Mphamvu
JF-Expert Member
- Jan 28, 2011
- 10,702
- 3,351
Kwema wapendwa? Kutokana na malalamiko ya baadhi ya members kuhusu avatar yangu, nimeamua kuchukua maamuzi ambayo ninadhani ni sahihi kwa mustakabali wangu na mustakabali wa JF kwa ujumla. Baadhi ya members ambao wamekuwa wakilalamika ni pamoja na Mpevu, FaizaFoxy na wengine wengi just to mention the few... Kumekuwa na malalamiko kuwa avatar yangu inadhalilisha utu wa mwanamke. Utetezi wangu kuhusu hoja hii ni kuwa mimi ni mfuasi wa Nadharia ya Mtazamo-Kike ya Kiafrika (African Feminism), hivyo avatar yangu ni sehemu ya yale ninayoyaamini. Nikilinganisha na hisia za walio wengi humu jamvini, nimeona kuwa utetezi huu si kitu na hivyo nimeamua kuutupilia mbali. Dai la pili ni kuwa kumekuwa na mkanganyiko kati ya jinsi yangu na picha iliyo kwenye avatar hiyo, wadau kadhaa wamekuwa wakihoji jinsi yangu, huku wengine wakidhani kuwa mimi ni msichana, kitu ambacho si kweli. Ili kuondoa mkanganyiko huo, nimeamua kutekeleza azma yangu ambayo nimeisema hapo juu...
Hoja hizi mbili, zimenisukuma kubadili avatar yangu na kuweka hii munayoiona sasa. Natumai wale niliowakwaza na avatar yangu ya mwanzo mmenisamehe...
Nawatakia msheherekeo mwema wa avatar yangu mpya!:welcome:
Hoja hizi mbili, zimenisukuma kubadili avatar yangu na kuweka hii munayoiona sasa. Natumai wale niliowakwaza na avatar yangu ya mwanzo mmenisamehe...
Nawatakia msheherekeo mwema wa avatar yangu mpya!:welcome: