Nimejifunza kitu ukimya ni hekima na silaha ya kumjibu mjinga

NostradamusEstrademe

JF-Expert Member
Jul 1, 2017
3,032
4,028

Haya hapa mambo 10 yaliyozingatiwa mkataba wa bandari Dar​

Mama nilishakuambiaga piga kazi usisikilize kelele za makondakta wanakulazimisha gari la kupanda wakati umekata ticket na basi lako unalijua. Au Kelele za chura zisikutishe wewe kunywa maji mungu akujalie hekima zaidi ya ulizonazo.Watu wanaleta mfumo dume hasa watu wa kanda flani ambao kwa asili mwanamke wanaona sio kitu kukukandia vile mwanamke ila tu nikuambie kitu dada yangu kila zama na kitabu chake ila kiukweli toka tupate uhuru hatujapata raisi mwenye hekima,mstahimilivu kama wewe ila yuko mzee mmoja namuhifadhi umeshamjua, sasa someni habari chini

. Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Plasduce Mbossa amebainisha mambo kumi muhimu yanayohusu mkataba wa uwekezaji na uendelezaji baina ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya DP World ya Dubai.

Mbossa amebainisha hayo jana Jumapili, Oktoba 22, 2023, Ikulu ya Chamwino, mkoani Dodoma, wakati mikataba mitatu mitatu ya uwekezaji na uendelezaji wa Bandari ya Dar es Salaam iliposainiwa mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Mbossa amesema, mikataba hiyo imezingatia vitu vingi ndani yake kwa maslahi mapana ya nchi. Ametaja mambo hayo kumi ni:

(i) Mikataba kuhusisha baadhi ya magati ya Bandari ya Dar es Salaam na sio maeneo yote ya Bandari ya Dar es Salaam na mikataba hii haihusishi bandari nyingine za mwambao na maziwa;

(ii) Mkataba huu una ukomo wa miaka 30 na utakuwa ukirejewa kila baada ya miaka 5 ikiwa ni pamoja na kurejea mpango wa uwekezaji;

(iii) Kutakuwa na kampuni ya uendeshaji ambayo TPA itamiliki hisa;

(iv) Kuwekwa kwa viwango vya utendaji (key performance indicators) ambazo mwekezaji anapaswa kuvifikia;

(v) Watumishi wa sasa wa TPA wamepewa nafasi ya kuchagua kubaki TPA au kuhamia kwa mwekezaji;

(vi) Jukumu la ulinzi na usalama katika eneo lote la bandari na yaliyokodishwa kwa Kampuni DP World yataendelea kubaki Serikalini;

(vii) Mwekezaji atalipa kodi na tozo zote za Serikali kwa kuzingaia Sheria za Tanzania;

(viii) Sheria za Tanzania zitatumika katika utekelezaji wa Mikataba hii,

(ix) Kutakuwa na fursa za watanzania kushiriki katika uwekezaji huu kupitia vifungu vya Sheria vinavyolinda maudhui ya ndani ya nchi (local contents), na

(x) Haki ya Serikali kujiondoa katika Mikataba hiyo imezingatiwa.

Source Mwananchi 23 october 2023
 

Attachments

  • Samia.jpg
    Samia.jpg
    37 KB · Views: 6
Back
Top Bottom