You nailed it Mrs ake.
Cha kwanza lady hana budi kumsamehe mama ake Kwa yote. Anapitia na atapitia magumu mengi na mama yake, but hana budi kumsamehe kama anataka aishi kwa amani. Hatujui nini kilitokea, but inawezekana mama yake ni mtu aliyeweka uchungu mkubwa moyoni, unfortunately uchungu huo anaumalizia kwa mtoto. Kuna kitu possibly kinachomuumiza kwenye yale mahusiano na baba mtoto, na hajawahi kukiachilia moyoni mwake wala kumove on. Maumivu yote anayahamishia kwa mtoto, siku akija kuyaachilia utashangaa atakavyoumia na kujuta juu ya yote anayokufanyia. Muombee mama ako, possibly anachokifanya ni out of her control, muombe Mungu aingilie kati.
Inaumiza mnoo, but mchukulie mama ako kama udhaifu wako, kama jaribu lako ambalo huwezi kumtupia mtu mwingine. Muombe Mungu akupe hekima ya kuishi na mama ako, na kila siku muombee mama ako akauachilie huo uchungu
Above all, kemea roho ya kukataliwa, kama alivyosema
mrsleo. Muombe Mungu akupe kibali mbele zake na mbele ya wanadamu. Hutokataliwa tena, hutochukiwa tena, utakubalika popote pale utakapokuwa na utakapoingia. Mungu akutie nguvu na akutetee katika hili