Chief Godlove akimbia na akaunti za msanii wake

Best home tutor

Senior Member
Joined
May 8, 2026
Posts
194
Reaction score
268
Msanii wa rap Bongo, Scorpion (Tgun Tozzy) ameeleza malalamiko yake akidai kuwa Chief Godlove amekimbia na chaneli yake ya YouTube huku akikataa kumpa mkataba wa lebo kama walivyokubaliana!.

"Barua ya wazi kwa tajiri Chief Godlove. Nimeamua kutumia njia hii kukufikishia ujumbe huu kwani WhatsApp na Instagram sikuoni (umeniblock). Kwanza nakushukuru kwa nafasi na muda uliowekeza katika safari yangu ya muziki kwa hilo Mungu akubariki."

"Tulianza kwa maono makubwa na makubaliano kwamba tungejenga brand yangu pamoja. Kwa kuamini maono hayo, nilikubali kukabidhi usimamizi wa akaunti zangu za mitandao ya kijamii na kufanya maamuzi makubwa si kwaajili ya maisha yangu tu pia kwaajili ya mkoa wangu (Rukwa) Sumbawanga."

"Lakini pia YouTube channel yangu ilihamishwa kwenye email bila idhini yangu kwa ahadi kwamba iko sehemu salama. Lakini baadaye mambo yalibadilika. Muda wa kusaini mkataba ulipofika, mawasiliano yakawa tofauti na hatimaye ukapost mtandaoni kuwa mimi sihusiani na label bali unanisopport tu."

"Nilipouliza uliniambia niendelee na kazi na nisingeweza kuendelea na kazi pasipo mkataba, niliomba kurejeshewa YouTube channel yangu sikupata majibu hatimae uliniblock."

"Leo sina ombi lingine zaidi ya kuomba YouTube channel yangu irejeshwe kwenye email yangu. Nilitengeneza imani kubwa kwa mashabiki zangu walio subscribe channel yangu ili kuni support. Biashara si uadui. Wakati mwingine ushirikiano unaweza kushindikana kwa sababu mbalimbali."

"Lakini naamini kila jambo linaweza kumalizika kwa amani, heshima na haki kwa kila upande. Mimi sina mali, sina nguvu sina Baba, sina Mama, wala uwezo wa kushindana na mtu yeyote. Nilichonacho ni ndoto yangu, kazi yangu na imani yangu kwa Mungu. Kwa heshima kubwa, naomba unirudishie YouTube channel yangu kwani haina kazi yoyote tuliyo fanya pamoja. Mungu akubariki. Tgun Tozzy" - Scorpion.
 
Yule chief mmbangaizaji tu hana lolote, msiamini maisha ya mitandaoni ! Ona sasa msanii wa watu yamemkuta !
Kabisa ,watu wanachizika na maisha ya waigizaji content creators ,kipindi kile Chief anaigiza na misafara na majumba ya maghorofa nilikuwa naona kabisa jamaa ni msanii ,nyumba aliyekuwa anajifanya yake hadi mwenyewe namjua ,ila wengi kawapiga pesa kwa jicho la tatu.
 
Tajiri anang'ang'ania channel ya youtube? Hahaaaa
 
Kabisa ,watu wanachizika na maisha ya waigizaji content creators ,kipindi kile Chief anaigiza na misafara na majumba ya maghorofa nilikuwa naona kabisa jamaa ni msanii ,nyumba aliyekuwa anajifanya yake hadi mwenyewe namjua ,ila wengi kawapiga pesa kwa jicho la tatu.
Bongolala kuna wjng wengi sana na kamwe hawatoisha

Ova
 
Back
Top Bottom