kyanyangwe
JF-Expert Member
- Oct 31, 2018
- 1,147
- 2,746
Last week siku ya tarehe 31 December, nilipanga nifanye tathmini ya aina ya marafiki zangu nilionao. Kiukweli mimi ni mtu wa kujitoa sana when it comes to matatizo ya wenzangu wanaonizunguka, nikisikia msiba wa rafiki ntaubeba kama wetu vile, rafiki akiniomba kitu kama kiko ndani ya uwezo wangu lazima nimsaidie.
Lakini recently kuna viashiria niliviona vikanistua mpaka nikaamua kuwafanyia tathmini marafiki zangu.
So tarehe 31 December 2022, nilijifungia ndani siku nzima, nikaanza kuwapigia rafiki zangu simu kuwaomba msaada kuwa nimepatwa na majanga flani nimetaitiwa na polisi so kuna kiasi flani cha kama elfu 50 kimenipelea hivyo naomba msaada then next day narudisha.
Ebana huwezi amini wale niliokua nawachukulia kama washkaji zangu hakuna hata aliyejigusa na mimi. Ila kuna mdau mmoja tena ni fundi ujenzi nae niliona nimpime coz huwa ananipiga vizinga vya hapa na pale ndiye aliyejitutumua akanitumia elfu 10 akaniambia hiyo nyingine hana nijaribu kucheck wadau wengine.
Na kuna demu mama ntilie nae nilikua nagonga kipindi flani huko nyuma nae akaniwezesha elfu 15, ila hawa washkaji tunaokaa nao kwenye viti virefu hakuna hata aliyeuliza hao polisi wamenitait kwa issue gani!
Kwa kweli hili jambo lilinitafakarisha sana aina ya watu ninaomingle nao katika maisha yangu. Nilichoamua niliblock number zao na kuzifuta kabisa, maana haina haja ya kuendelea kuongozana na watu wa aina hiyo.