Nimemchoka sana mama yangu

Nimemchoka sana mama yangu

Ingekuwa ni mama wa kambo tungesema anakutesa na ningeungana nawe kuwachukia ila kwa kuwa ni mama Mzazi hapo anakufundisha maisha. Kwa ujumla hilo ni jaribu tu, ipo siku litakuwa ni simulizi inayosisimua. Yupo Mungu Msemaji wa Mwisho
ila mamangu wa kambo yeye anaonesha upendo huwa anasema niende kuwasalimia japo mama hataki hataki niwasiliane nae Wala kwenda huko ila mama na babangu wanaongea tu vzuri.ila mimi nampenda sana mamangu wa kambo ananisikiliza na kunishauri.ananiambia niendelee kumtegemea Mungu na kunipa moyo.japo swez kumlalamikia kuhuc mamangu ila she is fine.tabia zake kama mama mdgo ila siyo mamangu. kunifundsha Maisha sijakataa...ila hana upendo naona kabsa hanipendi
 
Pole sana Mdogo wangu, I see mpaka nimehisi moyo kutikisika! Munguvatakufanyia wepesi utafanikiwa lakini kamwe usimsahau wala kumtenga mama IPO siku hao woote wanaokunyanyapaa watasimama Mbele yako vichwa chini wakihitaji msaada toka kwako,ni muda tu utawadia
 
Pole sana Mdogo wangu, I see mpaka nimehisi moyo kutikisika! Munguvatakufanyia wepesi utafanikiwa lakini kamwe usimsahau wala kumtenga mama IPO siku hao woote wanaokunyanyapaa watasimama Mbele yako vichwa chini wakihitaji msaada toka kwako,ni muda tu utawadia
Asante
 
Endelea kuvumilia huku ukitafuta kazi lakini pia sio mbaya ukajaribu kutafuta mawasiliano na baba yako mzazi huenda akawa msaada wako kwa upande fulani, si rahisi mama kumchukia mwanae kwa namna unavyoelezea lazima kutakuwa na sababu inayohusiana na baba yako mzazi huenda chuki hizo kaziamishia kwako.... be strong and time will tell!
 
pole sana, jitahd utafte kazi uhame nyumban, wazaz wengine wanakera kinyama
 
Huyo ndiyo mama wakweli mjelajela faida yake utakuja iona baadaye kaza buti halafu mama ni mama awe mkali awe mpole wewe wajibu wako ni kumtii
 
Hii habari inanikumbusha mama mmoja nae aliolewa akiwa na mtoto... Alomchukia sana yule mwanae wa nje ya ndoa na kuwathamini sana wandoa kitu kidogo anapigwa kusimangwa nk... In short... Yule wa nje ya ndoa aliolewa kwa heshima zote na ana maisha mazuri sana... Wale wa ndoa walizalishwa ovyo na kubaki majumbani... Kifupi mpende sana mama ako tena mpende kupita kiasi hata ukipata kazi zawadi ya kwanza mpe mama yako... Ipo siku... Ipo siku ipo siku inakuja atakuja tambua umuhimu wako... Nipm unipe no nikupigie kwa ushauri zaidi
 
Habari zenu wapendwa,

Mimi ni msichana niliyemaliza chuo lakini natafuta kazi. Naishi na wazazi wangu na wadogo zangu wa kike ambao nawapenda sana. Nimekulia na kulelewa na bibi sana na mama mdgo ambao wote walikua wapole na wakarimu ila mama mdogo alitangulia mbele ya haki.

Nilimpenda sana mamdogo kuliko mama yangu mzazi kwasababu alinipenda na kuchukua nafasi ya mzazi wangu na ndiye aliyeniambia mume wake mama siyo baba yangu mzazi ( ila ni baba yao wadogo zangu ) nikiwa darasa la sita.
Niliumia sana kwasababu mama yangu alikuwa hana time kabisa kunieleza hayo. Hapo form one ndo nikaanza kuishi na mama yangu ila jamani ni mkali kwangu adi naliaga. Kuna siku nilimuuliza mama mdgo kama huyu kweli ni mama yangu mzazi au la akasema ndo mamako.

My mum hana ukaribu na mimi, ananifokea kila wakati bila hata sababu. Hanaga shukrani in anything i do. Uzuri darasani nilikua nafanya vzuri sana nikishuka position kidgo atafoka likizo nzima. Nilikua nashika nafasi ya nne nikiwa naongoza wasichana ila nikiwa tu wa tano ataongea likizo nzima.

Anavyokuwa ananiangalia, utafikiri yeye ndo mama yangu wa kambo hata akipiga honi ya gari getini nikiwa tu nje nilikua nakimbilia chooni. Anyway namshukuru kwasababu yeye ndo aliyenisomesha. (japo ni wajibu wake).

Tatizo ni pale mama anavyokuwa hana mother to daughter love au affection. Hajali what I do. Naweza kumuomba hela anakuwa mkali mpaka namwambia basi mama natafuta njia napata na haulizi ila wadogo zangu wanapewa hata extra. Mimi sijawahi kununuliwa simu na mama ila wao wananunuliwa tena mimi ndo namsindikizaga mama kununua na haniulizi mimi napata wapi simu.

Nikitaka tuongee labda angalau nimwambie kitu kinachonisumbua au just kupata faraja ya mama anaongea kwa ukali kwamba kachoka au bwanae ondoka ila roho inaniumaga. Marafiki zangu wanavyoongelea mama zao huwa nawatazama na kuwatamani.

Nyumbani kuna mfanyakazi lakini kazi zote nafanya mimi na mama humtetea dada na kusema mimi sina umuhimu ndani wakati kutwa nzima mimi ndo najishughulisha ila nakaaga kimya hadi nikiwa chuo nikija kusalimia huwa hataki niondoke ili nifanye kazi. Nikimwambia mama nina test atasema bwanae kwani wewe wa kwanza kusoma mpaka nakosa raha nikiwa chuo nakuwaga very lonely na mawazo. Sikufanikiwa kupata mkopo wala hela ya matumizi hvyo nilikua nahudumiwa na mama. Aisee sitokuja kusahau mateso niliyopata chuo.

Nimelala hungry nights mpaka ilibidi nizoee. Hapo ndo nikaona nitakufa nikaanza mahusiano na wanaume kisa nipate hela. Hapo mama uwezo anao wakunisaidia lakini anasema hana hela nitafute wanaume tena kwa ukali.

Anyway nilipunguza ukaribu na mama hata upendo kwasababu nilijaribu kuwa karibu nae nipate mapenzi ya mama lakini nikashindwa. Afu yeye ndo anasema nina roho mbaya, sina upendo kama wadogo zangu. Ninamwangalia tu kwasababu najua yeye ndo hanipendi. Na anasema hivyo kwasababu anawasikiliza sana yuko karibu nao but she pushes me away yaani utafikiri niliokotwa.

Kuna wakati huwa natamani niolewe ila ndoa ina majanga yake pia na sina hata mtu. Na hali ya mama imenifanya nikose upendo kwa watu wengne niponipo tu all alone. Kuna wakati nakaa tu na kulia na kinachoniuma nikiwa 7 yrs nilishawahi kubakwa kijijini kwa bibi na mfanyakazi ila sijawahi kumwambia mama wala mtu yeyote.

Watu watakua wanajiuliza mbona sitaji baba. Baba yangu ana familia yake mkoani na alishasahau kama ana mtoto. Baba yangu wa kambo yupoyupo tu but sana sana anawajali wanae ila hainiumizi roho. Ninachomuomba Mungu niondoke nipate kazi hata mkoani mbali na mama yangu.

NB. Wazazi wa hivi especially wamama jaribu kuweni karibu na watoto wenu kuweni na upendo. Mimi siwezi elezea kila kitu hapa ila umuhimu wa mamangu ni kunisomesha tu tena kwa maneno namshukuru sana kwa hilo.

Wapendwa sjui mtanisaidiaje but nimevumilia sana ni mama yangu huyo ndo maana wengne hukimbia kwao au kutaka ndoa haraka ili waondoke makwao.

Wazazi badilikeni tafadhali.
Pole sana aisee, ila nashangaa mzaz unakosaje upendo na mwanao jaman duh! Ucjar mpnz yatakwsha uwe unasal sana mungu atasaidia tu
 
asante.hakuolewa na baba.baba alikua na familia tayari ndo akawa na mahusiano na mama.may be so
Sasa hapa hapa ndo kuna shida...kumbe alikuwa anatembea na Mme wa mtu?....mamaako inaonesha alikuwa kashakata tamaa ya yy kuolewa then akajiweka kwa huyo mme wa mtu lkn hakumpenda, mwanamke akiwa hampendi mwanaume hata mtoto/watoto wake huwa hawapendi, ndicho kilichokukumba Dada. Pole sana na sali sana asee!
 
sikiliza usisononeke haya yoote unayoyapitia yanakuongezea ujasiri jitahidi kuyafanya ni sehemu ya maisha yako ili uyazoee usihangaike na wanaume watakuingiza matatani zaidi ................ polee yataisha haya na utakuwa mwenye furaha tena ila usije kumfanyia mwnao hivyo si unaona uchungu unaoupata?

respect to my moma anatupenda sana kwakweli japo alifiwa na mumewe (baba yetu) akiwa bado mchanga lakini hakuolewa tena nguvu zake alielekeza kwetu


love you mama soo much
 
hilo ni fumbo zito, ebu jiulize kwanini mama yako hakukueleza habari kuhusiana na baba ako? atakae weza kukufumbulia fumbo hilo ni baba ako mzazi pekee...unajua wanawake huwa na akili tofauti kidogo pale anapoumizwa au anapopata ujauzito bila kutegemea....inawezekana mama ako alikupata pasipokutegemea...alijaribu kukutoa ikashindikana ata iweje hawezi/huwezi kuwa na mapenzi naye...inawezekana pia pengine uhusiano wake na baba yako uliathiri sana maisha ya mama yako pengine kutokana na mimba yako...hivyo aliichukia mimba akajikuta anakuchukia na wewe....ishi nae kwa upendo mpende kwa kuwa ndie aliekufanya ukafika hapo ulipo...usimchukie ila mtafute baba ako kipo kikubwa utakipata. ila kwakuwa hakupenda kukufahamisha habari za baba ako jitahidi kufanya jitihada za kumtafuta baba kwa siri iwe siri kubwa sana maana wazazi wa kike mara nyingine hawashindwi kutoa laana mara tuu uoneshapo dalili za kumfuata mzazi wa kiume...nakumbuka mimi mama angu alikuwa ananiambia sifa mbaya za baba angu...ili tu kuniweka mbali naye
 
pole mamy.. ila ukweli ni huu mama yako hana mapenzi na wewe tokea ukiwa tumboni labda baba alisababisha , labda anachukulia wewe ndiyo umemuharibia pamoja na kuwa ni starehe zake..endelea kumpenda na sina maana ujiependekeze kwake no muheshimu mama yako, fanya lile linalokupa faraja unataka nini maishani fanya hilo bila kujaili hakuna maisha marahisi kila jambo lina changamoto ni wewe kuwa tayari kuzikabili.... be positive usimuwaze sana mama yako usiwaze sana past yako.. nakueleza haya from experience maisha ni mind set and risk taking move on one day yes,,
 
Back
Top Bottom