LUBEDE
JF-Expert Member
- May 7, 2013
- 4,322
- 6,694
Naandika huku hali yangu ya akili ikiwa mbaya sana, mchumba wangu niliyeishi nae kwa miaka mi 3 amejifungua jana kwa upasuaji, na mwezi November mwaka huu ilikuwa tufunge ndoa.
Ndugu jamaa na marafiki wote tushawatangazia na vikao viwili vya ndugu kujiweka sawa vishafanyika, nimeenda leo asubuhi nimekutana na habari tofauti kuwa mke wangu ni MUATHIRIKA na kibaya ni kwamba alizaliwa nao.
Nimemuuliza kwanini hakuwahi kuniambia tangu mwanzoni, anasema na yeye alikuwa hajui, kesho na mimi nataka nikapime kama hospital 5 hivi ili nijue hali yangu, mwenye lolote la busara naomba anishauri na kunipa moyo, hivi inawezekana majibu ya kesho yakaniacha salama kweli?
Kubwa nawakumbusha wote kamwe usirudie kosa nililofanya mimi la kumwamini huyu mwanamke, tayari nimeshafanya kosa naomba nisilaumiwe.
Nishaurini vizuri nifanyaje kwa sasa, bado sijamwambia ndugu wala rafiki yeyote juu ya hili, nasubiri nipime kwanza ili nijue hatima yangu, nikipima nitareta mrejesho kwa litakalokuwa nimelipata huko.
Ahsanteni