Nimegundua mbinu mpya kabisa ya kuzalisha gas ya kupikia pasipo kuisha (Gas Re-recycling)

Anza kuchanga Vicent ili uwe na pesa uje utekeleze hilo uliloita uvumbuzi au tafuta business partner...
 
naombeni wazo la kuhalalisha nifanyeje ili niwape huduma kihalali mlipe na kodi nchi isonge, magumashi sitaki
Kama ni kweli si rahisi kihivyo watu wamepigwa mitama na wajeda ili tu bomba litoke mtwara mpaka dar to bagamoyo halafu leo wasikie kuna mtu mweusi eti anajua kurecycle gas. Utapotea kabla hujasema "mama" ni sawa sawa leo useme kuna majani ukila hayo yanafanya kazi 10 times more than ARVs unadhani kama ni kweli hayo makumpuni yaliyowekeza billions of money kwenye hiyo midawa watakuacha salama.
Kama uvumbuzi wako ni kweli then faidika nao mwenyewe Africa sio sehemu salama.kwa uvumbuzi wa aina yako...Maana hata ukiwauzia watu wawili wa3 upate vijisent ni suala la.muda tu watakujua na utashangaa unapewa kesi ya uhujumu uchumi mhaini utawekewa hadi ngada utapotea and no one will remember you.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mawazo kama haya ndiyo mazuri, je kwa kufanya hivi wenye kampuni hawawezi kunishitki?
Acha woga.Nunua mitungi ya gas.Ifute rangi paka rangi mpya isiyoonyesha gesi ya kampuni Gani.Anza kuuzia marafiki ndugu Na majirani .Ukiona inakubalika kaombe leseni ya kuuza mafuta Na gesi .Omba hati Agiza mitungi yako yenye nembo yako nenda kampuni za gesi kanunue gesi endelea Na maisha yako ya biashara yako omba hati miliki ya Ubuntu wako
 
Mkuu utafungwa kwa kuhujumu biashara ya watu, ni heri hata usingetaja jina la mtungi wa Gasi uliyoiachakachua. Kama ni kweli unachosema nasi nakushauri tafuta brand yako na mitungi yako upige hela kama TMT:)
 
Mwafrika ngozi nyeusi ni shida sana ana roho ya kwanini ni kiumbe wa ajabu sana.
 
Nahisi huyu jamaa analenga kuwafikirisha watu wajiulize inawezekanaje wakija na possibilities au alternatives wakaziandika hapa ndiyo anaanza nazo hizo
 
Nahisi huyu jamaa analenga kuwafikirisha watu wajiulize inawezekanaje wakija na possibilities au alternatives wakaziandika hapa ndiyo anaanza nazo hizo
Yuko kazini huyo wako wengi kama yeye wanaleta hot issue halafu anataka uende PM .kifupi uwe care ku PM
 
Mimi sijakuelewa hata kidogo.Naona Kama unaruka ruka tu.Usikute ulivoamua kujilaza usingizi umekupitia ndio unaota hizi ndoto.Au unamaanisha unaamua kugeuzana huo mwingine kuwa self container ili upate mboji?
 
Watanzania bwana wanapenda sana kujazana ujinga ambao ndiyo mtaji wa CCM kuendelea kutawala nchi yetu.Hivi gesi ni nini na inakuwaje inaisha kwenye mtungu na inakuwaje mtu aamini kwamba mtungi wenyewe unaweza kuzalisha gesi iliyomo ikiisha?

Watu tayari wameshaona jamaa ana bonge la "talent" kwa ivo atadhulumiwa na hawezi "kusaidiwa" na serikali. Ila jamaa ni mtunzi mahiri wa hadithi zihusuzo sayansi. Anaweza kuwa Isaac Asimov wa Tanzania.
Huu msafara sio wa mamba huu naogopa kujongea nao. Njaa sio nzuri mkuu atapasuka utumbo kwa kujaza mitungi huyo kijana. Mshaurini mapema
 
Back
Top Bottom