Nimeikubali hii...sina cha kuongeza...wewe je??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimeikubali hii...sina cha kuongeza...wewe je???

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Dark City, Dec 15, 2011.

 1. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #1
  Dec 15, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  [TABLE="class: yiv58725715MsoNormalTable"]
  [TR]
  [TD]Je umejipangaaje? Hapo mwanzo Mungu aliumba ulimwengu na wanyama wake. Kila mnyama alipewa
  miaka ya kuishi 30. Kati ya wanyama walioumbwa walikuwa Punda, Mbwa na
  binadamu. Mungu akawauliza wanyama hao Je! unadhani miaka hiyo thelathini
  inakutosha? Kila mmoja akajibu hivi:

  Punda: Mimi nikae nikitumikishwa miaka 30, niwe kihongo miaka yote hiyo?
  Loh! kazi hiyo ni kubwa sana . Mimi nipunguzie iwe miaka 10 tu inanitosha
  bwana.

  Mungu: Sawa wewe utaishi miaka kumi tu.

  Mbwa: Mimi nikae nikilala nje miaka thelathini! Kula majalalani, kubweka
  usiku kucha. Naomba unipunguzie niishi miaka kumi tu inanitosha.
  Nitajitahidi kwa kipindi hicho kulala nje, kubweka na kulinda usiku kucha.
  Watanitumia wapendavyo kunusa madawa ya kulevya, kukamata wanyama nk.

  Mungu: Sawa, umri wako utakuwa miaka kumi.

  Binadamu: Ha! Miaka 30 tu, nita enjoy nini mimi? Niongezee bwana.

  Mungu: Sawa, niliyoipunguza kwa punda na mbwa utaongezewa wewe. Nawe
  utaishi miaka sabini (30 + 20 + 20 = 70). Kipindi chako cha miaka 30
  utaishi maisha yafaayo binadamu, miaka ishirini inayoongezeka utakuwa na
  maisha ya punda, na miaka ishirini inayoongezeka utakuwa na maisha kama ya
  mbwa.

  Binadamu: Ahsante sana bwana na iwe kama ulivyosema.
  Miaka 0 – 30+: Maisha mazuri sana (hayo ndiyo maisha ya binadamu). Maisha
  ya kutafuta marafiki, maisha ya kulishwa, maisha ya kuwaandikia barua girl
  friends na boy friends, kutafuta pen pal. Maisha ya kuangalia mtindo mzuri
  wa nguo, nywele, kutembea kwa mikogo, kutuma message kila dakika,
  kupigiana simu kila saa, ugomvi usio na kichwa wala miguu, kujifunza
  kuvuta bangi, kunywa pombe, kuhudhuria madisco n.k.

  Miaka 35 – 50: (Maisha ya punda). Wengi wanajitegemea wameoa au kuolewa.
  Maisha magumu, unapanga chumba lakini mhh kodi sasa watoto watano na mke
  chumba kimoja, kibarua wa kubeba zege, kimbiza shilingi, huna muda wa
  kwenda disco tena au kuangalia mitindo mipya, hakuna kulala hapa. Watoto
  wanasumbua shule, wanaumwa, kadi nyingi za harusi, madeni hadi unawakimbia
  marafiki zako. Hii itaendelea hadi upite umri wa miaka hamsini.

  50+ tuseme 60: Mstaafu. Unakaa nyumbani, unalinda boma (maisha ya mbwa),
  nyumba imebomoka huna pesa ya kurepair, nyumba inavuja, watoto wote
  wameondoka wanahangaikia maisha yao na wake/waume zao. Huna jinsi wewe ni
  kama mlinzi wa eneo ulilochagua.

  Je! Katika maisha haya upo kundi gani? Jiandae hatua unayoendea ni ngumu
  zaidi. Jipange, wakati ni huu.


  JIPANGE SAWASAWA!!


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  Source: Mitandao

   
 2. Jakubumba

  Jakubumba JF-Expert Member

  #2
  Dec 15, 2011
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 1,627
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Napita tu topic ngumu kwangu ngoja niwasubili wachuzi wakuje!!!!!!!!!!!!!!!
   
 3. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #3
  Dec 15, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Wewe uko stage gani??

  Kwetu sie tulio kwenye vipindi vya punda au mbwa tumeguswa kweli kweli!!
   
 4. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #4
  Dec 15, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Mi stage zote hizo nimemeliza sijui inafuata ipi hapo
   
 5. Jakubumba

  Jakubumba JF-Expert Member

  #5
  Dec 15, 2011
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 1,627
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135

  mimi niko hio stage ya mwisho kabisa "jipange sawa sawa" hizo zingine nilisha pita, ila duu mshikaji sijui umefikilia nini hapo!!!!!!!!!!!!!! umegusa life zima mkuu!
   
 6. happiness win

  happiness win JF-Expert Member

  #6
  Dec 15, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 2,478
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Du! Hairuhusiwi kurudisha mkanda nyuma???? Maana hivi karibuni nitakuwa punda!
   
 7. W

  Wababa Senior Member

  #7
  Dec 15, 2011
  Joined: Jul 21, 2011
  Messages: 159
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hahahahahahahah
   
 8. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #8
  Dec 15, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160

  Pole sana Happinnes,

  Ndio maana wahenga walisema kuwa ujana ni maji ya moto!!

  Babu DC!!
   
 9. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #9
  Dec 15, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  ndo stage za maisha,dah sasa hivi natamani ningekuwa na ufahamu kama wa sasa halafu nirudishwe mdogo miaka kama 20
   
 10. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #10
  Dec 15, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Kuimbiwa pambio,.....LoL:eyebrows:!!!
   
 11. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #11
  Dec 15, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  stage ya nyoka,utakuwa unatambaa
   
 12. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #12
  Dec 15, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160

  Hiyo haiwezekani ila unaweza kuitumia vizuri hiyo stage uliyopo ili upate maximum returns!!
   
 13. harakat

  harakat JF-Expert Member

  #13
  Dec 15, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Stage ya simba ipo kwani?
   
 14. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #14
  Dec 15, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 739
  Trophy Points: 280
  Napita tu.
   
 15. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #15
  Dec 15, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  kwani ile miaka mitano ya mbwa imeenda wapi??
  Mi naitaka ile.......au mungu hajui hisabati?
   
 16. k

  kifuniboy Senior Member

  #16
  Dec 15, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 191
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  we nyambafu hili ni jukwaa la utani,na sisi sote hatutaniani na MUUMBA wetu

  kasafishe masaburi yako na uombe msamaha.,
   
 17. Mbimbinho

  Mbimbinho JF-Expert Member

  #17
  Dec 15, 2011
  Joined: Aug 1, 2009
  Messages: 6,027
  Likes Received: 2,868
  Trophy Points: 280
  Mmh, mi mbona nilianza na hiyo ya punda kabla hata ya kuanza darasa la kwanza, vipi ndio kusema kuwa inayofuata tena itakuwa hii hii?
   
 18. Rosweeter

  Rosweeter JF-Expert Member

  #18
  Dec 15, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 1,136
  Likes Received: 3,890
  Trophy Points: 280
  Sali sala yako ya mwisho
   
 19. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #19
  Dec 15, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,148
  Likes Received: 2,465
  Trophy Points: 280
  maisha ya mbwa wachache tutafika,ila yapunda tutayakoma.
   
 20. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #20
  Dec 15, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Mchezo woote upo 30 ya mwanzo... Ukichemka hapo lazima ugangamale ile mitano ijayo.... Ukichemka hapo.... IMO ndo unakua umechemka mazima thou sio lazima.... Kuna watu wamewahi toka kimaisha late 30s au early na late 40s....
   
Loading...