Nimemaliza 'kamshahara' ka October 2019 ndani ya siku 2

Change your attitude, Open your mind & dream Big.

Inaweza kuchukua muda kutimiza ndoto zako, lakini zitatimia, changamoto unazopitia zinakujenga kuwa bora baadae. Tunajifunza mengi tunapopitia maumivu katika maisha yetu ya kila siku.

Mungu anaziona juhudi zako na atakujibu maombi yako kwa wakati sahihi.

Keep fighting, never lose hope boss.
Ubarikiwe una maneno ya kutia faraja sana, be blessed
 
Pole sana...

Kwa kawaida mishahara inatakiwa ikutane...

Yani mwisho wa mwezi ukifikia, mshahara wa mwezi uliyopita bado upo na unaweza kukusogeza siku 15 zaidi, kabla hujaanza kutumia wa mwezi husika...

Cc: mahondaw
 
Salary ni tamu japo ni ndogo...Tunafanya kugawana kasungura kadogo tu kwa ajili ya kuishi.

Mshahara umetoka mchana October 24 , leo hii October 26 hakuna kitu.

'Kamshahara ka serikali' kamekuta madeni kimbwa, ngeu za kutosha dadeki.

Sijui nitatoboaje November 24!!

Kwa kawaida mshahara unatakiwa uishe baada ya siku ngapi wakuu?
Mbona kawaida tu
 
...Ndio maana hii inaitwa Bongo, Mkuu!
Hapo unatakiwa kutumia Bongo kuona utatoboaje hadi 24 November Mkuu!
 
Mimi kinachoniumiza kichwa jamani ntajenga kweli? Si nitakufa mapanga nyumba za watu
Pole sana ndugu ,ukitia nia naamini utajenga japo taratibu, nina miaka minne kazini ili nimejifunza mengi kuhusu suala la kujenga, nimegundua kwanini watumishi wanajengea kiinua mgongo haswa watumishi wa kawaida kama sisi, mshahara mdogo sana, matumiz mengi na wategemezi wengi sana. Kinachotakiwa ni kukubali kujitesa hata ndani ya miaka kadhaa, kukubali kukosa baadhi ya mambo muhimu kama kula mlo kamili, kuvaa nguo nzuri au kujumuika na marafiki kwenye mambo yaletayo furaha. Wakati mwingine unapaswa ukubali kuonekana u mtu wa ajabu ajabu kwa wengine, usiogope kukopa la msingi ukope kwa malengo, ishi wewe kama wewe, kama sehemu waweza kutembea kwa mguu basi usitumie nauli, fanya lolote lile ili punguze matumiz, anza kujenga hata ukiwa na laki moja anza utajikuta umejenga. Zaidi ni kwamba ukianza kujenga utajikuta umeenda mbali bila wewe kujua pesa unaipataje. Mungu azidi kutimiza haja za moyo wako.
 
Bora hata ww unapata hata huo mshahara..

Hapo ni kukopa tena tu!!
Salary ni tamu japo ni ndogo...Tunafanya kugawana kasungura kadogo tu kwa ajili ya kuishi.

Mshahara umetoka mchana October 24 , leo hii October 26 hakuna kitu.

'Kamshahara ka serikali' kamekuta madeni kimbwa, ngeu za kutosha dadeki.

Sijui nitatoboaje November 24!!

Kwa kawaida mshahara unatakiwa uishe baada ya siku ngapi wakuu?
 
Nakumbuka kuna jamaa yangu miaka hiyo tunafanya naye kazi.. Mshahara ukitoka badala ya kufurahi yeye anasikitika!
Yan siku nzima anakuwa na mawazo ya kufa mtu, ni taasisi chache sana na baadhi ya vyeo ndio wanaoneemeka na hizo kazi, tena wengi wao ni rushwa tu ndo zinawaokoa..
 
Back
Top Bottom