Nimegundua mbinu mpya kabisa ya kuzalisha gas ya kupikia pasipo kuisha (Gas Re-recycling)

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,284
21,397
Mara ya kwanza ilikuwa kama masihala baada ya gas kuisha nikiwa sina hata tsh kumi mfukoni, niliwaza sana siku hiyo, nikampigia jamaa yangu aniazime japo pesa kidogo bahati mbaya naye hakuwa na kitu kabisa,njaa ilivyozidi kuuma nilirudi tena jikoni nikawasha gas lakini sikufanikiwa ilikuwa imekwisha na mtungi niliunyanyua ulikuwa mwepesi:

Nilirudi kitandani nikasali halafu nikajilaza chali nikitizama darini.

Aisee Lilikuja wazo pale, lilikuwa ni wazo ambalo kama la kipuuzi sana lakini kwa njaa niliokuwa nayo sikuwa na namna niliamua kufanya!

ni wazo ambalo halikuwa na gharama kwasababu kila kitu kilikuwepo,Ni wazo lenye mbinu ya sayansi ya form two, Wala siyo mambo makubwa, Wala hayana mbwembwe kama za Monocotyledon na dicotyledon!

Nilitumia mbinu local kabisa! Gas ilijaa na ule mtungi nikaunyanyua ulikuwa mzito;
nilipikia kwa miezi haikuisha, Mwanzo niliogopa lakini hadi sasa hivi nakaribia mwaka gas haishi, wakati mwanzo kila baada ya miezi miwili nilikuwa najaza (exchange)

Katika kuhakikisha hilo nilinunua mtungi wa kampuni nyingine nikampa mtu atumie hadi iishe halafu anipatie mtungi, nilitumia mbinu ileile kuujaza nao umekubali, Hakika Sijaivujisha mbinu hii kwa mtu yoyote yule.

Nipo hapa natafakari nifanyeje ili nitajirike kupitia ubunifu huu je nitumie njia gani kutengeneza usalama wangu na wa wazo hili ili wenye nguvu wasinitapeli?

Pia Najiuliza vibari vya ubora nitapataje?
Ninapikia kila kitu hadi maharage yanaiva fasta tu.

Naombeni ushauri wenu wadau ili tufanikishe hili, wallah ikitiki tutafurahi wote, naendelea na uvumbuzi zaidi ili kufahamu naweza recycle mara ngapi kabla ya kubadili mtungi mwingine, lakini hadi sasa hivi sijabadili mtungi na gasi imo haiishi karibu mwaka sasa.

Note; Gasi hii naizalisha kwa kutumia mtungi uloisha gas tunayobadili madukani (original.) ya makampuni mbalimbali kama I.e Oryx's, mihan,lake n.k

KARIBUNI WADAU

Nachohitaji kutoka kwenu in ushauri Wa utaratibu za kufanya kihalali na kutengeneza security; kuna watu wanaforce niwaambie sasa sitaweza nikisema kwa MTU si ndiyo tayari nitakuwa nimetoa siri?, shida yangu ni process gani nifanye ili kuondoa magumashi
 
Africa kutoboa itakuwa ndoto za alinacha.

Wazungu wakivumbua wanaweka mambo wazi, ila waafrica wakivumbua wanajifungia chimbani ili wengine wasifaidike.
natafta security ya uvumbuzi Wangu Mkuu, nitautoa tu lakini maslahi yangunitayapaje?
 
Nimesoma sijaelewa mantiki ya hii thread kichwa cha habar na vilivyomo ndani ni toafaut kujisifia na kuilalamikia njaa sasa umefanyaje hadi kuwa na gesi haijulikani kwa nini ufungue thread kama sio muwazi? ndo mana wajinga kama wewe magufuli anawaponda kwa nyundo nzito vichwani.
 
Unachofanya najaribu kama kina wezekana, nisawa uunguze mafuta kama petrol au diesel alfu ufanye recycling yarudi kua mafuta tena.
kaka linaloshindikana kwako halishindikani kwa wote;
 
Ubinafsi, uchoyo ndio silaha kubwa inayomuangamiza maskini.

Kama ni kweli umegundua hilo, uza hiyo Technolojia kwenye makampuni ya Gas.

Nadhani utakuwa bilionea, mwenye hisa kwenye kampuni za Gas utakula Bata milele, vijukuu, kwa vitukuu.
 
Back
Top Bottom