Nimemchoka sana mama yangu

Nimemchoka sana mama yangu

Pole sana
Wanasemaga hakuna mam wawili ila baba unaweza ambiwa kila siku! Muombe Mungu akusaidie kukupa upendo and fight for your life ukifanikiwa atakupenda tu! Sure i tell you!
 
Kwa kuwa umekaa kwenye tumbo lake miezi tisa, ni mama mzazi ila pole kwa yote, mpe tu upendo mpaka aone aibu na kuna siku atajirudi. Akikuambia kitu changanya na akili zako za utu uzima ili ujue namna ya kujibu. Kila la heri utafanikiwa kimaisha mpaka ashangae. Amen
 
Pole sana ,,, Mimi simlaumu mama yako....Wenda Baba yako mzazi ,,Alipompa mimba kuna jambo alimfanyia ambalo linamfanya amchukie sana huyo bwana ,,sasa kwamantiki hiyo kila anapokuona we kumbukumbu ya yule jamaa inamuijia basi linakua tatizo.

Mie nakuhakikishia ,,kitendo cha mama yako kukubali kulea mimba mpaka akakuzaa niupendo nautjibitisho tosha kua anakupenda ,,, ANGEKUA hakupendi Angeitoaga hiyo mimba .

Sababu nimama ,,just show her love ,, mponde ponde na mahaba ,,, kuna siku atakukumbatia nakukuambia '"" my daughter you are my world ,you are my life "" I love you.
 
Lady Jay pole sana ujumbe wako umenitoa machozi maana naisi Mimi nawewe hii historia inafanana kuna wakati nasema bola walio yatima wana jua hawana wazazi wana amani Mimi naelewa inatesa sana hii imepelekea kuzaa Na kuwa single mother maana unajikuta unajiingiza katika mahusiano bila kutalajia pole mamy Mungu yupo mapito hayo bado nayapitia Mimi pia sina mapenzi Na mama yangu hata kidogo katika maisha sikuwahi kuipata upendo,furaha, najikuta napenda mama Wa wenzangu najisahau kama sio Wa kwangu Kiukweli sina upendo Na mama wala baba mama Na baba wanachukiana sana nimejikuta nampenda babu yangu bila babu nisingesoma Leo ata la kwanza Mimi nilitupwa kwenye kapu nje Na mwezi mmoja my dear mengine hatuwez kuyasema ndomana naangaika nisake kazi niondoke Mimi ata line nitabadili
Pole sana.
 
Pole sweetheart, Mimi mama yangu Nilikuwa nikimuudhi anasema lione n kufanana marehemu baba yako siufe km baba yako Hata kuzaa hutokuja kuzaa Wakati huo ndo Nilikuwa nimeolewa na sababu ya kuwahi kuolewa ni hayo matatizo ya kifamilia chuki yake kwa baba akaihamishia kwangu matokeo yake nimemchukia Mara mia zaidi yake.
Pole sana dear but jitahidi tu umsamehe upate amani.
 
Nimeumia sana,pole sana.Muombe Mungu akupe kazi na mume bora.iko siku.vumilia tuu
 
Habari zenu wapendwa,

Mimi ni msichana niliyemaliza chuo lakini natafuta kazi. Naishi na wazazi wangu na wadogo zangu wa kike ambao nawapenda sana. Nimekulia na kulelewa na bibi sana na mama mdgo ambao wote walikua wapole na wakarimu ila mama mdogo alitangulia mbele ya haki.

Nilimpenda sana mamdogo kuliko mama yangu mzazi kwasababu alinipenda na kuchukua nafasi ya mzazi wangu na ndiye aliyeniambia mume wake mama siyo baba yangu mzazi ( ila ni baba yao wadogo zangu ) nikiwa darasa la sita.
Niliumia sana kwasababu mama yangu alikuwa hana time kabisa kunieleza hayo. Hapo form one ndo nikaanza kuishi na mama yangu ila jamani ni mkali kwangu adi naliaga. Kuna siku nilimuuliza mama mdgo kama huyu kweli ni mama yangu mzazi au la akasema ndo mamako.

My mum hana ukaribu na mimi, ananifokea kila wakati bila hata sababu. Hanaga shukrani in anything i do. Uzuri darasani nilikua nafanya vzuri sana nikishuka position kidgo atafoka likizo nzima. Nilikua nashika nafasi ya nne nikiwa naongoza wasichana ila nikiwa tu wa tano ataongea likizo nzima.

Anavyokuwa ananiangalia, utafikiri yeye ndo mama yangu wa kambo hata akipiga honi ya gari getini nikiwa tu nje nilikua nakimbilia chooni. Anyway namshukuru kwasababu yeye ndo aliyenisomesha. (japo ni wajibu wake).

Tatizo ni pale mama anavyokuwa hana mother to daughter love au affection. Hajali what I do. Naweza kumuomba hela anakuwa mkali mpaka namwambia basi mama natafuta njia napata na haulizi ila wadogo zangu wanapewa hata extra. Mimi sijawahi kununuliwa simu na mama ila wao wananunuliwa tena mimi ndo namsindikizaga mama kununua na haniulizi mimi napata wapi simu.

Nikitaka tuongee labda angalau nimwambie kitu kinachonisumbua au just kupata faraja ya mama anaongea kwa ukali kwamba kachoka au bwanae ondoka ila roho inaniumaga. Marafiki zangu wanavyoongelea mama zao huwa nawatazama na kuwatamani.

Nyumbani kuna mfanyakazi lakini kazi zote nafanya mimi na mama humtetea dada na kusema mimi sina umuhimu ndani wakati kutwa nzima mimi ndo najishughulisha ila nakaaga kimya hadi nikiwa chuo nikija kusalimia huwa hataki niondoke ili nifanye kazi. Nikimwambia mama nina test atasema bwanae kwani wewe wa kwanza kusoma mpaka nakosa raha nikiwa chuo nakuwaga very lonely na mawazo. Sikufanikiwa kupata mkopo wala hela ya matumizi hvyo nilikua nahudumiwa na mama. Aisee sitokuja kusahau mateso niliyopata chuo.

Nimelala hungry nights mpaka ilibidi nizoee. Hapo ndo nikaona nitakufa nikaanza mahusiano na wanaume kisa nipate hela. Hapo mama uwezo anao wakunisaidia lakini anasema hana hela nitafute wanaume tena kwa ukali.

Anyway nilipunguza ukaribu na mama hata upendo kwasababu nilijaribu kuwa karibu nae nipate mapenzi ya mama lakini nikashindwa. Afu yeye ndo anasema nina roho mbaya, sina upendo kama wadogo zangu. Ninamwangalia tu kwasababu najua yeye ndo hanipendi. Na anasema hivyo kwasababu anawasikiliza sana yuko karibu nao but she pushes me away yaani utafikiri niliokotwa.

Kuna wakati huwa natamani niolewe ila ndoa ina majanga yake pia na sina hata mtu. Na hali ya mama imenifanya nikose upendo kwa watu wengne niponipo tu all alone. Kuna wakati nakaa tu na kulia na kinachoniuma nikiwa 7 yrs nilishawahi kubakwa kijijini kwa bibi na mfanyakazi ila sijawahi kumwambia mama wala mtu yeyote.

Watu watakua wanajiuliza mbona sitaji baba. Baba yangu ana familia yake mkoani na alishasahau kama ana mtoto. Baba yangu wa kambo yupoyupo tu but sana sana anawajali wanae ila hainiumizi roho. Ninachomuomba Mungu niondoke nipate kazi hata mkoani mbali na mama yangu.

NB. Wazazi wa hivi especially wamama jaribu kuweni karibu na watoto wenu kuweni na upendo. Mimi siwezi elezea kila kitu hapa ila umuhimu wa mamangu ni kunisomesha tu tena kwa maneno namshukuru sana kwa hilo.

Wapendwa sjui mtanisaidiaje but nimevumilia sana ni mama yangu huyo ndo maana wengne hukimbia kwao au kutaka ndoa haraka ili waondoke makwao.

Wazazi badilikeni tafadhali.
Pliz nitafute tuzungumze cuz hapo ulipo unahtaji physicalogical treatment tena kwa haraka sana!
 
Pole sana, ila nawewe jiangalie maisha unayoishi yanampendeza mamako? Isijekuwa anachukia tabia zako hakuchukii wewe
 
Pole mkuu. Kwavile una elimu,natumai soon utaondokana na hayo mateso.

Giza huwa nene panapokaribia kukucha.
 
Kwa hii story yawezekana mama yako anaona unamzeesha. She's 40 na ww uko 22, na akiangalia wenzie watoto wao bado wadogo. Na kibongobongo watu wasio kujua wakiona una Mtoto mkubwa wanadhani na ww ni muhenga. Atakuwa aina ya mama wasiopenda ukubwa, akikua kidogo ataacha
 
kuwa karibu na yule utayemweleza akakuiskia shida zako na anakupa attention kama mama
 
Pepo yako iko chini ya unyayo wa mama ako so jitahid kumtendea wema
 
Poleni sana dear, uwe unaomba sana Mungu kwake hakuna lisilowezekana anaweza hata mbadilisha hata mama ako akawa mzuri. Kuna wezekana mama yako alibakwa na wewe ndio ukapatikana akikuona anazidi kukumbushwa machungu. Kemea sana spirit ya kubakwa coz tayari ushasema na wewe ulibakwa usije Unaenda mpk kwa watoto wako. SAA zingine sisi watoto tunalipa dhambi za baba zetu, unakuta baba nbakaji na watoto wake pia wanabakwa. Ila kwa Yesu yote yawezekana anafuta laana zote
 
Habari zenu wapendwa,

Mimi ni msichana niliyemaliza chuo lakini natafuta kazi. Naishi na wazazi wangu na wadogo zangu wa kike ambao nawapenda sana. Nimekulia na kulelewa na bibi sana na mama mdgo ambao wote walikua wapole na wakarimu ila mama mdogo alitangulia mbele ya haki.

Nilimpenda sana mamdogo kuliko mama yangu mzazi kwasababu alinipenda na kuchukua nafasi ya mzazi wangu na ndiye aliyeniambia mume wake mama siyo baba yangu mzazi ( ila ni baba yao wadogo zangu ) nikiwa darasa la sita.
Niliumia sana kwasababu mama yangu alikuwa hana time kabisa kunieleza hayo. Hapo form one ndo nikaanza kuishi na mama yangu ila jamani ni mkali kwangu adi naliaga. Kuna siku nilimuuliza mama mdgo kama huyu kweli ni mama yangu mzazi au la akasema ndo mamako.

My mum hana ukaribu na mimi, ananifokea kila wakati bila hata sababu. Hanaga shukrani in anything i do. Uzuri darasani nilikua nafanya vzuri sana nikishuka position kidgo atafoka likizo nzima. Nilikua nashika nafasi ya nne nikiwa naongoza wasichana ila nikiwa tu wa tano ataongea likizo nzima.

Anavyokuwa ananiangalia, utafikiri yeye ndo mama yangu wa kambo hata akipiga honi ya gari getini nikiwa tu nje nilikua nakimbilia chooni. Anyway namshukuru kwasababu yeye ndo aliyenisomesha. (japo ni wajibu wake).

Tatizo ni pale mama anavyokuwa hana mother to daughter love au affection. Hajali what I do. Naweza kumuomba hela anakuwa mkali mpaka namwambia basi mama natafuta njia napata na haulizi ila wadogo zangu wanapewa hata extra. Mimi sijawahi kununuliwa simu na mama ila wao wananunuliwa tena mimi ndo namsindikizaga mama kununua na haniulizi mimi napata wapi simu.

Nikitaka tuongee labda angalau nimwambie kitu kinachonisumbua au just kupata faraja ya mama anaongea kwa ukali kwamba kachoka au bwanae ondoka ila roho inaniumaga. Marafiki zangu wanavyoongelea mama zao huwa nawatazama na kuwatamani.

Nyumbani kuna mfanyakazi lakini kazi zote nafanya mimi na mama humtetea dada na kusema mimi sina umuhimu ndani wakati kutwa nzima mimi ndo najishughulisha ila nakaaga kimya hadi nikiwa chuo nikija kusalimia huwa hataki niondoke ili nifanye kazi. Nikimwambia mama nina test atasema bwanae kwani wewe wa kwanza kusoma mpaka nakosa raha nikiwa chuo nakuwaga very lonely na mawazo. Sikufanikiwa kupata mkopo wala hela ya matumizi hvyo nilikua nahudumiwa na mama. Aisee sitokuja kusahau mateso niliyopata chuo.

Nimelala hungry nights mpaka ilibidi nizoee. Hapo ndo nikaona nitakufa nikaanza mahusiano na wanaume kisa nipate hela. Hapo mama uwezo anao wakunisaidia lakini anasema hana hela nitafute wanaume tena kwa ukali.

Anyway nilipunguza ukaribu na mama hata upendo kwasababu nilijaribu kuwa karibu nae nipate mapenzi ya mama lakini nikashindwa. Afu yeye ndo anasema nina roho mbaya, sina upendo kama wadogo zangu. Ninamwangalia tu kwasababu najua yeye ndo hanipendi. Na anasema hivyo kwasababu anawasikiliza sana yuko karibu nao but she pushes me away yaani utafikiri niliokotwa.

Kuna wakati huwa natamani niolewe ila ndoa ina majanga yake pia na sina hata mtu. Na hali ya mama imenifanya nikose upendo kwa watu wengne niponipo tu all alone. Kuna wakati nakaa tu na kulia na kinachoniuma nikiwa 7 yrs nilishawahi kubakwa kijijini kwa bibi na mfanyakazi ila sijawahi kumwambia mama wala mtu yeyote.

Watu watakua wanajiuliza mbona sitaji baba. Baba yangu ana familia yake mkoani na alishasahau kama ana mtoto. Baba yangu wa kambo yupoyupo tu but sana sana anawajali wanae ila hainiumizi roho. Ninachomuomba Mungu niondoke nipate kazi hata mkoani mbali na mama yangu.

NB. Wazazi wa hivi especially wamama jaribu kuweni karibu na watoto wenu kuweni na upendo. Mimi siwezi elezea kila kitu hapa ila umuhimu wa mamangu ni kunisomesha tu tena kwa maneno namshukuru sana kwa hilo.

Wapendwa sjui mtanisaidiaje but nimevumilia sana ni mama yangu huyo ndo maana wengne hukimbia kwao au kutaka ndoa haraka ili waondoke makwao.

Wazazi badilikeni tafadhali.
kwa nini usimmtafute baba yako huenda anakupenda na ashapigwa biti na mama yako asije au alishafichwa na mama yako
 
Back
Top Bottom