Nimeletewa IPhone 13 Pro max na rafiki yangu

Nimeletewa IPhone 13 Pro max na rafiki yangu

Hi ni copy yaaani fake...

Bei yake utauza chini ya laki
 
Wakuu mwezi uliopita rafiki yangu alikuja kunisabahi kutoka Marekani - Washington, mbali na vitu vingi ameniletea,ameniletea pia zawadi ya IPhone 13 Pro Max. Kiukweli, mimi sio muumini wa divice za Apple. Nilitaka kujua yafuatayo kutoka kwa wajuzi

Nikiamua kuiuza inaweza pata wanunuzi?

Naweza pata kiasi gani nikiiuza?

Ikiwa kuna yoyote anahitaji aniambie.

Location: Dar Es Salaam.
View attachment 2279122
Google uone inauzwa aje Kwa dollar, halafu badili Kwa pesa za Tanzania. Si chini ya milioni 2
 
Mwandish wa huu uzi nakushauri akili za kuambiwa changanya na ....la sivyo hutaiuza hiyo simu maan humu kuna wengne wanakatisha watu tamaa atar....
Yaani acha tu Mkuu,kuna watu humu wanaanza kunitukana hadi MATUSI sasa sijui wapi nimewakwaza, anyway God knows.
 
Niunganishe nae mkuu nimepelekee hii IPHONE 13 PRO MAX (COPY) FROM USA
no yake hii +255 738 680 955 ukimtumia tu picha ataleta mtazamo wake kama ni copy..kama wengine walivyogundua kupitia tu picha 🤣🤣🤣
 
Sijui kwanini watu wanaoishi ulaya/marekani huwa Ni wakarimu sana
Mazingira huwa yanawabadilisha. Upambanaji plus upatikanaji wa fursa za kujiingizia kipato kwa urahisi inawafanya kuondokana na roho za kibongo za kwann.

Maana akikupa wewe chochote ana uhakika atapata tena mara mbili yake so haina shida.

Kibongo bongo mtu anaweza kuwa na milioni kwenye akiba ukaomba akuazime 20,000 akipiga hesabu namna kaipata ile milioni anaona hapana, hatoweza kuichenji kwaajiri yako wacha tu asikupe kama ni dhambi MUNGU atasamehe.

Umasikini huwa unawafanya watu kuwa na tabia za ajabu sana kama ushirikina, uchoyo, ubinafsi, kubania wengine, kuchukia wengine bila kukosewa lolote, wivu, ghubu, etec.

Ndio maana babu yetu Nyerere alitusihi sana kuwa tuupige vita sana umasikini kwa maana huwa unaleta matatizo mengi sana.
 
Back
Top Bottom