Nimeibiwa 245,000/= MPESA VODACOM

chambalo kafao

Senior Member
Feb 8, 2014
193
209
Ndugu wana jamvi.
Jana saa mbili usiku nimeibiwa shilingi laki mbili na elfu arobaini na tano kwenye namba yangu ya vodacom yenye Mpesa. Fedha zimetolewa kwa wakala, na ujumbe nikaletewa kuwa nimepokea fedha taslimu toka kwa wakala huyo.

Ushahidi huu hapa.
6ES62D6M74W Imethibitishwa tarehe 28/5/19 saa 10:17 PM Pokea kiasi cha Tsh240,000.00 kutoka kwa 430185 - MWANAHAMISI RAJABU ISSA kwa ada ya Tsh5,000.00. Salio lako jipya la M-Pesa ni Tsh675.00.

Cha ajabu ni kuwa muda huo, mimi nilikuwa na simu yangu na sikufanya muamala huu.
Mara moja niliwapigia huduma kwa mteja Mpesa Vodacom ambao wamesema nisubiri masaa 72.
Swali kwa wataalam.
1.Ni nini hasa kimefanyika hadi namba yangu ikatoa fedha nipopajua ilihali simu yangu ninayo?
2. Je nitaweza kupata fedha zangu hizi?
3. Je niendelee kutumia namba hii au niachane nayo?

Nawasilisha.
 
Huwa namba zinaingiliana.
kama uliwahi kabla wakala hajampa huyo mtu pesa...utazipata.ila kama ulichelewa...kuna mawili.
1 wakala kulipa
2 kupoteza.

Ni kwa mara ya kwanza kutokea? Endelea na mamba yako ila badili nenosiri.
 
Tafuta humu kuna sehemu ya Vodacom watakujibu haraka halafu sio kusubiri tu nenda ofisi zao zilizopo eneo ulipo ili ikafanyie kazi na w/kazi utakaowatambua ili kama una malalamiko unakuwa unawajua watu kwa majina na sura. Pia unaweza kupeleka malalamiko yako polisi au TCRA
 
Ebu Fanya ulivyoelekezwa hapa
 
Mimi kulikuwa na mtindo, usiku mida ya saa 3 nakuta message ya kwamba sh 1000 imetolewa kwa wakala anaitwa J4U.

Kwa week unaweza Kuta twice au thrice nikabadilisha namba ya Siri. Things are good.

Voda nayo ni hovyo tuu
 
Tafuta humu kuna sehemu ya Vodacom watakujibu haraka halafu sio kusubiri tu nenda ofisi zao zilizopo eneo ulipo ili ikafanyie kazi na w/kazi utakaowatambua ili kama una malalamiko unakuwa unawajua watu kwa majina na sura. Pia unaweza kupeleka malalamiko yako polisi au TCRA
Nashukuru sana.
Naenda ofisi zao za Morogoro Mjini.
Nawashukuru wote kwa msaada.
Humu ndani Vodacom sijawapata bado.
 
hiki kipindi kigumu tutapigwa kila angle kwa kweli........maana kila siku kuna thread ya malalamiko ya mtu kupata kipigo cha kifedha...pole sana mkuu
 
Swali la msingi ni kwamba kuna uwezekano wa wewe kurudishiwa hela yako au ndo utakua umepigwa?
 
Ndugu wana jamvi.
Jana saa mbili usiku nimeibiwa shilingi laki mbili na elfu arobaini na tano kwenye namba yangu ya vodacom yenye Mpesa. Fedha zimetolewa kwa wakala, na ujumbe nikaletewa kuwa nimepokea fedha taslimu toka kwa wakala huyo.

Ushahidi huu hapa.
6ES62D6M74W Imethibitishwa tarehe 28/5/19 saa 10:17 PM Pokea kiasi cha Tsh240,000.00 kutoka kwa 430185 - MWANAHAMISI RAJABU ISSA kwa ada ya Tsh5,000.00. Salio lako jipya la M-Pesa ni Tsh675.00.

Cha ajabu ni kuwa muda huo, mimi nilikuwa na simu yangu na sikufanya muamala huu.
Mara moja niliwapigia huduma kwa mteja Mpesa Vodacom ambao wamesema nisubiri masaa 72.
Swali kwa wataalam.
1.Ni nini hasa kimefanyika hadi namba yangu ikatoa fedha nipopajua ilihali simu yangu ninayo?
2. Je nitaweza kupata fedha zangu hizi?
3. Je niendelee kutumia namba hii au niachane nayo?

Nawasilisha.
Simu unayo wewe ,hela inatokaje bila wewe kuitoa?
Kikulacho ki nguoni mwako
 
Elezea vizuri inakuaje?Na voda hawajui ili suala?
Uliza swali sehemu ambayo hujaelewa maana naamini hayo maelezo yamekamilika. Wanalijua ndio maana siku zote tunasisitizwa kutunza namba zetu za siri, watakuwa labda wanalitafutia mwarobaini
 
Back
Top Bottom