Nimekuta 74,549,940.36 kwenye account yangu

Chukua zote hamisha kwenye ac ya Rafiki au ndugu unayemwamini...likija sanuka kesi haitazidi miaka 2,au kufagia mwananyamala hospital..baada ya hapo..unarudi kitaa maisha safi..Ila usirogwe kurudisha..hao wamejichanganya....MTU anaogopa kutumbuliwa umeingiziwa..'Hainaga ushemela tunakulaga'
 
Ni kosa tu la kiufundi.

Benki wakirekebisha wataliona.

Pesa si yako hivyo tumia hiyohiyo 735000 ambayo ndiyo yako.

Ile sheria ya benki kwa Tanzania inasemaje kuhusu hili kosa?

Je benki wana ruhusa kutoa hiyo fedha kutoka kwenye akaunti ya jamaa bila kwanza kumjulisha kosa walilofanya wao benki?

Nawaomba wataalam wa benki watusaidie hapa.

Ila ningekuwa ni mimi tayari nimeshariana na wakili wangu.
 
Kumbe ni wewe uliyepotea na hela yangu? Nilishangaa sana kukuta akaunti yangu haina kitu wakati siku kama mbili hivi niliweka 74,600,000/= Nakuomba mkuu uende benki haraka sana ukarudishe hiyo hela!
 
Hakuna kitu kama icho una kiasi hicho benk unakumbuka kuweka hadi madoido ya rangi kwenye uzi.!.....mashaka mashakani
 
ripot bank usije fungwa bure huko mbelen

lakin hii stori tamu
umenikumbusha enzi zile za utoto nilitamani sana ndege ya WORLD BANK ianguke nje ya nyumba yetu
umeua mkuu! ndoto hufanana, niliwahi kuota nimeokota kikapu kimejaa noti ile nagutuka asubuhi sikuamini hadi nilizama uvunguni kukitafuta. kumbe hisia za sadaka kanisani. acha buana ndoto zinatesa kisaikolojia
 
Sasahivi atalia mtu kama mbuzi, hivi JF sikuhizi naona matapeli wanaongezeka..ulisikia wapi mtu anaingiziwa hela zote hizo aje hapa atangaze kirahisi hivyo. Hapa pana watu wengi ikiwemo wa wa crdb haina tofauti na kwenda benki na kuwa uliza, hii ni series, episode ya kwanza!! ..sasa mchekeeni muone mtu asipolia kama mbuzi hapa meeeeeeeeeeee...
 
Watoto wa Kishua ndo mnaomba ushauri wa kijinga humu. Ndege kajileta mwenyewe bandani kwanini usimtafune ? million 70's zingeingia kwangu Leo kesho ningekuwa Ruhaa Mbuyuni na Mang'ola kufanya yangu.
 
Ahsante sana ndugu,nimepata ufumbuzi tayari,Tulikuwa tunapata sana tabu kazini tellers wote,ngoja wiki ijayo nikareport.....Thanks very much brother,ubarikiwe sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…