Nimeipenda sana Hii Thread. Hebu soma na wewe uchangie.

Dah! Enzi zetu sisi, ukimgusa tu mtoto wa shule kwa maswali kama hayo, anakutajia kila bila wasi wasi wowote.

Kwanza tulikuwa tunawajuwa viongozi wote wa chama na serikali, yaani si mawaziri tu hata makatibu kata wa jimbo lako karibia wote unawajua.

Si hayo tu, nchi zote za duniani na mazao yao makuu, kijiografia na mengine kadha wa kadhaa.

Sijui kizazi iki kimekubwa na maradhi gani.
hiki kizazi kimeuliwa,jaribu kupitia vitabu vya hasa vya mitaala vinavyo tumika shule za msingi na secondary.
tumlaumu mungai kwa nguvu zote alipoleta hoja ya kuchanganya masomo mfano somo la maarifa ya jamiihili somo limekusanya masomo matatu geography history na uraia uelewa wangu walimu husomea masomo mawili lakini mwalimumhuamua ama hutokea kuwa competence kwenye somo moja, sasa kwa kuyaunganisha haya masomo bila kuwaawnda waalimu mungai aliamua kuua elimu ya msingi,
ukichunguza wanachosoma shule ya msingi chini ya somo la maarifa ya jamii sio history wala sio geography ila wanasoma kitu nusu ya hapo sijui kitaitwaje,
njoo hilo liitwalo stadi za kazi ni mseto wa masomo yafuatayo sanaa&muziki, ufundi,sayansi kilimo na sayansi-kimu pia linajumuisha michezo, hapa kweli tunaweza kutengeneza syllabus kwa kuchanganya mseto huu!!!
alitaka pia kuunganisha phisics na chemistry o'level ila ukifika form three yanatenganishwa
hii ndiyo sumu iliyo anza kuua elimu yetu, ili kuweza kukidhi huu mchanyato mambo ya msingi kwenye syllabus yaliondolewa yaliachwa machache sana ambayo ni ya msingi,NINAWEZA KUSEMA DARASA LA KWANZA MPAKA LA SABA WANAJIFUNZA KUSOMA NA KUANDIKA,ALIYE DARASA LA SABA ANA MIAKA 7 HERUFI ZOTE ANAZIJUA NA HANA WALIMU WA KUMBADILISHIA MAZOEZI ACHA AANGALIE RALEVANCHA MAANA ELIMU YA DARASANI INAONESHA KUTO MSAIDIA LABDA HII YA WEZA KUMSAIDIA KUMTUNZA MUMEWE AU MKEWE HAPO BAADAEnani anajua?? ya mungu mengi
 
Hii mada imenikuna sana, pamoja na mengineyo huko nyuma kulikuwa na competition kubwa sana katika kupata nafasi za kuingia sekondari, hivyo karibu wote waliokuwa wanajiunga na sekondari walikuwa na uwezo, siku hizi hasa baada ya kuanzishwa kwa shule za kata kiwango cha ufaulu wa kuingia sec. kimeshuka na bado maeneo mengine wanatafuta wanafunzi tofauti na zamani.

Elimu ya siku hizi ni kucrame maswali na past papers, hivyo wanafunzi wanakuwa na uwezo mdogo wa kufikiri na kupanuka kimawazo.

Uchakachuaji wa mitihani yaani wizi - angalau mwaka huu inaonekana kulikuwa na udhibiti mkali wa mitihani ndio maana matokea hayakuwa mazuri. Udhibiti ukiwa mkali kiwango kitakuwa na zoezi hili lianzie shule za msingi. Uchakachuaji unaakuwepo kwa vile walimu wakuu wanaambiwa wataadhibiwa ikiwa hawatafaulisha, je unategemea mwalimu afanye nini badala ya kuiba mitihani ili aokoe ajira.
?
Mitihani ya darasa la nne na form II irudishwe, ni bora mwanafunzi arudie darasa hata mara tatu kuliko kumsukuma madarasa ya mbele matokeo yake tunapata wahitimu mbumbumbu. Sio lazima kila mtoto aende sekondari, hawa wana ajira zao bora waandaliwe, hivi kila mtu akifika chuo kikuu nani atasukuma mikokoteni?nani atachuma chai?nani atachimba mitaro?nani atavua samaki? any way thats a joke, nadhani ni muhimu tukiwa serious na mfumo wa elimu yetu.

Haya ni macheche nadhani wanajamii wanayo mengine niwape nafasi.
 
sio lazima kujua kila kitu, sasa ukimjua chifu wa tabora ndio utajuwa ushaelimika??
 
sio lazima kujua kila kitu, sasa ukimjua chifu wa tabora ndio utajuwa ushaelimika??


yaelekea wewe ni mmoja wa watu wenye stake katika shule hizo ndiyo maana unawatetea. Mtoto kidato cha pili anaulizwa swali rahisi hivyo anashindwa wewe unaona siyo ishu!
Kuna uozo upo kwenye hizo shule ni vizuri tujue, ada inayolipwa hizi shule inatakiwa iendane na output.
 
It should be taken as a challenge. Hiyo aibu ifanye tuboreshe miundombinu kielimu. Too bad our president is Just Kidding (J. K.)
 
Kwani hamjui km siku hizi kuna certificate without education!!
Skuli kibaooo, lkn watoto hawajali hata kusoma, wanajua ikifika time ya mitihani usahtayarishiwa pepa na majibu yake ni copy and paste tu.
Matokeo yakija wamepasi, lkn kichwani hamna kitu, hawahawa ndo baadae wanakua na nyadhifa kubwa kubwa makazini. Nani anajali!!!?
 
Yaani niliwacheki hao watoto siku moja , ilibidi nizime tv yaani hawa watoto wa sasa hivi hamna kitu kichwani hata kidogo.
 
Siasa huvuruga ufanisi wa mambo, walitangaza F.II kuna kurudia bila 30 sasa wamesema tusubiri mwaka mwingne, ukifika kutajitokeza jingne. Hapo lazima kuwa na wanafunzi vilaza wengi. Nawashukuru mlionikumbusha zamani tulipoweza kutaja nchi nyingi, viongozi wake, uchumi wake, masuala ya uhuru, n.k ktk enzi zisizoitwa enzi za habari/tehama,sayansi na techn. n.k! Sasa vyote hivyo vipo, kuhabarika kwa watoto wetu na maarifa viko wapi??
Tungeanza kwa kuitazama tena Patriotic song! Tanzania.. Tz...nakupenda kwa moyo wotee... Mambo gani hayo!
 
Siasa huvuruga ufanisi wa mambo, walitangaza F.II kuna kurudia bila 30 sasa wamesema tusubiri mwaka mwingne, ukifika kutajitokeza jingne. Hapo lazima kuwa na wanafunzi vilaza wengi. Nawashukuru mlionikumbusha zamani tulipoweza kutaja nchi nyingi, viongozi wake, uchumi wake, masuala ya uhuru, n.k ktk enzi zisizoitwa enzi za habari/tehama,sayansi na techn. n.k! Sasa vyote hivyo vipo, kuhabarika kwa watoto wetu na maarifa viko wapi??
Tungeanza kwa kuitazama tena Patriotic song! Tanzania.. Tz...nakupenda kwa moyo wotee... Mambo gani hayo!

Tulikuwa tunajua mikoa yote na inalima nini kama zao la chakula,au biashara. Darasa la tano mtu anachora ramani ya Tanzania na mikoa yote(enzi hizo-25),bila wasi!

Kama si mazao basi unakuwa unajua mikoa inayotegemea uvuvi,bandari,n.k.

Tunajua mpaka viwanda vyote vilivyopo mikoani,na sababu ya viwanda hivyo kuanzishwa...
Ah.. Elimu ilikuwa zamani bana!
 
Back
Top Bottom