Nimefukuzwa kazi leo, kama umeajiriwa jifunze kitu hapa

Amicus Curiae

JF-Expert Member
Sep 12, 2012
4,809
6,342
My name is Amicus Curiae, a very prominent lawyer in ..... City.

Nilifika pale ofisini mapema sana miaka kadhaa iliyopita wakati ofisi iko kwenye kipindi kigumu, nikaishi nao hivyohivyo tena kwa upendo, nikawafundisha kazi makumi ya Wanasheria (Mawakili), wakafanikiwa na wengine hawakuaga baada ya kuona mafanikio, boss akawa anawanung'unikia kwangu.

Boss wangu akawa amefanya mambo makubwa sana lakini kipindi hicho kilikuwa kipindi cha nyuma mno. Nikaiga mambo yaleyale ya boss akanisifia yeye mwenyewe na kwa wengine ofisini.

Kumbe mule ndani ofisini watu wakawa wananionea wivu ila ukikutana nao wanakuchekeaaaa... (jamani unafiki upo).

Nikawa nafanya kazi zote zenye malipo makubwa ofisini huku kwa upendo nikiwapa kazi za kunisaidia sambamba na fedha kwa vijana wote pale ofisini ili na wenyewe wapate pesa za kujikimu.

Kumbe roho inawauma. Juzijuzi bila mimi kujua wakapanga njama kwamba nifukuzwe ili wao ndiyo waonekane. Yale yote niliyokuwa nawashirikisha kwa upendo wakayaweka bayana. Boss pamoja na kuniamini akawaamini wao zaidi na kinifukuza kwasababu alishapandikizwa sumu kali sana.

Jamani don't trust anyone. Nakumbuka niliitwa kwenye ofisi ya hasimu (mpinzani) wa ofisi ya boss wangu mara mbili ili niiodhoofishe ofisi ya boss wangu ila nikakataa. Siku niliyoenda kukataa hiyo offer nilikuwa na huyo mtu wa ofisini aliyenichafua, kumbe yeye ndiye aliyefanya yote hadi kufikia hapa nilipo.

Leo nimefukuzwa, HAKUNA ALIYENIPIGIA SIMU HATA YA KINAFKI KUNIPA POLE.

Jamani ukijiona una kitu cha PEKEE kinachopendwa na boss wako jihadhari na hao mashost au mabest wa ofisini, utaula wa chuya.

Nimewasamehe wote and I am moving on.

Mungu na wanadamu. Naomba kubakia. Amen.
 
Wahi ajira nyingine kama bado huna uwezo wa kuwa business owner

 
Nilipata zabuni kubwa ya kutoa service kampuni X. Iliyo kuwa chini ya uongozi wa wahindi na mzungu.

Wakamleta kijana wa kihindi tumfundishe kazi mimi na jamaa yangu niliyemleta tusaidiane kazi.
Muhindi alipojua kuchokonoa mifumo kidogo tukapewa barua ya kusitishiwa mkataba.

Siku ya tatu tukaitwa tena na baada ya miezi miwili tukatemwa mazima na barua zetu za bonus na kusitishiwa mkataba tena.

Simfundishi kazi muhindi labda awe mtoto wa baba yangu wa nje ya ndoa.
 
Back
Top Bottom