Aisee kwanza hongera na pole sana kwa mapito hayo.
Kwenye njia ya mafanikio kuna vikwazo vingi mno na vya kukatisha tamaa.
Kilimo ni fursa nzuri ila usiombe yatokee majanga, Mimi binafsi kilimo kiliacha nipatwe na ugonjwa wa moyo, niliacha kazi, niliitwa tapeli, nilipoteza ndugu na marafiki wote, niliacha masomo ya juu wakati nimelipa hela zote, niliuza kila asset yangu mpaka mashamba yenyewe na vifaa vyake na sikupata ahueni hata robo, yaani matatizo yalizidi mpaka nikawa nalala njiani. Watoto wangu wote waliacha shule hata nisijue naanzia wapi.
Ushauri wangu usijaribu kukopa tena au kutumia asset zako zote kwenye kilimo ambacho bado hujajua soko lake au ustawi wake utakuwaje huko shambani hasa kilimo kinachotegemea mvua.
Kama utapata kazi weka nusu ya hela kwenye hiyo ndoto yako huenda sera zetu za kilimo cha biashara zitakuwa nzuri baadae.
Mwisho kabisa usikate tamaa, omba Mungu sana, na yamekukuta ukiwa bado huna familia kubwa na umeweza kukwepa madeni mengi.