Nimekataliwa ukweni kisa kabila langu

Nimekataliwa ukweni kisa kabila langu

Nina chuki na nani?

Nina chuki na mapumbavu kama haya,yanayoacha wanawake wazuri kabisa wa nyumbani kwao,linaenda kujipendekeza kuoa mahali hata hawataki ona kivuli chake

I'm really angry with these kind of fools!

Hisia potofu?

Hisia potofu ndio nyie mnazo..Hisia za hovyo mno....

Wewe unadhani Wajita wote wakioa wanawake wengine kama huyu mwehu kutakua na kitu kinaitwa "wajita" on this earth?

Charity begins at home,na ufanye kwa vitendo,sio mnatuletea upumbavu hapa nakimbia majukumu ya jamii zenu zilizowalea na kuwapa all this wealth!

Potofu ni nyie vilaza,hamuoni shida za jamii zenu mnaona za wengine kwanza...Bunch of clowns!

😂😂 tunasocialize
 
Watu wote waki-socialize kama hivi Wajita wote wangefutika....

Atleast huko unakoenda upendwe na uhitajike basi,cha ajabu wao hawataki kumuona huyu mtu!

Kabila nyingi zishakuwa museto.
Familia chache zinaulizia kabila la mtu fulani.
 
Hahaha,mnaona sasa baadhi ya tabia mbovumbovu za makabila yenu zinavyo waharibia.Inaonekana wazazi wameenda mbali zaidi miaka kadhaa mbele na wakaona pia kuna uwezekano ukaja wapeleka wajukuu zao musoma wakakeketwe.
 
Jimilikishie kinyemela mzae watoto ingalao wawili then warudie tena na vijukuu uone kama watatia neno.
 
Tukushauri halafu baadaye uende kumpiga panga mtoto wa watu.

Ila wajita siyo katili sana kama wakurya eti? Kuna mkurya mmoja alioaga sista angu aisee,kila mara ukienda kwa sista utakuta ana kama kuvimba vimba hiv usoni na vimakovu vya hapa na pale.kwa kuwa wazazi walimkatalia asiolewe huko akawa anawaficha kinachoendelea baadaye akaweka wazi,mbwa alikuwa anamtembezea kipigo hatari
Aisee nimeshuhudia katika makuzi yangu, tukikuwa tunakaa na mzee mmoja kama Chacha Marwa, alikuwa anamfurumusha mke wake anamkimbiza akiwa na Gobore distance ndefu mama akiwa mtupu na hapo amepokonyoka kwenye mikono alipokuwa akila makofi na mitama.

Kuna usiku mmoja kilisikika kilio kikubwa baadae kikawa kinaslow down kumbe mama wa watu alikuwa ndo anakata pumzi.

Hata hivyo naona wengi now wanastaraabika kiaina!!!
 
Maana yangu ni kwamba ungekuwa na hela mwanamke asingekuletea hivyo vijisababu
Nitafute hela halafu. Wachumi wanatwambia pesa haijawahi kutosha, kwa hiyo hela natafuta na mambo mengine yanaendelea
 
Hakuna kitu kinaitwa mseto,ni jamii kubwa na stronger zaidi inameza jamii ndogo na weaker...

Wewe unapoona jamii yako inamezwa na jamii kubwa zaidi halafu unakaa unakenua meno inaonesha you even do not know who you are kabisa!

Ni ajabu sana mtu unaacha jamii uliyotoka inapata shida ya kuolewa halafu unaenda kutoa offer ya kuoa jamii ingine unaacha kwenu?

Ni ajabu,that can never register into my head,wewe kwako ni sawa which is okay!

Hizo habar za jamii weak/ strong/inferior/superior hazina mantiki kwa usitawi wa jamii ya leo.

Upo nyuma ya karne katoto😂😂
Zilikuwa ni nyakati za agano la kale
 
Maana yangu ni kwamba ungekuwa na hela mwanamke asingekuletea hivyo vijisababu
Lkn hivo visababu sijaletewa na mwanamke bali ndugu zake. Mwanamke wangu sio tu namhudumia bali anajua mimi ni mpambanaji
 
Mzee,acha unafiki basi

Kuna jamii zilizoendelea zaidi ya jamii zingine,kweli au uongo?

Ukibisha hili wewe utakua sio mkweli!

Jamii strong kitamaduni na kiuchumi humeza jamii weak!

Hiyo ni FACT!

Eti jamii ya leo,jamii ya leo ipi?Tanzania ni muunganiko wa jamii zaidi ya 300!

Tanzania hakuna jamii/kabila moja tu!


Eti agano la kale

Kuacha wanawake wa kwenu hawaolewi unaenda kuoa kwenye jamii nyingine iliyoendelea ndio agano jipya?

Mostly watu hua mnapenda kukimbilia jamii bora zilizowazidi kujipendekeza kuoa huko..

Mnachukia jamii mlizotoka sababu vichwani mwenu mnadhani kujiunga na jamii kubwa kutawapa uhalali wa kusikia na nyie ni bora...

Huu ndio mwanzo wa kujichukia nyie binafsi na kukimbilia jamii ambazo hata haziwataki kama huyu kichaa humu alifukuzwa getini kwa watu!
Maneno mengi ya nini mkuu!

sahivi uwezi kujinasibu kwa kabila hasa linapo kuja jambo la mahusiano ya mtu na mtu. over

Ndio, unahoja ya msingi lakini ishapitwa na wakati( dunia ya sahivi hatuzungumziu habari za makabila)
 
Aisee nimeshuhudia katika makuzi yangu, tukikuwa tunakaa na mzee mmoja kama Chacha Marwa, alikuwa anamfurumusha mke wake anamkimbiza akiwa na Gobore distance ndefu mama akiwa mtupu na hapo amepokonyoka kwenye mikono alipokuwa akila makofi na mitama.
Kuna usiku mmoja kilisikika kilio kikubwa baadae kikawa kinaslow down kumbe mama wa watu alikuwa ndo anakata pumzi.
Hata hivyo naona wengi now wanastaraabika kiaina!!!
Ni asimilia ndogo sana inayofanya hayo, wengi wamestaarabika.
 
😂 wanaolewa na wanao wapenda..kwani lazima kuoana
We kijana umekulia wapi?
Tangu unafika hapo hujaona wanandoa kabila tofati.
Huyo jamaa mpuuze tu, anaonekana ana shida kichwani. Anaandika vitu utadhani kakatwa kichwa.
 
Hi kitu imeniuma sana wakuu, sikutegemea Karne hi bado kuna ubaguzi wa aina hii.

Iko hivi, nimempata binti wa kibena tumependana na tukakubaliana tuoane, kimbembe ni pale alipowapa taarifa nyumbani kwao kuwa kapata mchumba mjita wa Musoma.

Walivyosikia tu Musoma wakaitisha kikao Cha familia na kukataa katakata kuwa binti yao hawezi olewa Musoma. Sababu zao ni
1. Musoma ni mbali na kwao(Njombe). Ikumbukwe mimi na binti wore tunaishi Dar es Salaam
2. Watu wa Musoma ni wakatili sana

Wakuu, kusema kweli kutoka moyoni mwangu nampenda sana huyu binti, sijui nitumie njia gani kupindua meza maana kwa Hali ilivyo yeye binafsi ni Kama anaelekea kuwatii ndugu zake (Yuko dilemma)

Naombeni mnishauri, nifanyeje au nitumie njia gani ili kuweza kumuoa huyu binti.

Ahsanteni.
Ww ilitakiwa ukitambulishe mwenyewe. Tena unajitambulisha ukiwa umejaza mazawadi kibao. Kumbula mikono mitupu hailambwi
 
Nani kakwambia ujinasibu kwa kabila?

Nani kakwambia ni kosa kupenda familia yako kwanza?

Wajibu wako hapa duniani ni kupenda nyumbani kwako kwanza then uangalie wengine

Kabila ni jamii ya watu,cha ajabu umepewa sumu uone neno kabila kama ni kosa kuwepo...

Haiwezi kua kosa jamii ya watu kuwepo hapa duniani,wewe umefundishwa uchukie jamii yako as if wewe kuzaliwa kwenye hiyo jamii ni dhambi

Wewe kua na jamii yako sio kwamba eti utabagua jamii ingine

Na wewe kujifanya kuichukia jamii yako kwa kuipenda ingine pia ni ubaguzi kwenye negative direction..

Kwa kifupi wewe na mimi hatuna tofauti

Wewe unachukia jamii yako maana yake unaibagua na mimi naichukia jamii ingine maana yake naibagua

Wewe na mimi tupo pamoja,hakuna la maana unalofanya kunizidi maana wewe unabagua watu wako unakotoka mimi nafanya kinyume chake!

Wewe ni mbaguzi sana tena sio mbaguzi tu umeenda mbali hadi kuwa na chuki zaidi.

Huwezi kuzuia upendo wa tu wawili waliopendana kwa kigezo cha ukabila.
Unachaotakiwa kujua hamna kabila bora kuliko lingine.

Jamii ya watu walio na mtizamo chanya tutakupinga na tutakuona mtu wa ovyo kabisa tena waajabu sana.

Kosa ni pale na pale tu mtu analazimishwa kuolewa / kuoa kwa kigezo cha kabila, dini, kanda n.k

Ifikie mahali ukubali ukweli.
sahivi kila kitu kimekuwa mseto
Hakuna jamii pure zote zimekanganyana kwa sababu za kidini, kielimu, kiuchumi . N.k
Mkuu ndoa waachie wenyewe wewe kama mzazi hutakiwi kuvunja mahusiano au ndoa za wapendwa wako kwa ideologie zisizo na maaana.

Naomba kuishia hapo kama utakuwa mwelewa its ok. Otherwise endelea na misimamo yako ya kikabila ukitoka huko utaingia kidini.
 
Mimi nimezaa na mbena hatari Sana mpaka Sasa wazazi hawajanitafuta na mtoto ana miaka miwili sasahivi
 
Nyie wakurya mna roho mbaya sana...ni wakatili sana...badilikeni aiseee
 
Binti amekua biashara tayari?

Binti amekua commodity yupo kwenye market place?

Tusha-objectify woman to a commodity to be bought and re-sold around!

Aiseee
Mila za africa sio sawa na za wazungu nk. Mfano USA sheria ya nchi hairuhusu kabisa poligamy, lakini tz inaruhusu. Hata mambo ya mahari etc, USA au Europe HAYAPO. Kama uliamua kuoa mbena, manake na mila zake pia inabidi uzikubali. Kama ulijua lazima ukoo ukukubalie ilibidi utafute njia za kupambana ukubalike. Sasa ulishafanya makosa, mchumba umekataliwa, na yeye pia anaona familia ni muhimu kuliko ww sababu ya mila zake na ANAKUKATAA MAMOJA. Na bado unaona umeonewa. Kama unataka modern woman asiyefuata traditions kama hizo, ungemtafuta huyo. Hii ni kukujibu ww na pia aliyeleta mada
 
Back
Top Bottom