Nimefukuzwa kazi leo, kama umeajiriwa jifunze kitu hapa

Pole sana Mkuu!.

Umenikumbusha mbali sana.

2014 kuna nafasi wazi ndani ya ofisi. Tangazo la ndani likapitishwa watu wenye sifa waombe.

Kule ofisini na mikoani waliposikia nimeomba nafasi, wala hakuna hata mmoja mwingine aliyefikisha barua.

Walishajua kuwa wasingetoboa. Uzuri ni kuwa, uwezo wa kila mmoja unajulikana.

Nikaitwa interview na utawala. Nikapiga vema sana, mno.

Nikaambiwa kwa kuwa nipo pekee yangu na nimeridhisha, basi Jumatatu nitapewa barua ya kupandishwa cheo na kuanza majukumu.

Aisee!. Wiki ikapita, ya pili mpaka mwezi. Nikapewa tena taarifa, interview haikuwa rasmi kwa sababu haiwezekani nafasi niombe mwenyewe..

Kwa kuwa hakuna mtu wa ndani aliyeomba, wakatangaza nafasi kwa watu wa nje. Wakachukuliwa tukawa jumla wanne.

Interview walitoa kwa watu wa nje, ila pia management ilikuwepo.

Nilikuwa wa kwanza vivyo hivyo.

Cha ajabu, napewa taarifa sitoweza kushika nafasi husika. Kwa sababu wamepata taarifa kutoka kwa coworkers kwamba nilitishia kufukuza wafanyakazi watakaodiriki kushindana nami kwenye kuomba nafasi.

Wakaona soo kunitimua. Nikatolewa HQ na kuhamishiwa mkoani, tena katika nafasi ya chini kabisa. Jamaa wa nje akapewa nafasi.

Nikapotezea na kuhamia mikoani. Nikaendeleza kwata. Kule ofisini (kitengo nilichokuwa) mambo yaliwazidi. Miezi miwili tu napaewa barua ya kurushishwa HQ. Jamaa naye aliyepata nafasi haridhishi.

Narudi HQ, miezi minne hali si nzuri. Jamaa akasitishiwa mkataba. Nikachukua nafasi.

Usihuzunike Mkuu. Uwezo na bidii yako vitakutetea.

Mungu akubariki.
 
My name is Amicus Curiae, a very prominent lawyer in the Capital City of .......

Nilifika pale ofisini mapema sana miaka kadhaa iliyopita wakati ofisi iko kwenye kipindi kigumu, nikaishi nao hivyohivyo tena kwa upendo, nikawafundisha kazi makumi ya Wanasheria (Mawakili), wakafanikiwa na wengine hawakuaga baada ya kuona mafanikio, boss akawa anawanung'unikia kwangu.

Boss wangu akawa amefanya mambo makubwa sana lakini kipindi hicho kilikuwa kipindi cha nyuma mno. Nikaiga mambo yaleyale ya boss akanisifia yeye mwenyewe na kwa wengine ofisini.

Kumbe mule ndani ofisini watu wakawa wananionea wivu ila ukikutana nao wanakuchekeaaaa... (jamani unafiki upo).

Nikawa nafanya kazi zote zenye malipo makubwa ofisini huku kwa upendo nikiwapa kazi za kunisaidia sambamba na fedha kwa vijana wote pale ofisini ili na wenyewe wapate pesa za kujikimu.

Kumbe roho inawauma. Juzijuzi bila mimi kujua wakapanga njama kwamba nifukuzwe ili wao ndiyo waonekane. Yale yote niliyokuwa nawashirikisha kwa upendo wakayaweka bayana. Boss pamoja na kuniamini akawaamini wao zaidi na kinifukuza kwasababu alishapandikizwa sumu kali sana.

Jamani don't trust anyone. Nakumbuka niliitwa kwenye ofisi ya hasimu (mpinzani) wa ofisi ya boss wangu mara mbili ili niiodhoofishe ofisi ya boss wangu ila nikakataa. Siku niliyoenda kukataa hiyo offer nilikuwa na huyo mtu wa ofisini aliyenichafua, kumbe yeye ndiye aliyefanya yote hadi kufikia hapa nilipo.

Leo nimefukuzwa, HAKUNA ALIYENIPIGIA SIMU HATA YA KINAFKI KUNIPA POLE.

Jamani ukijiona una kitu cha PEKEE kinachopendwa na boss wako jihadhari na hao mashost au mabest wa ofisini, utaula wa chuya.

Nimewasamehe wote and I am moving on.

Mungu na wanadamu. Naomba kubakia. Amen.
Sasa wewe ni wakili senior,muda wote huo unapata hela umeshindwa au unashindwa kufungua firm yako na kuchukua wateja wako toka kwa huyo bazazi aliekufukuza na mambo yakaenda?hebu acha kulia lia mitandaoni,ni aibu sana kwa wakili kama wewe but pole kwa kufukuzwa Kazi
 
Connection ni nyingi mno mkuu..
Msomi rafiki wa mahakama....hizi ni changamoto ambazo utazivuka tu mkuu.

Mimi pia nilipata situation moja ktk firm niliyokuwepo mambo yakavurugika...ila mpaka leo things are moving on.

Utashinda...Mungu na akuvushe. Badala ya kuwakasirikia hao waliokuchoma..wewe mshukuru Mungu. Fanya maombi ya sifa na shukrani kwa Mungu.

Adui yako siyo hao wafitini hapo ofisini bali aduo yako halisi ni roho iliyo nyuma yao hao waliokufitini...nguvu za giza, roho wachafu. Hawa ndiyo wako nyuma ya waliokufitini...lengo ni kukuharibia ili imani yako kwa Mungu ijaribiwe. Stand firm, do not waver. Mungu atakupigania.
 
Amen mkuu wangu.
 
My name is Amicus Curiae, a very prominent lawyer in the Capital City of .......

Nilifika pale ofisini mapema sana miaka kadhaa iliyopita wakati ofisi iko kwenye kipindi kigumu, nikaishi nao hivyohivyo tena kwa upendo, nikawafundisha kazi makumi ya Wanasheria (Mawakili), wakafanikiwa na wengine hawakuaga baada ya kuona mafanikio, boss akawa anawanung'unikia kwangu.

Boss wangu akawa amefanya mambo makubwa sana lakini kipindi hicho kilikuwa kipindi cha nyuma mno. Nikaiga mambo yaleyale ya boss akanisifia yeye mwenyewe na kwa wengine ofisini.

Kumbe mule ndani ofisini watu wakawa wananionea wivu ila ukikutana nao wanakuchekeaaaa... (jamani unafiki upo).

Nikawa nafanya kazi zote zenye malipo makubwa ofisini huku kwa upendo nikiwapa kazi za kunisaidia sambamba na fedha kwa vijana wote pale ofisini ili na wenyewe wapate pesa za kujikimu.

Kumbe roho inawauma. Juzijuzi bila mimi kujua wakapanga njama kwamba nifukuzwe ili wao ndiyo waonekane. Yale yote niliyokuwa nawashirikisha kwa upendo wakayaweka bayana. Boss pamoja na kuniamini akawaamini wao zaidi na kinifukuza kwasababu alishapandikizwa sumu kali sana.

Jamani don't trust anyone. Nakumbuka niliitwa kwenye ofisi ya hasimu (mpinzani) wa ofisi ya boss wangu mara mbili ili niiodhoofishe ofisi ya boss wangu ila nikakataa. Siku niliyoenda kukataa hiyo offer nilikuwa na huyo mtu wa ofisini aliyenichafua, kumbe yeye ndiye aliyefanya yote hadi kufikia hapa nilipo.

Leo nimefukuzwa, HAKUNA ALIYENIPIGIA SIMU HATA YA KINAFKI KUNIPA POLE.

Jamani ukijiona una kitu cha PEKEE kinachopendwa na boss wako jihadhari na hao mashost au mabest wa ofisini, utaula wa chuya.

Nimewasamehe wote and I am moving on.

Mungu na wanadamu. Naomba kubakia. Amen.
Pole mi mwenyewe nilishapataga mtihan km huo ,hakuna hata mmoja alotuma sms ya pole hata ya kinafik,tena yule ambae nilikua department nae moja na lift alikua akinipa mara kwa mara ,lakin Kuna kipind nilikua nikipishana nae Yuko kwny pikpik yake hata salaam hakuna,nam nikawapotezeaga mazima na mkoa nikahama,sasa mwaka juz nkapigiwa cm na jiran yng wa uko ,akanambia fulan amejiua kwa kujinyonga ,Wala ckusikitika Wala kufurah ,nikamwambia okay,nkaendelea na mambo yng,rafik wa kwel Yesu ndugu yangu wa kweli mwanangu, that's my slogan tangu nifukuzwe Kaz nilijifunza kuiangalia dunia kwa namna hiyo,
 
Pole mkuu, rafiki ako mkubwa ndio adui yakk mkubwa

Sent using Jamii Forums mobile app
Marafiki katika maisha hawatabiliki kamwe.

Falsafa ya BOB inasema hivi

"Your worst enemy could be your best friend, and your best friend your worst enemy." - Bob Marley

Ufikapo wakati sahihi, kial lafiki hujiweka bayana, Ni kama shilingi ilivyo na pande mbili, Ndugu yetu kaonyeshwa upande mmoja wa shilingi.

Rejea
- Who The Cap Fit (1976) - Bob Marley & The Wailers

Back
Top Bottom