Nimekataliwa kisa ni mwanachuo

The Garang

JF-Expert Member
Jan 16, 2018
2,333
4,152
Habarini za jioni wana jamvi.

Kuna binti tumefahamiana miaka miwili iliopita, ni dada ambae tunakaa sehemu moja.
Aliniomba urafiki kwa kuwa alikuwa ananijuaa lakini mie sikuwa namjuaa kwakuwa kwao ni geti kali kidogo na ni mtu wa kushinda dukani.

Maisha yakaendelea baada ya kumkubalia ombi lake, tukafahamiana vizuri , stories za maisha na kujuliana hali zikaendeleaa.

Kwa kipindi hicho chote sikuwahi kumtamkiaa kuwa nampenda na ofcoz sikuwa namhitaji japo ye anasema ni sealed , hii alinambia katika piga piga story kama unavojua jinsia mbili mkikutana mkashibana basi story kama hizi hazikosi.

Inshort dogo anavosema hana mtu anae date nae na kweli ukiangalia routines zake, ni mtu wa dukani, kanisani na home tu.

Siku za hivi karibuni nimekuwa nikimgusia kuhusu suala la mahusiano lakini ameonekana anapinga na sababu kuu anayoniambiaa nikuwa siwezi oana na msomi mie , nyie wasomi mnadharau na mbaya zaidi kanambiaa sikupendi though tulikuwa tunaongeaa katika joking. LAKINI point yake kubwa hawezi oana na mwanachuo kwasababu.
1.ni waongo sana.
2.wanajidai sana, kwaio bora atafutee ambae hajasoma mwenzake
Elimu yake ni std 7 but anaakili sana za maisha na business.

Nyingine pia, jana hiyo , kuna dada namfahamu anafanya kazi sehemu fulani ni form 4 graduate wa 2018 ,nikamgusia habari za mchumba wake akasema ye hana , nkamuuliza vipi nikutafutiee huku chuoni akanambiaa HAPANA wanachuo ni waongo na hatuna time na watu tuliowaacha mtaaani.

Vilpi ndugu yangu, ushawai kataliwa au kataa mtu kwakuwa ye ni msomi au mwanachuo ??? Kama ndio ulipewa au ulitoa kisingizio gani.
 
Huyo mwanamke aliyekukataaa yupo sahihi kabisa kwa zifuatazo

Kwanza:kiakili bado anakuona haujakomaa kujenga familia

Pili:Huna uwezo wa kumuhudumia kwa kuwa hela zako unategemea boom au upige mizinga kwa wazee

Ushauli wangu dogo komaa na shule tafuta pesa jipange kimaisha weka mipango sawa ukizingatia hayo hakuna mwanamke atakayekutaa
 
Huyo mwanamke aliyekukataaa yupo sahihi kabisa kwa zifuatazo

Kwanza:kiakili bado anakuona haujakomaa kujenga familia

Pili:Huna uwezo wa kumuhudumia kwa kuwa hela zako unategemea boom au upige mizinga kwa wazee

Ushauli wangu dogo komaa na shule tafuta pesa jipange kimaisha weka mipango sawa ukizingatia hayo hakuna mwanamke atakayekutaa
Asante kaka, ushauri mzuri wenye kuuma LAKINI yeye anachosemea hata baada ya kumaliza masomo still hawezi olewa na mwanamme mwanachuo au msomi, sio tu kwangu lakini atayeyote atae kuja kama ni mwanachuo kwake hamfai
 
Ndio mnakutana sasa chupa na mfuniko, make nanyie vibrazamen vya chuo huwa mnajikuta sana, ukishanunua sabufa ya kichina shingshong, ukanunua na pazia, na jagi la tokyo unajiona maisha umeyapatiiiiia......
saiv hatutumii mapaziaa ndugu, afu kati ya vyote ulivosema sina hata kimojaa vyote nagongeaa tu kwa wadau.

Anyway naiikuna napofikia, wa chuo ninayee ila ukorean mwingi usitoke tu kwenda mjini anataka zawadi, lqkini yeye hataa hatoii
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom