Nimeitwa kuanza mafunzo ya jeshi la zimamoto

Nimeitwa kuanza mafunzo ya jeshi la zimamoto

Nahisi huyu anadanganya. Mwaka juzi wakati watu wameomba mwaka jana then waliopita wakastopishwaa. .@Ayochemichal toa taarifa ya kueleweka la sivyo tunashauri hewa
 
Majeshi Tanzania ni haya tu;
1. JWTZ baba yao
2. POLISI mtoto wa kwanza
3. MAGEREZA mtoto wa pili
4. JKT mtoto wa mwisho ambaye bado anaishi kwa baba

Hao wengine sijui zimamoto ni kikosi, uhamiaji ni idara ndio maana wako chini ya utumishi sawa na walimu manesi

Hata pia katiba inatambua majeshi ni jw polisi Magereza na jkt ndo maana utawaona pale uwanja wa Uhuru wakipiga kwata
 
Kuchamba kwingi mwisho unatoka na Mavi
1. Jeshi la Polisi
-----------(a) Trafick
----------(b) FFU
2. Jeshi la Zima moto
3. Jeshi la Wananchi
-----------(a) Jeshi la majini (Navy)
-----------(b) Anga (Air Force)
-----------(c) Nchi kavu (Combat)
4. Jeshi la Uhamiaji
5. Jeshi la Kujenga Taifa
6. Jeshi la Magereza
akhasante bwana Troll aka Putin hapa swadakta nimekuelewa kwa kudadavua
 
hivi na wale wa uhamiaji mwaka jana november veepeee.... au ndo hewa.....
 
Yan we postpone na kama ikishindikana acha kabisa chuo nenda depo, mtaa sio poa kabisa
 
  • Thanks
Reactions: zzz
Uhamiaji imekua jeshi.fuatilia na ujue m
Ni kweli ambapo idara ina vitengo vifuatavyo
  1. Divisheni ya Pasi, Uraia na Utaifa;
  2. Divisheni ya Visa, Pasi na Vibali;
  3. Divisheni ya Usimamizi na Uthibiti wa Mipaka;
  4. Ofisi ya Zanzibar;
  5. Divisheni ya Utawala, Fedha na Uhasibu;
  6. Kitengo cha Sheria;
  7. Chuo cha Taaluma za Uhamiaji Tanzania; na
  8. Ofisi za Uhamiaji za Mikoa
[/QUOTE
Majeshi Tanzania ni haya tu;
1. JWTZ baba yao
2. POLISI mtoto wa kwanza
3. MAGEREZA mtoto wa pili
4. JKT mtoto wa mwisho ambaye bado anaishi kwa baba

Hao wengine sijui zimamoto ni kikosi, uhamiaji ni idara ndio maana wako chini ya utumishi sawa na walimu manesi

Hata pia katiba inatambua majeshi ni jw polisi Magereza na jkt ndo maana utawaona pale uwanja wa Uhuru wakipiga kwata
Zimamoto na uhamiaji nayo yamebadilishiwa sheria ya yaliyoyaazisha na yamepewa hadhi ya majeshi zamani zimamoto. Ni kikosi na uhamiaji idara
 
Si kweli jeshi la zimamoto hakuna kozi inayoendeshwa saivi angalia usitapeliwe, kwa Maelezo zaidi nenda Makao yao makuu jengo la usharika mnazi 1,,,,,over
 
Mkuu hebu nisaidie, hivi nini maana ya neno 'jeshi'?
Tusiende mbali kama wabunge bungeni wanaliongelea jeshi la zimamoto na uokoaji, pia raisi kamteua kamishna generali wa jeshi la zimamoto na uokoaji ina maana lingekua sio jeshi asingetamka neno jeshi, sema watz wengi vichwa vyao vimejaa funza kama hao wanaobisha kua fire sio jeshi
 
Kama lengo ni kujiajili endelea
Kama lengo ni kuajiliwa ailisha mwaka

hairisha masomo, nenda kwenye mafunzo mtaani sio mkuu

mwenyewe niliombagA bt nimedilitiwA kamA veep fanyA mpangO wA deferment huko chuO then kapige depo si unajuA mzee wA chatO aelewekI

Salama Mdogo wango, Nenda

Nenda zimamoto kwanza asee chuo utakuja kumalizia baadae Ajira Ngumu sana sana kwa sasa

Hairisha mwaka ndugu kamata ajira then urudi shule sio kesi

Nenda zimamoto...usije ukajutia baadae...hxo coz zenyewe watu wapo kibao aamesoma na hawana ajira...

Binafsi nakushauri uende kwenye ajira kwasababu shule tayar unayo ukiahirisha bado hujaikosa lakini ajira huna ukiipotezea umeikosa...so ili usiwe looser NENDA ZIMAMOTO.

Nenda zimamoto
Siku hizi ajira ngumu bahati haiji Mara mbili.....postpone chuo zen ukimalizana na zimamoto utarudi chuo ukiwa tayari una ajira

Kama hii ni habari ya kweli ahirisha masomo chuoni uende mafunzo halafu utakuja kumalizia chuo ukiwa na ajira yako, huku mtaani sio kwa mchezo mchezo sasa hivi..

Dah kaka kama me nakushauli uende uko zmamoto kwanza IPO mambo ya ndani pili ata nafas ya kusoma zpo

Yan we postpone na kama ikishindikana acha kabisa chuo nenda depo, mtaa sio poa kabisa
Hivi ni nani aliyewadanganya kwamba ukienda mafunzo ya Zimamoto ni ajira ya moja kwa moja? Au ni utaratibu mpya?
 
Hivi ni nani aliyewadana kwamba ukienda mafunzo ya Zimamoto ni ajira ya moja kwa moja? Au ni utaratibu mpya?
Kwanza Hanna kozi inayoendeshwa saivi wala itakayoendeshwa mwaka huu, Huyo jamaa amepigiwa na matapeli
 
Hivi ni nani aliyewadanganya kwamba ukienda mafunzo ya Zimamoto ni ajira ya moja kwa moja? Au ni utaratibu mpya?
Ndo umuelekeze vizuri kijana wako basi apate uelewa wa kutosha
 
Hivi ni nani aliyewadanganya kwamba ukienda mafunzo ya Zimamoto ni ajira ya moja kwa moja? Au ni utaratibu mpya?
Bora umeuliza swali. mwaka juzi mwishoni walitangaza mmoja wa wadogo zangu aliomba pia. hilo ni jeshi la zimamoto hao ni kama polisi na magareza hama uhamiaji. najua jeshi hilo linachuo chake pale fire dsm kinatoa mafunzo kama chuo kingine pia. aliomba chuo cha zimamoto hama aliomba jeshi la zimamoto? Kwa ref ya mwaka juzi nakumbuka walitangaza nafasi za kazi jeshi la zimamoto
Tangazo la Kazi Jeshi la Zima moto na uokoaji Jan 2014


Jeshi la Zima moto na uokoaji

Phone: No calls required please
Position: Sajini Wa Zimamoto na Uokoaji (Sergeant of Fire and Rescue)-Nafasi 190

Location: Dar es Salaam
Deadline :Feb 1 2014

Descriptions:

Kamishina wa Jeshi la Zima moto na uokoaji anawatangazia Watanzania wenye Sifa kutuma maombi ya kazi kujaza nafasi za kazi zifuatazo;

Qualifications:
Sifa za Mwombaji.
Mwombaji awe amehitimu na kupata cheti cha mtihani wa kidato cha sita.
Mwenye ujuzi katika fani zifuatazo atafikiriwa zaidi.
Na diploma ya kawaida ya Uuguzi au awe na cheti cha majaribio ya ufundi Daraja la 1 katika moja ya fani ya Umakenika , ufundi bomba, ufundi umeme, uchomeaji, ufundi uashi na ufundi seremala.

Kazi za Kufanya.
i.Kusimamia kazi za chumba cha mawasiliano;
ii.Kusimamia kazi za uzimaji moto na uokoaji;
iii.Kuandaa utaratibu wa ukaguzi wa vituo vya maji vya Zimamoto (Fire Hydrants Inspection);
Kutunza kumbukumbu za kituo na
v.Kutekeleza kazi nyingine atakazopangiwa na viongozi wake wa kazi.

How to apply:
MASHARTI MUHIMU YA KUZINGATIA.
i.Mwombaji awe raia wa Tanzania mwenye umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 30, mwenye afya njema na ambaye hajaoa au kuolewa.
ii.Mwombaji awe hajatenda kosa lolote la jinai.
iii.Mwombaji awe tayari kuhudhuria mafunzo ya kijeshi kwa muda usiopungua miezi 6 kabla ya kuajiriwa.
iv.Mwombaji awe tayari kufanya kazi mahali popote atakaopopangiwa ndani ya Nchi.
v.Mwombaji aliyehudhuria na kufaulu mafunzo ya Zimamoto na Uokoaji yanayotolewa na Chuo cha Zimamoto na Uokoaji au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali , atafikiriwa kwanza.
vi.Waombaji wenye sifa waliohudhuria na kufaulu mafunzo ya Jeshi la kujenga Taifa.
vii. Barua zote za maombi ziambatanishwe na nakala za vyeti vya masomo ya kidato cha nne na sita pamoja na vya taaluma/ujuzi, wasifu wa mwombaji(CV),Ikiwa na majina ya wadhamini watatu na anwani zao, nakala ya cheti cha kuzaliwa na picha mbili ndogo za pasipoti.
viii. Mwombaji aandike kazi aliyoomba juu ya bahasha.
ix. Mwisho wa kupokea maombi ni Tarehe 1 Februari, 2014.
x.Barua zote za maombi zitumwe kwa njia ya Posta.
xi.Mwombaji wa kazi ya Sajini na Konstebo wa Zimamoto na Uokoaji watume barua za maombi kwa abnuani ifuatayo;

Kamishina Jenerali,
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,
S.L.P 5821,
DAR ES SALAAM.

Waombaji wa kazi ya Mkaguzi Msaidizi wa Zimamoto na Uokoaji watume barua za maombi kwa anuani ifuatayo:
Katibu Mkuu,
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
SL.P 9223,
DAR ES SALAAM.

From Daily News Monday January 20,2014.
 
Back
Top Bottom