya kujishikiza yaan kazi.
Ikibidi amia kwa ndugu zako ukakae kuliko hapo sbb utazidi kujiongezea matatizo.
Ila hata ukipata kazi usiwadharau ndugu zako, au mama yako.
 
WW LAZIMA UWE WIFE MATERIAL UKIINGIA KWENYE NDOA SIO SIRI NATAFUTA WATU WA HIVI, WALIOPITIA CHANGAMOTO, HAKUNA LINALOSABABISHWA WASUMBUA SIO WABINYA SAUTI WENGINE HUKO MTAANI
Mr mwanamke kupitia maisha magumu haimfanyi kuwa wife material
Kuwa wife material ni zawadi kutoka kwa Mungu na siyo kila mwanamke ni wife material
Unaweza kumuoa mwanamke ambaye amepitia maisha magumu lkn baada ya kumhifadhi na kumpa kila kitu anachotaka anaanza kukudharau na kukuona hakufai.

Ndiyo maana tunasema Mke mwema au mume mwema hutoka kwa Mungu.
 
Kwanza pole sana kwa mtihani huo wa maisha, pili hongera kwa kuweza kukabiliana na tatizo hadi kufika hapa hadi kuweza kumaliza shule salama. Kinachotukutokea wewe, sio mwisho wa dunia, umefika nusu ya kutatua tatizo, maana umeshajua tatizo liko wapi. Cha kufanya waite mama zako wadogo na wazee wengine uwaelezee kwa kina suala hili, hakikisha unaweka katika maandishi kama ulivyoweka hapa, uwalezee kwa kina na kisha uwape hayo maandishi ili wao watafute namna ya 1) kukusaidia wewe kisakolojia maana unaweza kuharibikiwa zaidi, 2) wao watatafuta namna ya kuzungumza na mama yako kuhusu hali hiyo. Inawezekana mama yako kwa kuzibwa na hasira fulani au hofu, wala haoni jinsi anavyokutendea, ni kama amejisahau. Kuna uwezekano mkubwa kukawa na tatizo kati ya mama yako na baba yako katika mahusiano yao huko nyuma. Mwisho, anza mchakato wa kumtafuta baba yako, naye kaa naye mpe maelezo pamoja na maandishi, ikishindikana muandikie hata barua. Kwa kiasi kikubwa utakuwa umepunguza sana tatizo.
 
Njia sahihi ni kwenda Kwenye Kanisa la Kiroho mpokee Yesu Furaha Yako itarudi na wala hutajuta kamwe.Nina uhakika wa hili ninalo kwambia.
 
Pole sana mdada. Mungu Yupo Pamoja na ww. Hata me nlipata Matatzo kama ww lakn sasa Nnafanya kaz Mbal na familia yng. Kwa Ushaur na Kupeana Nguvu Njoo Pm. Asante
 
After abusing you emotionally for so long...now you have become heartless too and that is why you don feel love and possibly empathy to other people...so sorry!!!!
 
Daaah childhood sexual assault pia umepitia!!!...your brain psyche is no longer the same
 
Pole sana dada,mama yako anahasira sana sana na baba yako,amezipatiliza hasira hizo kwako.Hongera unakaribia kujitegemea kaza buti.
 
Habari zenu wapendwa,

Mimi ni msichana niliyemaliza chuo lakini natafuta kazi. Naishi na wazazi wangu na wadogo zangu wa kike ambao nawapenda sana. Nimekulia na kulelewa na bibi sana na mama mdgo ambao wote walikua wapole na wakarimu ila mama mdogo alitangulia mbele ya haki.

Nilimpenda sana mamdogo kuliko mama yangu mzazi kwasababu alinipenda na kuchukua nafasi ya mzazi wangu na ndiye aliyeniambia mume wake mama siyo baba yangu mzazi ( ila ni baba yao wadogo zangu ) nikiwa darasa la sita.
Niliumia sana kwasababu mama yangu alikuwa hana time kabisa kunieleza hayo. Hapo form one ndo nikaanza kuishi na mama yangu ila jamani ni mkali kwangu adi naliaga. Kuna siku nilimuuliza mama mdgo kama huyu kweli ni mama yangu mzazi au la akasema ndo mamako.

My mum hana ukaribu na mimi, ananifokea kila wakati bila hata sababu. Hanaga shukrani in anything i do. Uzuri darasani nilikua nafanya vzuri sana nikishuka position kidgo atafoka likizo nzima. Nilikua nashika nafasi ya nne nikiwa naongoza wasichana ila nikiwa tu wa tano ataongea likizo nzima.

Anavyokuwa ananiangalia, utafikiri yeye ndo mama yangu wa kambo hata akipiga honi ya gari getini nikiwa tu nje nilikua nakimbilia chooni. Anyway namshukuru kwasababu yeye ndo aliyenisomesha. (japo ni wajibu wake).

Tatizo ni pale mama anavyokuwa hana mother to daughter love au affection. Hajali what I do. Naweza kumuomba hela anakuwa mkali mpaka namwambia basi mama natafuta njia napata na haulizi ila wadogo zangu wanapewa hata extra. Mimi sijawahi kununuliwa simu na mama ila wao wananunuliwa tena mimi ndo namsindikizaga mama kununua na haniulizi mimi napata wapi simu.

Nikitaka tuongee labda angalau nimwambie kitu kinachonisumbua au just kupata faraja ya mama anaongea kwa ukali kwamba kachoka au bwanae ondoka ila roho inaniumaga. Marafiki zangu wanavyoongelea mama zao huwa nawatazama na kuwatamani.

Nyumbani kuna mfanyakazi lakini kazi zote nafanya mimi na mama humtetea dada na kusema mimi sina umuhimu ndani wakati kutwa nzima mimi ndo najishughulisha ila nakaaga kimya hadi nikiwa chuo nikija kusalimia huwa hataki niondoke ili nifanye kazi. Nikimwambia mama nina test atasema bwanae kwani wewe wa kwanza kusoma mpaka nakosa raha nikiwa chuo nakuwaga very lonely na mawazo. Sikufanikiwa kupata mkopo wala hela ya matumizi hvyo nilikua nahudumiwa na mama. Aisee sitokuja kusahau mateso niliyopata chuo.

Nimelala hungry nights mpaka ilibidi nizoee. Hapo ndo nikaona nitakufa nikaanza mahusiano na wanaume kisa nipate hela. Hapo mama uwezo anao wakunisaidia lakini anasema hana hela nitafute wanaume tena kwa ukali.

Anyway nilipunguza ukaribu na mama hata upendo kwasababu nilijaribu kuwa karibu nae nipate mapenzi ya mama lakini nikashindwa. Afu yeye ndo anasema nina roho mbaya, sina upendo kama wadogo zangu. Ninamwangalia tu kwasababu najua yeye ndo hanipendi. Na anasema hivyo kwasababu anawasikiliza sana yuko karibu nao but she pushes me away yaani utafikiri niliokotwa.

Kuna wakati huwa natamani niolewe ila ndoa ina majanga yake pia na sina hata mtu. Na hali ya mama imenifanya nikose upendo kwa watu wengne niponipo tu all alone. Kuna wakati nakaa tu na kulia na kinachoniuma nikiwa 7 yrs nilishawahi kubakwa kijijini kwa bibi na mfanyakazi ila sijawahi kumwambia mama wala mtu yeyote.

Watu watakua wanajiuliza mbona sitaji baba. Baba yangu ana familia yake mkoani na alishasahau kama ana mtoto. Baba yangu wa kambo yupoyupo tu but sana sana anawajali wanae ila hainiumizi roho. Ninachomuomba Mungu niondoke nipate kazi hata mkoani mbali na mama yangu.

NB. Wazazi wa hivi especially wamama jaribu kuweni karibu na watoto wenu kuweni na upendo. Mimi siwezi elezea kila kitu hapa ila umuhimu wa mamangu ni kunisomesha tu tena kwa maneno namshukuru sana kwa hilo.

Wapendwa sjui mtanisaidiaje but nimevumilia sana ni mama yangu huyo ndo maana wengne hukimbia kwao au kutaka ndoa haraka ili waondoke makwao.

Wazazi badilikeni tafadhali.
Kama umeweza kuvumilia kipindi chote hicho, endelea na moyo wa uvumilivu... Utapata kazi na uatasogea mbali naye...
But for sure when you will be far lazima atakutafuta with lots of regrets... Usimchukie maziwa yake ndio yamekufikisha hapo..

Polw saana
 
Pole sana Lady Jay, unaweza sema mama yako ana umri gani na wewe una umpri gani?
 
Easy, mama yako alimpenda baba yako mzazi, alitamani kuwa nae maishani, something went wrong, ndoto zake zikazimika, aliumia sana lakini tayari ulishapatikana wewe, baba wa kambo nae ana mapenzi na mama yako, sema hakupenda kuoa single mother, alijikuta tu. Kila akikaa na mama yako chumbani ana kazi ya kumsimanga tu kuhusu wewe, anamzidishia hasira mama yako ajute kwann alikuzaa mapema na bwana yule ambaye taarifa za ujauzito wako hazikumpendeza kwakuwa hakuwa tayari kuzaa na mama yako.
Huna makosa, just move on with yo life.
Mpende akupendae, asiekupenda let them go.
 
Haya yote ni maisha
Ipo siku yatakwisha
Ona leo nahangaika
Mambo yamebadilika...

Yote maisha - madee
 
Dah nimeckitika sana nanimejifananisha me nilivyo, mama yangu aliniacha (alifariki) nikiwa namiaka 6 ila kwawakat huo ckuona tatizo niliona kawaida sana ila nimekuja kumlilia mama yangu nilipofika darasa latano, mpaka Leo nataman sana uwepo wawazazi wangu ila asikwambie mtu mama mzazi nimzazi2 so cjui mama yako anatatizo gani
 
Back
Top Bottom