Spika Dkt. Tulia, (Watu Wangu 10 Bora nilioikutana nao live nakuonyesha upendo mkubwa)

conductor

JF-Expert Member
May 29, 2013
718
570
Ukibahatika kukutana na Mh.Dr.Akson Tulia ofisini kwake, Ni mkalimu Sana,msikilizaji mzuri, mwenye upendo unaoonekana kabisa.

Nilikutana nae mwaka jana ofisin kwake jijin Dodoma, licha ya ugumu kupata nafasi hiyo kwa walio wengi,Sehem za kukaguliwa tu nikama 4. hivi (vua mkanda,Saa,kama una siraha weka pale,kitamburisho nk), utaswet sana kumfikia mh.

Ila sasa ukivuka "very humble enough to feel FREEDOM " ana smile,anakupa uwanja wa kujieleze,anashare nawe anachotaka kujua. Pia unaona kabisa ni mzaz,na Mwalimu by nature.

Sio mnafiki hata kidogo.shida sasa iko huku kwa wanamugambo na CHAWA wake shida tupu. Vijana wake wapiga picha pia unaoona kabisa walivyo happy kufanya ofisi nae.(sasa kimbembe kutana na hao wabunge WA kawaida na CEO wa makampuni ya umma utadhan ndo DR.TULIA sasa wanajivuta Sana.

Lakinie pia tembelea TULIA TRUST kule Mbeya yule dada manager, afisa Mahusiano na Mzee wa busara Bwana MORISI utapenda Sana.(moyoni niliwaza sana kumbe kuna watu wazuri TZ tena wenye uelewa mkubwa na UPENDO.

2. Manager Mmoja wa kike NBC _HQ floor ya pili .
Ukiingia pia unapata tabu kweli kupata kibari cha kuonana nae, nilisubir masaa kadhaa ili kupata kibari mpaka ujielezee pale mapokez kama una appointment,una barua wakati mwingine onyesha kitamburisho na passport.(wanathan hawataki usionane na boss wao) nia yangu ni kuonana na mkurugenz mkuu ila wakaamua kunielekeza kwake, ukiingia tu ana sura sio rafik niya kujihami flani hivi hasa akiona we ni jinsia ingine, ila mkianza kuongea na anavuojitoa kusaidia na kuelekeza namna ya kufanikisha hakika utaenjoy uduma yake kiofisi.

3. V.C UDSM
Ahaaa! Utapenda sana argument zake ila sasa pale reception kuna wamama umri umesogea nao utata sasa, nilipoongea kifaransa nadhan walioona hatutaelewana ndo nikaonana nae. Nilipenda sana alivyo organised .

4. Prof.KAMUZOLA
Aisee licha ya umri kwenda lakin unaoona namna anavyotaka ufanikiwe katika swala lako, na atakupa njia mbadala kwenda mbele.(smart enough).

5.Mwanasheria mmoja Yuko Pale wizara ya michezo Mfupi hivi mweusi (uwanja wa Mkapa)
Nimewahi kumshawishi aache ile Ajira nimpeleke nje ya nchi awe CEO, kama wakenya walivyozagaa Tanzania.

Nilimjua baada ya dada mmoja anasura ya kimasai pale mzito sana kuamua analamika sana, afu yuko slow sikuonaga hata tabasam yake kwa trip zote pale, sasa documents zangu zilipofika kwa yule bwana alioonyesha kukerwa na kulimbikiza file, anasema kinachowezeka kimalizike leo pamoja na DR.SINGO walioonyesha maana ya kuongoza

5. Reception pale ofis za Emirates Posta yuko dada mmoja mzur (manager sio mtz nilivyomuoona)nilitaka kupata ufafanuzi baada ya kuhairisha safar yangu. Unapata hamu ya kutumia uduma zao .

6.MR. D.KWAY pale PEPS HQ, manager sijuh shule yake lakini ningekuwa mshauri WA RAISI yule jamaa ningempa aende TTCL kama marketing director nawaambia watu wataama TIGO,VODA, AIRTEL nk. Maana yule bwana kwanza anapenda staff wenzake, unaoona anavyosikitishwa na wafanyakaz au viongoz wabinafs na wasiopenda nchi yao. Ipo siku nitashaur mifumo ione ubora wake sio kama mabos zake.

7.(US EMBASSY & RWANDA). they are good in communication skill and diplomatic.

8.Afisa police usalama barabaran kile kituo kilicho karibu na UBALOZI wa USA, jamaa mweusi,mfupi ana rafudh kama Waha ni baada ya kubishana na police huko barabarani, nikasema twende kwa boss wako nipate maelezo mazuri jamaa nilioona ameiva katika kusoma saikolojia za watu. Sio kila kitu utumie sheria wakati mwingine vaa uhalisia kama ungekuwa wewe?. Inatosha kujipa namna ya kukabiliana na hoja ya mteja.

9. Walinzi wote walioko kwenye gate kubwa uwanja wa Mkapa.JKT

10. MANAGER wa MAWASILIANO AKIBA COMMERCIAL BANK.hq.karibu na Serena hotel na CRDB HQ Posta salute kwenu..yenye kujua maana ya kupokea WATEJA.

B. Watu 5 ambao sitak kabisa kukutana nao hata kama ni mgonjwa Wangu simpeleki Bora afe

1. Kanali Mbuge ahaaa sitasahau nisema Tu damu hazikuivana (nadhani ni mwanajeshi huyu mwamba).ningekuwa kiongoz nampeleka anakuwa mlinzi wa magereza Tu atakapo foka non stop na kuamin nje ya argument.

2. Mkata maji wa DAWASCO receptionist wao anafanya KAZI kutokea ofisi zilizoko karibu na CHUO KIKUU cha ardh.mdada hivi mweupe dah shida Sana usipokuwa makini unaweza kuta umemtemea mate.

3. Wapiga picha wote dsm kwenye parking za maegesho au magari dah, yaan ukitoka nje tu kunua maji au vocha tayari kasha vaa gar lako na kurekodi afu woote madhan wanafana tabia utadhan una stress muda wote.

4. Jamaa mmoja yuko clouds TV,Mweusi hivi mrefu kiasi anajihusisha na michezo anadharau kishenz sijuh ndo boss wa ndondo yule nimewahi ona akitoa maelekezo ya zawadi KUHUSU ndondo.

5. KAMPUNI ya Airtel na Kula bando ukienda kuuliza wakupe sababu .dah utadhan wanafurahia matatizo yako.
 
Namba 5 ndio umeharibu,huu mwandiko ndio umfanye mtumishi aache kazi yake umpe u CEO nchi za watu,pathetic
 
Huu uzi unahusisha customer care. Umeongelea pepsi ila kuna jamaa mmoja namuhifadh jina nadhan ni area sales manager wa upande wa goba unaenda mwezi wa nne nahitaj fridge had leo bila bila. Ubaya ata ukimpigia simu hakumbuk kabisa inabid uanze mwanzo. Hadi nimekata upepo
 
Ukimaliza kupata huduma, mpatie appreciation, mwambie ahsante kwa huduma nzuri, nmeridhika!
 
Kweli airtel ni ovyo kipeo cha saba.

Na hilo linachochewa na wafanya kazi wa kampuni.. Ni watu wasiojali lolote wala chochote.
 
Ukibahatika kukutana na Mh.Dr.Akson Tulia ofisini kwake, Ni mkalimu Sana,msikilizaji mzuri, mwenye upendo unaoonekana kabisa...
Ulichoandika inaonyesha kweli umeyaishi na kukutana nayo unakila sababu ya kuaminika! I wish uliowa endorse wasome huu Uzi ili waongeze morali ya kazi!
 
Back
Top Bottom