Nimeitwa kwenye interview NSSF kwa njia ya sms!!!

Ndibalema

JF-Expert Member
Apr 26, 2008
10,956
4,648
Wadau leo nimeitwa kwenye interview na NSSF. Namshukuru Mungu kwa hatua hiyo.
lakini Hofu zangu ni zifuatazo,
Kwanini watumie sms? wapo serious kweli?
Interview inafanyika IFM!! obvious ni watu wengi sana wameitwa, je ni kama ile ya UDOM na NHIF?
sms yenyewe inasomeka hivi,

We refer to your application for employment with NSSF. We would like to invite you for an aptitude test to be conducted at the Institute of Finance Management(IFM) campus Shaaban Robert street in Dar es Salaam on Saturday, 31st December, 2011 at 12:00PM.....
(nimeifupisha kuokoa muda)

Je kuna yeyote humu na yeye ametumiwa sms hiyo?
 
Mkuu we nenda pale ila uwe na tahadhari kubwa ikibidi uwe na mabaunsa maana jmosi hao jamaa hufanya kazi half day na ni mida hiyo ya ku duty off wao wanataka wakonduct interview halafu eneo tofauti waweza kuwa wazee wa david kameruni
 
Ingia kwenye mtandao, angalia website ya nssf. Utafute namba yao ya mawasiliano, tena landline. Wapigie uwaulize kuhusu hiyo interview na wakuambie kama ni kweli. That sounds fishy, mtajikuta wengi hapo na kuwa desperate na kuanza kudaiwa hongo. Utanasa mtegoni!
 
Tena hzo sms zimetumwa usiku wa mamane,hawa jamaa hawako serious kabisa[y/QUOTE]

Hawako serious kivipi? Watu waliotuma maombi ni zaidi ya elfu 20 na hawa jamaa walikuwa wanaumiza vichwa namna ya kuwapunguza watu ili wabaki wachache. Sasa kilichofanyika nahc ni kuwa namba zimeingizwa kwenye system na msg zimetumwa in bulk,zinatumwa ucku ili kuondoa congestion kwenye mtandao endapo zitatumwa day time.

IMPACT YAKE:
Wale ambao zitashindwa kuingia msg kwenye simu zao ndo imekula kwao waliopata ndo watajua hyo kitu na wanaenda kufanya mtihan kwanza b4 interview. Lengo wabaki wachaaachee.
 
Kama wewe ni Juma, Hamad,Issa, Ahmed and the like usiwe na hofu!
Acha kuendekeza mambo ya udini wewe!....tena hii inaonesha jinsi gani wewe ulivyo mdini ndo maana baada ya kutafakari na kutoa points za msingi we unaleta udini......ACHA HIZO ***** WEWE.
 
Hhahaha yale yale ya UDOM, NHIF, what i know hizo position tayari watu walishaanza training...nyie mnaenda kuzugwa tuu hakuna kitu hapo ni wizi mtupu...utakachofaidi ni kujuana na watu na kuonana na marafiki zako mliopoteana kwa muda...

Mkuu umesema ukweli yaani mimi nikifikiriaga hapo nashikwa na machungu yaani mnapigishwa foleni kupiga interview kumbe tayari mtu ameshapatikana wa kumuweka, this is bull sh***t
 
Kwanza Hongera Kaka kwa kuitwa kwa Interview!!
Hiyo inawezekana Brother ikawa ni kweli kabisa, huwezi jua kwa nini wameamua kukutumia sms labda watu ni wengi sana!!
Kwa mfano NHIF wao waliamua kutangaza kwenye Tv na Gazeti!!
Kwa hiyo mimi sioni kutumiwa sms ikawa ni Big deal ya wewe uwe na wasiwasi, kumbuka hiyo nayo ni means of communication!!
Cha msingi wewe nenda ukajaribu bahati yako!!
Mimi mwenyewe pia nilituma application bado nasikilizia!!
 
ni kweli mkuu, mi pia nimetumiwa sms ila bahati mbaya imefika nusu, nashukuru data nyingne nimepata kwako. Twende tukajaribu bahati zetu bila kujari kukatishwa tamaa na maneno ya watu. What i believe is that if God says Yes no one can say NO. Good lucky
 
hata mimi wamenitumia hyo sms mda huu2! je hizo aptitude test inakuwaje wadau?
 
We refer to your application for employment with NSSF. We would like to invite you for an aptitude test to be conducted at the Institute of Finance Management(IFM) campus Shaaban Robert street in Dar es Salaam on Saturday, 31st December, 2011 at 12:00PM.....

Kaka binafsi huwa nafurahi sana pole watanzania wenzangu wanapopata mafanikio ila hapa naomba niungne na wadau kuwa ''tahere'' hii jaribu kuwasiliana na nssf makau makuu ujihakikishie inawezekana mnajengewa mazingira fulani chafu usipuuzie hata hivyo tumuachie mungu
 
habari ndugu yangu! hata mm wamentumia sms lakn imekuja nusu....plls tunaomba ututumie full sms uliyotumiwa ww nasi tupateona
 
Back
Top Bottom