Nimekumbuka Uchaguzi Mkuu mwaka 2015

Ironbutterfly

JF-Expert Member
Feb 5, 2023
3,044
8,165
Habari za jumapili wana ukumbi.

Katika kumalizia mapumziko ya mwisho wa juma,nimekaa sebulen kwangu,nikakumbuka uchaguzi wa mwaka 2015.

Mchakato ulianza na kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura,enzi hizo naishi mbezi Luis, nakumbuka nilikuwa na ujauzito wa miezi kadhaa, kulikuwa na foleni ndefu Sana pale kituoni mbezi shuleni, kwani watu walikuwa wamehamasika sana. Dada mmoja mwandikaji anakiona akaniita, akanisajili haraka nikachukua na namba yake, nikamwachia na hela ya soda.

Kwakuwa watu walikuwa nyomi na wengi hasa watumishi,walikuwa wanaona kero, hasa wanaume kwenda kujiandikisha, basi nilipopata kitambulisho changu,nikaenda nacho ofisini, nikawaonyesha co-workers,wengi wakavutiwa na uharaka wa huduma niliyopata, wakaniomba niwakonekti na yule madam, basi nikampatia yule madamu lile dil manake alikuwa anachaji elfu kumi kwa kichwa.Akawasajil karibia wote ofisini kwetu,tulikuwa idara kubwa yenye watumishi 26.

Baada ya hapo ikafika siku yakupiga kura,kituo kikiwa palepale, mbezi shuleni,nikafika na kupewa kipaumbele manake tumbo lilishakuwa kubwa, kwenye miezi saba huko, Nikamchagua mnyika nakumbuka, alikuwa anapambana na fenela Mkangala na presidaa nikampa mzee lowasa.

Ni mwaka wangu wa kwanza kupiga kura toka nimezaliwa, kumchagua mbunge na Raisi wa nchi, tena nikiwa na ujauzito wa mwanangu wa kwanza, nilishiriki kikamilifu pasipo kujali hali niliyokuwa nayo.

Fast forward 2020, nikiwa nishahama kituo cha kazi, uchaguzi wa 2020,niliko sikuweza kushiriki kupiga kura kwani hakikuwa kituo nilikojiandikisha, Ila ajabu Sasa,zilikusanywa namba za watumishi ambao tulikuwa tumejiandikisha vituo tofauti na wilaya nilipo pamoja na majina yetu, walikopeleka wanajua wenyewe🤔Ila Nina hakika nilipiga kura mbezi daslam ilhali nilikuwa nimehamishia makazi mkoa x🤣🤣maajabu ya Rajabu.🙏

Nimekumbuka tu experience hii niliyopitia miaka 8 iliyopita,nikiwa naadhimisha miaka 8 ya kuzaliwa my first son🙏 Happy birthday son 😍😋 more life to you babe.
 
Uchaguzi wa 2015 uliingiza majuto makuu Kwa watanzania wengi, ulibadili kabisa aina ya siasa Za tanzania baada ya dikteta mwendazake kuingia.
2020 huwa sihesabii Km kulikuwa na uchaguzi zaidi ya uchafuzi tu
 
Hata mimi mwaka 2015 ulikua ni mwaka wangu wa kwanza na wa mwisho kupiga kura katika Jamuhuri ya Tanzania, nilikipigia chama changu cha CCM ngazi zote, nilijua tu ushindi lazima

Happy Birthday to your Son, Mungu ampe kila hitaji la Moyo wake
 
Nilikuwa kijijini. Nilienda kupiga kura nikakuta hata watu wanaojua kusoma na kuandika walijidai hawajui ili wapigiwe kura kuhakikisha ushindi kwa ccm na hii ni baada ya kupokea 10
 
Hata mimi mwaka 2015 ulikua ni mwaka wangu wa kwanza na wa mwisho kupiga kura katika Jamuhuri ya Tanzania, nilikipigia chama changu cha CCM ngazi zote, nilijua tu ushindi lazima

Happy Birthday to your Son, Mungu ampe kila hitaji la Moyo wake
Amina 🙏 napokea kwa niaba yake,he is such a handsome and brilliant boy,Mungu alinibariki kupitia huyu kijana wangu.
 
Habari za jumapili wana ukumbi.

Katika kumalizia mapumziko ya mwisho wa juma,nimekaa sebulen kwangu,nikakumbuka uchaguzi wa mwaka 2015.

Mchakato ulianza na kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura,enzi hizo naishi mbezi Luis, nakumbuka nilikuwa na ujauzito wa miezi kadhaa, kulikuwa na foleni ndefu Sana pale kituoni mbezi shuleni, kwani watu walikuwa wamehamasika sana. Dada mmoja mwandikaji anakiona akaniita, akanisajili haraka nikachukua na namba yake, nikamwachia na hela ya soda.

Kwakuwa watu walikuwa nyomi na wengi hasa watumishi,walikuwa wanaona kero, hasa wanaume kwenda kujiandikisha, basi nilipopata kitambulisho changu,nikaenda nacho ofisini, nikawaonyesha co-workers,wengi wakavutiwa na uharaka wa huduma niliyopata, wakaniomba niwakonekti na yule madam, basi nikampatia yule madamu lile dil manake alikuwa anachaji elfu kumi kwa kichwa.Akawasajil karibia wote ofisini kwetu,tulikuwa idara kubwa yenye watumishi 26.

Baada ya hapo ikafika siku yakupiga kura,kituo kikiwa palepale, mbezi shuleni,nikafika na kupewa kipaumbele manake tumbo lilishakuwa kubwa, kwenye miezi saba huko, Nikamchagua mnyika nakumbuka, alikuwa anapambana na fenela Mkangala na presidaa nikampa mzee lowasa.

Ni mwaka wangu wa kwanza kupiga kura toka nimezaliwa, kumchagua mbunge na Raisi wa nchi, tena nikiwa na ujauzito wa mwanangu wa kwanza, nilishiriki kikamilifu pasipo kujali hali niliyokuwa nayo.

Fast forward 2020, nikiwa nishahama kituo cha kazi, uchaguzi wa 2020,niliko sikuweza kushiriki kupiga kura kwani hakikuwa kituo nilikojiandikisha, Ila ajabu Sasa,zilikusanywa namba za watumishi ambao tulikuwa tumejiandikisha vituo tofauti na wilaya nilipo pamoja na majina yetu, walikopeleka wanajua wenyewe🤔Ila Nina hakika nilipiga kura mbezi daslam ilhali nilikuwa nimehamishia makazi mkoa x🤣🤣maajabu ya Rajabu.🙏

Nimekumbuka tu experience hii niliyopitia miaka 8 iliyopita,nikiwa naadhimisha miaka 8 ya kuzaliwa my first son🙏 Happy birthday son 😍😋 more life to you babe.
Nampa pole mwanao 🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom