Nimeliwa hela zangu kijinga kweli leo

Napoleone

JF-Expert Member
Apr 11, 2012
10,087
15,961
So ni hivi, leo mida flani nikajisogeza mahala flani huku kwetu kwa lengo la ku swim kidogo na kupata ka kinywaji kagumu, actually sija-swim nilikua nawaangalia tu wadada wakiswim.

Basi ikafika mida mazoea na binti mmoja yakawa mazito sana gafla akaongezeka na mwingine wakawa wawili basi unajua watoto wa kike unawakuta na vichupi tuu kwenye maji kama bata huwezi chomoa kwa lolote watalohitaji siwajui hawanijui.

Nikawanunulia chakula, vinywaji, wamemaliza kuswim tukawa pamoja nini story za hapa na pale. Sasa ikawa shida ku choose nani nioneshe interest kwake maana kila mmoja anamvuto wake na kuomba namba imekua tabu namwomba yupi namwacha yupi

Basi mwisho wa siku tumeagana tuu nimeshindwa chukua namba ila promise ni kwamba next weekend watakuepo pale

Now nimekaa sebuleni najikuna tuu huku nikiangalia my fav series workaholics

Msos wa binti mmoja elf16 na vinywaji smirnof ice tatu tatu. Sasa zidisha mara mbili

Enewei

Ishakula kwangu hiyo
 
situation yako naielewa mkuu, ni nadra watu wengi kukuelewa.. sikilizia wknd ijayo, hapo ww unapoint kubwa sana ya kuwala, maana lazims wamestaajabu how come this dude katugharamia na hajashoboka zaid kuchukua namba, they must be feeling you man, na umewaacha wamechanganyikiwa zaidi.

next weeknd watakuepo, ww jichange tu ila this time chukua contacts na alika mmoja geto huo mwaliko hautakataliwa asilani.. ndo ushapata chombo hapo!
 
Ndugu yangu pole sana.
Ilinitokea miaka fulani nikiwa nasaka demu wa kuzugia kisiwani Unguja.
Nikakutana na mabinti warembo watatu Forodhani wapo kwenye kimkeka na keki kubwa ya birthday.
Nilikaa pembeni yao, mmoja akaniomba niwapige picha, mazoea yakaanzia hapo.
Nikaja kugundua ni wanafunzi wa Chuo kikuu Tunguu.
Nikaona niwape ofa ili walau nitanue wigo wa kunizoea ili nimpate mmoja wao.
Nikaanza na juice za miwa glass kubwa tatu (3,000/-)plus chips sahani tatu (4,500) na mishikaki ya kuku miwili kwa kila mmoja (6,000)
Baada ya muda wakasema wana hamu na shawarma-wakati huo ilikuwa 3500 la pack moja (10,500/-). Jumla nilimaliza kama 24,000/-
Kufikia saa tatu usiku kabla sijaomba namba ikaja kirikuu wakaniaga na kuondoka.
Dah, safari ya kutoka Forodhani kwenda Mkunazini nilipokuwa naishi ikawa ndefu sana. Nilihisi kuumia sana moyoni yaani 24,000/- nimeimaliza bila kuambulia chochote.

Baada ya wiki nikiwa Restaurant fulani maeneo ya Malindi pale karibu na benki ya Exim; ghafla nikaitwa Uncle Uncle, kugeuka hivi ni yule binti aliyekuwa na birthday.
Kutokea hapo sikujutia ile 24,000/- maana ilikuwa ndio msingi wa kuniwezesha kula vitu vinono.

Usife moyo baharia, ipo siku utaanza kula faida ila pia hasara inaweza kutokea.

Alamsiki.
 
Jamaa yangu kutoka Forodhani kwenda Mkunazini safari ikawa ndefu kwa ajili ya 24,000/= kweli Azimio la Arusha liliwafundisha kubana matumizi
 
Chakula 16K+ Smirnoff 3(15K,1 per 5K) =21
21 ×2 = 42K
So uko hapo na mapu.mbu yako mawili unalilia elfu 42?

Siku nyingine ukiwa huna hela uwe unabaki nyumbani. Hela za starehe uwa hazisikitikiwi
😕😕😕😕
 
Ili mbegu izae lazima ife kwanza.Kwa hiyo ili siku nyingine ufanikiwe ni lazima utoe kwani mkono utoao ndio upokeao
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom