Nimekwisha na UKIMWI

Nina amini sana kuwa huyu akipima atakutwa yupo vizuri sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana kaka. Zingatia ushauri chanya huko juu na uufate.
 
Kitakachokuuwa ni mawazo hayo uliyoyaandika kwenye kichwa cha mada ila sio ukimwi

Tulia kama hujui kinachoendelea vile
 
Nakuombea Mungu kwa yote mema
Mwangalie mwanao na mkeo.
Usitumie madawa yao kama utakuwa nao
Kula vizuri na usiwazie kabisa huo ugonjwa maana ukiuwazia tu ndio unaanza kuwa na msongo wa mawazo na kuiona dunia sio mahali pako.

Ukimwi ni uongo
 
Pole sana
Usikate tamaa hilo ni jaribu la kawaida sana kumbuka kuna mtu umri wako amepata ajali kakatika miguu yote hawezi kutembea na mwingine amepofuka macho umri Kama wako hawezi kuona tena jiangalie je wewe na wao wapi ni bora zaidi usikufuru wala usihuzunike jipe moyo huwezi juwa mipango ya Mungu akakuinua kupitia hilo jaribu
 
mkuu usijifanye kama upo smart sana,haya yamenikuta ila na wewe siku yako inakuja hasa kama una aamini ukiwa kwenye ndoa ndio utakuwa salama,nimekiri makosa yangu,lkn pia kuishi nae miaka 3 nilimaanisha kuwa nae kwenye mahusiano,sikuwa sawa kipindi naandika,nilipanga kuanza kuishi nae baada ya ndoa,naomba usinihukumu hasa kama bado upo hai,lolote nawe laweza kukutokea,tena huwenda likawa baya zaidi ya hili la kwangu,kinachonipa moyo ni kwamba wiki tatu zimepita kuna mdogo wa rafiki yangu nilimtolea damu,na nahisi hadi wakaniruhusu nitoe inamaanisha ilikuwa salama,kesho ndio siku ambayo tajua mbivu na mbichi,nahisi kwa sasa nahitaji faraja zaidi na si kejeri,hii ishu haina mwenyewe,tuombe uzima kesho nitarejesha nitakachotoka nacho maabara...all in all nimefarijika sana kwa wana JF wengi kwa kuwa watu dynamic,mnajua jambo la utani na jambo ambalo ni serious,imenipa moyo sana na narudia kushukuru kwa wote mliooonyeshwa kuguswa na tatizo langu,ki`zaidi mlionifuata PM na kunipa msaada wa mawazo na kila kitu...
 
Usipanic,ukimwi ni ugonjwa kama magonjwa mengine,sikuhizi watu wanaogopa kansa na kisukari na mgonjwa ya INI na mioyo yakutibia India,Pima fuata ushauri utaishi vizuri mno na familia yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hujaisha Mkuu.

Kapime kwanza, kuna probability kubwa tu ya kutembea na mtu aliyeathirika several times na bado ukabaki kuwa salama.

Nimekutana na kesi zaidi ya 5 (uhalisia siyo story ya kutunga) ambapo mke ameathirika lakini mume ni mzima.

Usiwe na hofu Mkuu. Hata ikitokea umeathirika bado una muda mrefu tu wa kuishi hapa duniani. Kuna mtu (namfahamu) ameathirika tangu mwaka 1992 lakini hadi leo ni mzima mwenye siha njema kabisa.

Mungu akupiganie Mkuu, maisha ni mlolongo wa matatizo mengi yenye chembechembe kidogo za furaha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee saidia kuelimisha watu nimependa hii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe nenda kapime ataukipatikana nao wewe hutakuwa wa kwanza,la mhimu kubali hali utakayokutana nayo,kwa wakati huu huna haja yakuogopa dawa zipo ukijikubali na kutumia dawa utadunda tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…