Nimeipenda sana Hii Thread. Hebu soma na wewe uchangie. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimeipenda sana Hii Thread. Hebu soma na wewe uchangie.

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Joloe, Apr 21, 2011.

 1. Joloe

  Joloe Member

  #1
  Apr 21, 2011
  Joined: Jun 19, 2009
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  SKONGA SKONGA SKONGA

  Hivi jaman watu tunafauatilia vizuri kile kipindi cha SKONGA cha EATV kinachoenedeshwa na Alan. Kiukweli nampa big-up sana Yule dogo lakini kinadhalilisha taifa(sorry kama ni neno kali sana that is the way I see it). Sisemi hivi sababu nakichukia kipindi chenyewe ..hapana, bali jinsi umbumbu wa watoto wetu wa shule unavorushwa hewani dunia ione. Mwanafunzi anaulizwa Libya iko bara gani anajibu “mi sijui sijawahi kufika. Hii TV inatizamwa na watu wengi sana. Hivi viongozi wetu wanapata picha gani? Au wanasuburi wakifa tujijue na li nchi letu. Kiukweli ukichunguza sana utaona vijana wengi walioko sekondari they know nothing. Hata maswali ya kipuuzi kabiisa watasema hawajui. Binti anaulizwa na Alan kuwa ni mwenyeji wa wapi akasita kwanza kwa kutokuelewa mantiki ya swali lenyewe..Alan akauliza tena wazazi wako wanatokea mkoa gani, akajibu Tabora

  Mwanafunzi anaulizwa nitajie chief wa Tabora anasema hamjui halafu animezaliwa Dar kwa hiyo mambo ya huko hayajui.Lakini msichana kama huyu ukimuuliza Alehandro wa tamthilia ya Ralavencha anaelewa kila hatua ya EPISODE. Sa sijui kama viongozi wetu wanangalia hiki kipindi na ku figure out ni taifa lipi wanaliandaa? Au ndo habari za watajijua wenyewe. Ukiacha hawa wanafunzi kutojua kitu pia tunadhalilika mbele ya uso wa wanaotuona. Kila siku tunapiga kelele mafisadi mafisadi lakin tunajua kama taifa linateketea kwa ajili ya kuua kizazi hiki. Katika taifa hili kuna anaeona HAKI ELIMU wanafanya nini(they are so good these people). Nadhani sasa inabidi tubadili ile kauli yetu ya MUNGU IBARIKI TANZANIA ila tuseme MUNGU INUSURU TANZANIA. Mi si mwandishi mzuri lakini nimetoa dukuduku langu.
  Sorry for bothering to dare.

  Hivi watotO wetu wataweza kuingia kwenye challange ya EAST AFRICAN COMMUNITY kweli na uozo huu?????????????????????
   
 2. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #2
  Apr 21, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Ni kweli hicho kipindi watotot wa secondary hawaelewi kitu kabisa ni aibu sana kwa taifa
   
 3. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #3
  Apr 21, 2011
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,031
  Likes Received: 3,223
  Trophy Points: 280
  Sio secondari tu,,hata vyuo vikuu. Refer zain university competition ndo utaelewa namaanisha nini.
   
 4. MkimbizwaMbio

  MkimbizwaMbio JF-Expert Member

  #4
  Apr 21, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Lakini mkuu maswali ya "zain university competition" ni ya kitotot sana wali sio ya level ya chuo kikuu.
   
 5. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #5
  Apr 21, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Inasikitisha sana kwa Taifa letu kwamba vijana wamekuwa wagumu kujifunza mambo ya msingi ambayo yangeweza kuwasaidia. Lakini hapa tusitupe lawama zote kwa serikali, nasi wazazi tumewapa sana uhuru vijana wetu na wanafanya vile wanavyoona inafaa kwao kwa sasa. Wazazi tunawajibika kuhakikisha watoto wetu wanajifunza nini? katika maisha yao ya kila siku. Siku hizi wazazi tumeziachia zaidi shule, haswa pale ambapo tunapata uwezo wa kuwapeleka hizi shule za binafsi huwa tunaamini huko watajifunza kila kitu na kuhasau kwamba wengi wanaomiliki shule hizi wako zaidi kibiashara.

  Wito wangu kwa wazazi tuchukue hatua nyumbani kuhakikisha vijana wetu wanapata muda wa kujifunza vitu vya msingi, binafsi nimejaribu kuweka utaratibu wa kuhakikisha kwamba watoto wangu wanaangalia taarifa ya habari kila siku na kuchukua notice. Vijana wengi hawafuatilii hata taarifa za habari na badala yake wanasubiri muda wa kuangalia tamthilia ambapo hapo binafsi sioni kama kuna kitu wanachojifunza zaidi ya burudani.
   
 6. assa von micky

  assa von micky Senior Member

  #6
  Apr 21, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 146
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hiyo ni trela picha kamili inakuja, shule za kata ,vyuo vikuu vya kata ,siasa hata kwenye mambo ya taaluma ,,wanafunzi kuanzia shule za msingi ,sekondari hadi vyuo hawana habari na maarifa ya kujitafutia ,wao wanachokijua ni kukopy na kupaste,,
   
 7. Obe

  Obe JF-Expert Member

  #7
  Apr 21, 2011
  Joined: Dec 31, 2007
  Messages: 5,978
  Likes Received: 20,356
  Trophy Points: 280
  Vijana wengi hawapendi kujisomea kwa ajili ya kupata taarifa, sikai kusikiliza muziki lakini ni vizuri kutumia muda mchache kupata taarifa na hasa kwa kusikiliza taarifa za habari, kusoma magazeti na majarida ya maarifa. Inashangaza sna kijana wa sekondari hajui Libya iko bara gani, au kw vile yy sio mkazi wa tbr hajui mkoa huo unaongoza kwa uzalishaji wa zao gani la biashara
   
 8. A

  Aine JF-Expert Member

  #8
  Apr 21, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ni kipindi kizuri ila uelewa wa wanafunzi ndiyo tatizo. Kama ulikuwa unafuatilia kile kipindi cha Msoud Kipanya cha kutafuta wawakilishi wa Maisha Plus mikoani, zile interview walizokuwa wanafanyiwa! mtu anaulizwa ataje Mawaziri wakuu angalau watatu waliopita waliowataja ni aibu hata kusema hapa. Kweli nami nakubaliana kwamba hata wazazi wanachangia watoto kutokufanya vizuri shuleni na hatimaye makazini kwa kuendekeza tu umagharibi. Utakuta mtoto anaangalia kipindi ambacho hata wewe mzazi huwezi kuangalia lakini mtoto humkemei so anaona ni kawaida tu as far as mzazi kaniona na haja comment chochote basi ndiyo inakuwa hivyo hadi anakua. Hapa ni suala la wazazi na walimu si walimu pekee, walimu nao wanachoka hasa mtoto akijifanya sharobaro, wanamuacha tu better waendelee na wanaowasikiliza!
   
 9. Cestus

  Cestus JF-Expert Member

  #9
  Apr 21, 2011
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 1,000
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  hapo kwnye la revancha umenikumbusha mbal....!
   
 10. sweetdada

  sweetdada JF-Expert Member

  #10
  Apr 21, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 540
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Joloe,

  kwa kweli nikiangalia avatar yako natishika naweza kuota usiku for real duuh
   
 11. jockey emmanuel

  jockey emmanuel JF-Expert Member

  #11
  Apr 21, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 330
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  nimeipenda kwa kweli yani hapa tz wanaopata elimu yenye uafadhali kdg ni wanafunzi wa private xculz....mi nipo barbro,hapa tunawaonaga wanafunzi wa kwembe wakipita...ukiongea nao wana sema walimu ndo wanasepa saa 4 wanafunzi wanaenda shule wakijisikia...unadhani wata mjua huyo chifu wa tabora...?inasikitisha kuona kuwa jambo hili limeshika nafasi sana...niliongea na wanafunzi nlomaliza nao drs la 7...wengi wameacha shule kisa masomo magumu...inasikitisha,eti english ni ya private scholars....je tutafika?...
   
 12. Barbie Maliposa

  Barbie Maliposa Senior Member

  #12
  Apr 21, 2011
  Joined: Feb 9, 2011
  Messages: 153
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  JOLOE,Naogopa kweli hiyo avatar yako........:scared::scared::scared:
   
 13. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #13
  Apr 21, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Haya ndo matokeo ya taifa lililokumbatia siasa likaacha tasnia nyingine!!!!
  Haya ndo matokeo ya viongozi wanao waza matumbo yao na kusahau wananchi!!!!
  Haya ndo matokeo ya kuanzisha shule za kata bila mchakato mathubuti!!!
  Haya ndo matokeo ya kujivua gamba ka kichwani ukasahau magamba ya sehemu nyingine za mwili!!!
   
 14. Joloe

  Joloe Member

  #14
  Apr 21, 2011
  Joined: Jun 19, 2009
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakika ndo mambo peke vijana wetu wanayojua. hata wengine ukiwauliza kwa haraka ukamkurupusha ataje rais wa nchi kabal ya JK atanaweza sema hata Mrema.
   
 15. Joloe

  Joloe Member

  #15
  Apr 21, 2011
  Joined: Jun 19, 2009
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Boss hiyo ni kuonyesha nina hasira sana. Nchi yetu imekuwa kama haina wenyewe. Hili ndo zao linalopelekea watu baadaye wanashindwa kuvumilia wanaamuia kupambana na kuuana.
   
 16. Joloe

  Joloe Member

  #16
  Apr 21, 2011
  Joined: Jun 19, 2009
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Usiogope hayo ni majicho tu.
   
 17. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #17
  Apr 21, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  chukua hatua Tafakari.....
   
 18. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #18
  Apr 21, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  Kitu cha Rodriguez Asniegas... Haha!
   
 19. T

  Thatoo New Member

  #19
  Apr 21, 2011
  Joined: Apr 21, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yeah....! Kweli watoto wetu /wadogo zetu kwakweli wanasikitisha......huwa najitahidi kutazama kipindi kile mara kwa mara kirushwapo lakini huwa mimi binafsi japo sijaulizwa swali ....lakini huwa nahisi rohoyangu kuumia sana hasa nionapo jinsi vijana wanavyokimbia camera, hawapendi kuulizwa maswali kabisaaa ......!!! naweza kusema sio ni kuogopa make wanajua hakuna walijualo kwayale watakayo ulizwa na muongoza kipindi ni aibu kubwa sana , nakumbuka mmoja aliwahi kuulizwa swali anasema atajibu lakini asi chukuliwe video, huyu alikuwa mwingi sana wa kiswahili lakini nasikitika hakuwa na chochote kichwani kabisa wa kike huyu alikuwa na walifatia wengi wa kiume nao vilevile , labda tuu tungemuuliza bwana Alan wa mtangazaji popote alipo , atupe takwimu fupi ya nini anachokiona na tatizo ni nini hasa anapowauliza maswali watoto hawa ,manake utafikili wamerogwa hivi............!! kabisa maswali ya darasa la 5-6-7 hawajui kabisa hawa, ni aibu sana , make ninachojiuliza ni je ...?? watoto wa huko Burundi, Rwwanda, Uganda ,Kenya nasikia mpaka Lilongwe huko wanaipata EATV, wanawachukuliaje hawa watanzania wadogo wanaposhindwa maswali ya uelewa wa kawwaida rahisi kabisa.....?? mi nadhani jitihada zinahitajika laa sivyo ......naogopa hata kusema kwamba hawa Rwanda na Burundi mpaka hapa tunaweza tusiwashike tena baada ya miaka michache, ni aibu kubwa ........Alan popote ulipo tusaidie mawazoyako
   
 20. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #20
  Apr 22, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Dah! Enzi zetu sisi, ukimgusa tu mtoto wa shule kwa maswali kama hayo, anakutajia kila bila wasi wasi wowote.

  Kwanza tulikuwa tunawajuwa viongozi wote wa chama na serikali, yaani si mawaziri tu hata makatibu kata wa jimbo lako karibia wote unawajua.

  Si hayo tu, nchi zote za duniani na mazao yao makuu, kijiografia na mengine kadha wa kadhaa.

  Sijui kizazi iki kimekubwa na maradhi gani.
   
Loading...