Nimejenga ujenzi rahisi kwa Milioni 7 tu

Nimejenga ujenzi rahisi kwa Milioni 7 tu

Wakuu, poleni na janga hili la corona. I hope mnachukua tahadhari zote ili kubaki salama. Basi leo nimeona vema nishee namna nilovokamilisha ujenzi wa kijibanda changu. Najua kuna mtu ntakua nmemsaidia na kumtia moyo kwamba kwa kidogo alichonacho, inawezekana kuepukana na adha za ma faza house.

Nyumba nimejenga ni ndogo ila inanitosha. Ni vyumba viwili vya kulala, sebule, choo na korido fulani ambapo ndo kuna jiko kupikia. Kiwanja nilinunua 25 kwa 25 nilinunua mwaka juzi 2018 kwa sh milion4.5 locationi ni madale mwisho. So nkaona kujenga nyumba kubwa itanichukua muda mrefu kulinganisha na kipato changu, so nkajenga nyumba hii ndogo pemben kabisa ya uwanza, na kuacha nafasi kubwa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba kubwa hapo baadae. Nyumba hii imeanza kuchimbwa msingi tar 22 feb 2020 na baada ya siku 29 me nkahamia.

Baada ya kuezeka milangoni na madirisha nmewekaMa drill. Na nyavu za kukinga mbu. Bado cjaweka plasta. Na chini ni rough floor. Sijaweka ceiling board , namaanisha dari. Hii nmeweka chooni tuu. Milango ya mbao ni miwili wa chooni na wa sebuleni. Umeme pia bado ila nmeshalipia nawasubiri jamaa wakuje kuwasha.

So nyumba hii cjacomplicate saana. Nmejenga simple tuu. Maana kuna bandiko niliona humu jf jamaa alisema ujenzi ni ww na maamuzi yako unatakaje. Unaweza jenga kwa m10 ramani ile ile ambayo mwingne kajenga kwa m20.

Gharama za ujenzi.
Vifaa vya ujenzi vyote vilinunuliwa siku moja. Tar 22 feb 2020. Lengo la kununua kwa siku moja ni kupunguza gharama za usafiri kununua kimoja kimoja. Nilinunua na nikaweka hapa kwa jirani yangu.

Vifaa vyote vilinunuliwa maduka ya madale mwisho. Actually kabla sijanunua nilienda maduka ya town tegeta kule, nkaulizia bei baada ya kupiga tathmin nkagundua cjakwepa kitu. Nei ni zile zile tuu. So nkaona bora ninunue madale ntasave kidogo kweenye usafiri. So gharama ni kama ifuatavyo.

Bati geji 32 @ 18,500 = 740,000
Cement 37 @13,500 = 499,500
Mbao papi 18 @ 10,000 = 180,000
Mbao kenchi 40 @ 5,800 = 232,000
Mbao zege 15 @ 75,000 = 112,5000
Misumari nchi 4 kg 10 @ 3,000 = 30,000
Misumari bati kg 9 @ 6,000 = 54,000
Misumari nchi 3 kg 2 @ 3,000 = 6,000
Koa 2 @ 3,500= 7,000
Nondo 10 @ 18,000 = 180,000
Sink la choo 1 @ 18,000
Bomba 2 nchi 4 @ 13,000 = 26,000
Bomba nusu nchi 1.5 @ 7,500 = 3,500
Pitrap 1 @ 2,500
Elbow 2 @ 3,500 = 7,000
Usafiri 40,000
Kuchimba shimo la choo 230,000
Mchanga tipa 4 @55,000 = 220,000
Kokoto tipa 1 @ 150,000
Tofali 1650 @ 1025 = 1,691,250
Grill madirisha 4 @ 150,000= 600,000
Grill mlango 1 @ 200,000
Grill dirisha choo 1 @ 30,000
Mlango wa sebule 150,000
Nyavu za mbu na zile zingne nilisahau kurekodi. Lets say 100,000

Fundi 1,300,000 ( alifanya kila kitu)
Saidia fundi 29 days @10,000 = 290,000
Chakula mchana 29 days @ 3,000= 87,000
Jumla niliyopata kwa gharama zote hizo juu ni
7,200,000


Sent using Jamii Forums mobile app
Hongera sana Mkuu nina cha kujifunza
 
Hongera sana mkuu ila kwenye ma grill ya madirisha manne ,mbona picha ya mbele tayari yapo manne ina maana nyuma hakuna dirisha hata moja au haujanunua umepiga bati kwenye dirisha?
 
Kawann umepaua kwa bati hizo??? Bora ungeoau kwa mgongo ndogo za rangi..

Halafu umeharakisha Sana...hiyo nyumba umejenga kwa kulipua sana
 
Una moyo yaani mpaka sink la choo na vifaa vyake umenunua kabisa kabla ya kuchimba msingi wa nyumba
Bro niliamua tuu. Nilikaa na fundi wangu, tukapanga bajeti. Nkamueleza aina ya nyumba nnayotaka. Bajeti tulipiga bada ya kujua bei ya vifaa. So nkacheki mfuko wangu nilikua na m6. Nkaamua naanza hivo hivo. Now here I am
 
Tukubaliane kuwa nyumba haijaisha,finishing bado. Plaster, zege,vigae/niru, top za madirisha
 
Hal
mkuu pole sana
Sina gharama specific za msingi. Me nilinunua tofali, cement kila kitu tukaanza ujenzi. Cjui msingi umekula tofali ngap, wala cement kiasi gani. Ckua na muda kuhesabu. Nilikua na kimbizana na kodi. Olikua inaisha mwez huo so sikua na plan kulipa kodi tena
 
Hongera mkuu

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
Picha
Hongera sana mkuu ila kwenye ma grill ya madirisha manne ,mbona picha ya mbele tayari yapo manne ina maana nyuma hakuna dirisha hata moja au haujanunua umepiga bati kwenye dirisha?
Ya mbele yako manne??? Cjui unahesabu vipi. Me najua mbele madirisha yako mawili na mlango. Pembeni kuna dirisha moja, na nyuma lipo moja
 
Picha

Ya mbele yako manne??? Cjui unahesabu vipi. Me najua mbele madirisha yako mawili na mlango. Pembeni kuna dirisha moja, na nyuma lipo moja
Mkuu picha ya kwanza juu inaonesha mbele na pembeni. Mbele kuna madirisha mawili,pembeni mawili jumla manne. Je upande mwingine usioonekana na nyuma hakuna madirisha?
 
Mkuu picha ya kwanza juu inaonesha mbele na pembeni. Mbele kuna madirisha mawili,pembeni mawili jumla manne. Je upande mwingine usioonekana na nyuma hakuna madirisha?
Upande wa nyuma kuna dirisha dogo la choo. Bahati sina picha. Labda kesho asubuh nipige picha
 
Back
Top Bottom