Zero Hours
JF-Expert Member
- Apr 1, 2011
- 12,943
- 18,665
Wakuu nimeibiwa simu mpya kabisa . Yani siku nimeinunua usiku ikaibiwa. Ni simu ya 1.7m. Siwezi sema ni aina gani mana uyo mwizi anaweza kuwa humu.
Naombeni ushauri nifanyeje ili niipate. Polisi nimeisha enda kwa kitengo cha cyber crime na pesa ya maji nimewapa ili wanitaftie, ila wananizungusha mpaka sasa.
Nimetenga 300,000 kwa atakayenisaidia kumpata huyu mwizi coz kanipiga hata pesa.( Laki nane)
Update. 31 May 2017.
Nimefanikiwa kupata simu yangu. Jana ilikamatwa na leo polisi wamenikabidhi simu yangu.
Hivi ndvyo nilivyo fanikiwa kuipata.
Kwanza kabisa nilitoa report polisi baada ya kuibiwa simu. Uzuri nilikuwa na box ambalo lilikuwa na IMEI no za simu. Nilifanikiwa kupata RB na kupangiwa mpelelezi ambaye anahusika katika kitengo cha Cyber crime.
To be honest, hapa Tz hakuna kitu cha bure. So ili kumotivate huyu mpelelezi ilibidi nimpe pesa kidogo ambayo angetumia kwa costs zozote ambazo angekutana nazo ili afanikishe hilo zoezi mapema sana.
Hii simu iliibiwa tarehe 20 na nikaipata tarehe 30 mwezi huo huo. So ilichukua siku 10 mpaka kuipata. Upatikanaji wake umechukua kamda karefu kidogo sababu hawa wezi wa siku hizi wapo makini sana. Wao hawarisk hata kidogo kuweka line kwenye simu walizoiba.
Katika mazingira ya kuibiwa simu yangu ni kuwa aliyeiba alimpelekea muuzaji. Hawa ni kama receivers au wakala wa simu za wizi. Wao wananunua simu za wizi na kuziuza. Hawa wauzaji nao wapo makini sana. Hawarisk hata siku moja kuweka line. Wao wanasubiri atakaye nunua ndye awe wa kwanza kuweka line.
simu ilikaa siku 9 bila line kusoma. Siku ya 10 ndyo line ikasoma na ikatuma location ilipokuwa coz na internet iliwekwa on. Location ilipokuwa haikuwa mbali na kituo cha polisi. Yani ni kama 900m. So ndyo maafisa polisi kwenda fasta kwenye ile location na kukuta mnunuzi akimuhesabia laki 9 muuzaji. Wakamkamata na hatua za kipelelezi zinaendelea ili mwizi ajulikane.
Mytake.
1.Kuweni makini sana hasa pale mnaponunua simu za mkononi kupitia kwa watu msiowajua na si madukani.
2. Ukiwa unanunua simu used, hakikisha IMEI ya ndani ya battery au nyuma ya simu inaendana na inayoonekana kwenye system.
3. Unaponunua simu hakikisha unatunza box lake vizuri. Siku hizi polisi wanauliza box kuliko receipt maana receipt mtu anaweza enda dukani na akapewa tu.
4. Ukiibiwa simu, Report mapema sana polisi. Na polisi wape "ushirikiano".