Nimeitwa kwenye interview NSSF kwa njia ya sms!!!

Hhahaha yale yale ya UDOM, NHIF, what i know hizo position tayari watu walishaanza training...nyie mnaenda kuzugwa tuu hakuna kitu hapo ni wizi mtupu...utakachofaidi ni kujuana na watu na kuonana na marafiki zako mliopoteana kwa muda...

Acha majungu, una ushahidi na hilo. Uncle nenda kwenye interview. Jiamini na jiandae vizuri, Ifahamu vema kazi uliyoomba na changamoto zake. Itetee taaluma yako, waonyeshe kuwa wewe umeiva. Jiandae kuwauliza maswali kadhaa na wewe. Kwa haya unaweza kufanikiwa by 80%. Achana na majungu

Wengi wetu kwenye interviews tunakosa kazi kwa uzuzu tu wa kuzoea kudesa madarasani, tunafikiri hata kwenye interview tunaweza kudesa.

NHIF na UDOM kila nafasi moja ilikuwa na waombaji 200 - 500 wote wana sifa unafanyaje? Wengine vilaza walikimbia written interview. Kama hujui na ulizoe kudesa, njoo ujiunge nasi na kazi ya uvuvi.
 
Tena hzo sms zimetumwa usiku wa mamane,hawa jamaa hawako serious kabisa[y/QUOTE]

Hawako serious kivipi? Watu waliotuma maombi ni zaidi ya elfu 20 na hawa jamaa walikuwa wanaumiza vichwa namna ya kuwapunguza watu ili wabaki wachache. Sasa kilichofanyika nahc ni kuwa namba zimeingizwa kwenye system na msg zimetumwa in bulk,zinatumwa ucku ili kuondoa congestion kwenye mtandao endapo zitatumwa day time.

IMPACT YAKE:
Wale ambao zitashindwa kuingia msg kwenye simu zao ndo imekula kwao waliopata ndo watajua hyo kitu na wanaenda kufanya mtihan kwanza b4 interview. Lengo wabaki wachaaachee.

yaani wanashindwa ku shortlist inamaana hawajui wanahitaji watu wa aina gani? usiishi kwa hisia nyepesi kama hizi. ni wavivu hao, walipoteza uelekeo
 
jamaa wamentumia hii msg leo . ha ha ha ha ha hawapo nais wahuni , wamentumia siku ya deadline , siku moja kabla ya mtihani wenyewe , then sipo dar ,
 
yaani wanashindwa ku shortlist inamaana hawajui wanahitaji watu wa aina gani? usiishi kwa hisia nyepesi kama hizi. ni wavivu hao, walipoteza uelekeo

Mzigo wa mwenzio kanda la sufi. Umeshajiuliza mwaka wenu mmemaliza chuo wangapi? Wangapi hawana ajira? Wangapi wana sifa zinazotangazwa hawana ajira au wanataka kubadilisha ajira? To be fair wote wenye sifa wapewe nafasi sawa na vilaza waliopita mitiahani kwa kudesa ili kupata vyeti wajichuje wenyewe. nyie vijana mna shida, wengi wenu mnasomea mitihani na siyo ujuzi. Ukiwa mahiri mwajiri hawezi kukutupa nje kwa sababu hakujui. Nani anataka kuharibu biashara yake?
 
Back
Top Bottom