Nimefiwa...

Nimefiwa...

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
10,702
Reaction score
3,345
...na mtoto wa dada yangu, yaani mjomba'angu, if you know what am I saying. Marehemu aliitwa Nelasi, binti wa miaka 10, mwanafunzi wa Shule ya Msingi Elu, Morogoro, aliumwa ghafla ugonjwa kama degedege (nina hakika sio), akalazwa zahanati ya Chuo Kikuu Mzumbe kwa siku kadhaa, jana akahamishiwa Hospitali ya Manispaa Morogoro, ambako mauti yalimfika majira ya saa 10 jioni, takribani saa moja baada ya kufikishwa hapo. Msiba uko Chuo Kikuu Mzumbe, nyumbani kwa wazazi wa marehemu.
Alfajiri nitaanza safari ya kwenda huko... BWANA AMETOA, BWANA AMETWAA. JINA LAKE LIHIMIDIWE!
 
Masikini Nelasi... RIP.
Pole sana pal, Mungu akuzidishie nguvu
Wafikishie wazaxi wa marhem pole zetu.
 
Pole sana mkuu, kazi ya mola haina makosa kuwa na imani kuwa siku yake imefika na ucmulilie au kumuuliza mungu kwa nini kaamua kufanya hivyo kwa kiyi ya mungu haina makosa huenda kuna baya zaid ya hilo kaepusha huko mbele.Mngu akutie nguvu, akupe ujasiri na hekima ktk kipindi hiki kigumu kwako
 
Pole kaka....
Nawaombea faraja ya Mungu....
Wape pole wafiwa wote na ufike salama
 
Mungu awape moyo wa ujasiri ktk kipindi hk kigumu. Marehemu apumzike kwa amani, AMEN.
 
poleni sana Mphamvu..binti alikuwa bado mdogo mungu amwepe pema peponi
 
Pole Mkuu Mphamvu, nifikishie salamu zangu za pole kwa wazazi wa Marehemu...
R.I.P Nelasi..
 
Pole mkuu, masikini Nelasi katutoka bado mbichi!
Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu...........amina
 
Back
Top Bottom