Nimekwisha na UKIMWI

Pole sana mkuu Mungu akutie nguvu sana nenda kapime kwanza ili ujijue kama ni kweli umeathirika au vipi pole sana
 
Kuishi na mwanamke miaka mi3 bila ndoa ni uzinzi,Mungu hapendi uzinzi,ametukataza katika vitabu vyake vyote tunavyoviamaini,ulimkosea mungu wako kwanza muombe msamaha.Huwezi kumuamini mtu bila kupima miaka yooote hiyo,Hapo ulipo najua umechanganyikiwa sana,lakini njia rahisi kuliko zote nikupata majibu ya vipimo vyako mwenyewe,ingawa majibu mimi na wewe tunayahisi ni mabaya tu,lakini heri kuupata ukweli.Kukaza mwanamke aliyeathirika miaka yote hiyo kavu kavu hakujawawahi kumuacha mtu salama.Omba Mungu Amigo,then kapime kwani nini?Kwa imani ya dini maisha yetu yalishapangwa yooote hatubadilishi japo kidogo.MKUU GOODLUCK!
 
Pole sana Mkuu! Sina la kukuambia zaidi ya kukuombea. Pia amini kuwa vyovyote vile majibu yatakavyokuwa, siyo mwisho wa maisha yako. Kuna dawa zinazotumika na wengi na zimeendelea kuwasaidia kuishi maisha ya kawaida. Ninajua umefadhaika sana lakini Mungu Ataendelea kukuongoza katika hili. Poleni sana wote, wewe, mchumba wako na huyo Malaika mliyempata!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
UKIMWI sio issue kabisa siku hizi mkuu.
We kapime ukiambiwa unao endelea n maisha kama kawa kula vizuri pumzika vizuri na mazoezi kwa mbali.

Kwani kwa hiyo miaka 3 umeona tofauti yoyote katika mwili wako?
Saa nyingine UKIMWI ni suala la kisaikolojia tu.

Watu wenye 'strong mind' hawababaishwi nao kabisa.
 
Hospital moja tu inatosha .. Somo ni kwamba msifanye mapenzi kabla ya ndoa... Ukitaka kuoa mkapime
 
Ukimwi kama Malaria mkuu usiwe na shaka kabisa.Unaweza ukawa umesalimika.
 
Nini wasiwasi, watu wamegundulika na ukimwi tangu 1997 hadi leo wanadunda wanakula maisha kama sio wao, wewe hujapima pressure juu, kapime ukikutwa nao anza doze hakuna tatizo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mke wangu ni MUATHIRIKA na kibaya ni kwamba alizaliwa nao.

Nimemuuliza kwanini hakuwahi kuniambia tangu mwanzoni, anasema na yeye alikuwa hajui

alizaliwa nao alafu hakufahamu kama anao🙁 Inawezekana kweli? na nani amemwambia amezaliwa nao? hajawahi kuugua kabla ya hapo?, na wakati akihudhuria clinic hakupimwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…