Nimekuwa Kituko Ofisini....

Nishakufahamu kumbe tunafanya kazi pamoja. Natamani niku-itroduce kwa JF members lakini naheshimu sheria za Jamii Forums sitaki kupigwa BAN.
 
Juzi baada ya saa za kazi, nikiwa naondoka ofisini nilikuta akina dada wa hapa ofisini getini wakinunua machungwa. Nikamuomba dada mmoja kwa kumwambia naomba "Tukatiane" chungwa aliloshika mkononi. Ajabu watu waliosikia waliangua kicheko. Sasa imekuwa kero kila mtu anayeniona ktk korido za ofisi hasa wasichana salamu zao huwa "Tukatiane", hata nikiwa mbali mijitu inapaza sauti "TUKATIANE"

Kwa mawazo yako wewe unadhani ni kipi walichokidhani ambacho kiko tofauti na ulivyodhamiria ?
 
ok mkuu!kwa hiyo midume yote akiwemo erickb52 wanataka wakatiane na yule dada,na wadada wote akiwemo cheusimangala wanataka wakatiane na wewe?kinachokushinda nini sasa mtoto wa kiume?si uwajibike!kawanunulie tenga zima la machungwa tandale mkatiane mkuu!

ngoja niwajibike kwa kununua tenga zima tukatiane, huenda huu utani utaisha....!
 
Nishakufahamu kumbe tunafanya kazi pamoja. Natamani niku-itroduce kwa JF members lakini naheshimu sheria za Jamii Forums sitaki kupigwa BAN.

Bora umeliona hilo mapema maana PAW na wenzake wako macho..
 
Kuna siku naongea kwenye serious meeting, ofisi ngeni hata siwaju. Nikasema neno 'unakaza hapa', nilijuuta! Mi sipendi kiswahili kwa hili tu!
 
ha ha haaah!! Kiswahili bwana, kinachanganya kweli...
 
Juzi baada ya saa za kazi, nikiwa naondoka ofisini nilikuta akina dada wa hapa ofisini getini wakinunua machungwa. Nikamuomba dada mmoja kwa kumwambia naomba "Tukatiane" chungwa aliloshika mkononi. Ajabu watu waliosikia waliangua kicheko. Sasa imekuwa kero kila mtu anayeniona ktk korido za ofisi hasa wasichana salamu zao huwa "Tukatiane", hata nikiwa mbali mijitu inapaza sauti "TUKATIANE"

Ha ha haaaa!!! Hii ni fedheha kweli kweli.
 
Kuna siku naongea kwenye serious meeting, ofisi ngeni hata siwaju. Nikasema neno 'unakaza hapa', nilijuuta! Mi sipendi kiswahili kwa hili tu!

Mbona hata hapa JF hayo yapo?

Mmesahau ule uzi wa yule jamaa aliyeandika.... " Leo nimenusurika kuliwa kwenye tiGO pesa...."

Ile thread kwa dakika kumi page ya kwanza ilijaa! Sasa uliza hizo komenti zao.. "badili heading","nimekuja mbiombio nikidhani...", yaani siku ile nilishangaa sana!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom